24/07/2025
Alikuwepo kijana maskini aliyekuwa akitembeza maua kwenye barabara kuu. Siku moja mzee mmoja alimsimamisha na kumwambia.
"Kwanini unauza maua kwenye barabara iliyojaa magari ambayo yanahatarisha maisha yako?"
Yule mvulana akamjibu. "Familia yangu ni maskini haimudu gharama za kunisomesha."
Yule mzee akamwambia. "Lakini unakosea kijana. Unahatarisha sana maisha yako unapokimbizana humu barabarani. Je, unatambua kuwa unaweza kugongwa na gari?"
Yule mvulana akamweleza kwa sauti ya chini. "Ninahitaji kutengeneza pesa ili niweze kurudi shuleni"
Yule mzee akapiga makofi kwa mshangao na kumwambia. "Lakini maisha yako ni muhimu kuliko elimu. Watu wengi sana hawakwenda shule lakini waliishia kuwa watu wakuu sana. unaenda kufa eti kwasababu unataka kuelimika? Sasa nikwambie kitu, ukigongwa na gari utakufa, na ukifa, hakutakuwepo elimu tena kwaajili yako. Unanielewa?
Tena yule mzee akaongeza. " Elimu sio ufunguo wa mafanikio. Usihatarishe maisha yako kwaajili yake."
Yule mvulana maskini akawaza sana juu ya maneno ya yule mzee huku akimtazama akiyoyoma. Kwa siku kadhaa aliwaza na kuwazua hadi akaamua kutouza maua tena.
Miaka kumi na mitano baadae, yule mvulana alikua na kuwa kijana mdogo na alikuwa maskini bila hata ya kuwa na chanzo cha kipato. Siku moja, alikutana na mzee mmoja na kumuomba msaada.
"Samahani baba, unaweza kunipa msaada wa pesa hata kidogo?"
Yule mzee akafura. "Kha! Kwanini hukusoma ili uweze kujisaidia?"
Yule kijana akamjibu, "Wazazi wangu walikuwa maskini, hawakuweza kunisomesha"
Yule mzee akaropoka kwa sauti. "Usiwalaumu wazazi wako. Watu wengi walifanya kazi kwa bidii sana na kuhatarisha maisha yao k**a watoto wadogo ili waweze kulipia gharama za shule, kwasababu walitambua umuhimu wa elimu. Ila wewe hukufanya chochote, hivyo huu ni uzembe wako na kosa lako!"
Yule kijana alijisikia kuumizwa sana na kuvunjika moyo kutokana na maneno ya yule baba. Na zaidi vile alivyokuwa anamkumbuka kuwa ni mtu huyo huyo aliyekutana nae miaka kumi na tano iliy