Olive Health n Nutrition Clinics

  • Home
  • Olive Health n Nutrition Clinics

Olive Health n Nutrition Clinics HEALTH WELLNESS & NUTRITION

OLIVE HERBAL 'N' NUTRITION CLINIC with DR MWANGI For more information call0714366766 or 0101401678
24/01/2022

OLIVE HERBAL 'N' NUTRITION CLINIC with DR MWANGI

For more information call

0714366766 or 0101401678

22/01/2022
20/11/2021
18/11/2021
SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA NA TIBA ZAKETatizo la kutopata mimba linawasumbua wengi na huwapata familia kadhaa ka...
16/11/2021

SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA NA TIBA ZAKE

Tatizo la kutopata mimba linawasumbua wengi na huwapata familia kadhaa katika jamii, huweza kumpata mtu mmoja kati ya wanandoa 12 na ni tatizo linalowapata watu zaidi ya milioni 24 duniani kote.

Ugumba ni hali ya kutoweza kupata ujauzito katika kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya mapenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango. Mtiririko wa upataji ujauzito ni k**a ifuatavyo;

Baada ya mwezi mmoja wa ndoa uwezo wa kushika ujauzito ni asilimia 20, baada ya miezi mitatu ya ndoa ni asilimia 50, baada ya miezi sita ya ndoa ni asilimia 75 na baada ya miezi 12 ni asilimia 90 mwanamke huweza kupata ujauzito.

Hali hii inaweza kutokea kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke, ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakidhani wanawake peke yao ndio ambao hupata tatizo hilo.

Tatizo hili limegawanywa katika vipengele viwili kimoja ni kile ambacho mwanamke hushindwa kupata mimba baada ya mwaka mmoja wa kufanya tendo la ndoa na mume wake bila kutumia kinga kwa mwanamke mwenye umri chini ya miaka 35 (primary infertility).

Kipengele cha pili ni kile kijulikanacho k**a 'secondary infertility' ambapo mwanamke hushindwa kubeba mimba wakati siku za nyuma alishawahi kupata ujauzito.

Tatizo la ugumba huweza kupatiwa matibabu na kuisha.

KUNA TAFAUTI GANI KATI YA UGUMBA NA UTASA?

Tofauti na ugumba, utasa ni hali ya mwanamke kutoweza kushika ujauzito kabisa au mwanaume kutoweza kusababisha ujauzito kwa mwanamke kabisa.

Mtu tasa hana uwezo wa kupata mimba au kumpa mwenzi wake mimba kabisa, wakati mgumba ana uwezo wa kuja kupata mimba iwapo tatizo litaondolewa.

NINI HUSABABISHA UGUMBA?

Kuna sababu mbalimbali ambazo hupelekea ugumba kutokea kwa mwanaume au mwanamke.

WANAUME
Ugumba kwa wanaume hutokana na tatizo katika mbegu za kiume, manii kuwa kidogo, manii kushindwa kutembea, manii kuwa na umbo lisislo la kawaida au kuziba kwa mijira ya mbegu za kiume.

Tatizo kwenye mbegu za kiume linaweza kutokana na;

- Uvutaji wa sigara
- Dawa za kulevya k**a matumizi ya bangi kwa wingi,
- Mionzi (radiations)
- Unywaji wa pombe
- Kemikali k**a DDT, risasi (lead)
- Kufanya kazi mazingira yenye joto kali k**a viwanda vya chuma.
- Kuziba kwa mirija ya mbegu za kiume kutokana na magonjwa ya zinaa

WANAWAKE
Tatizo la ugumba husababishwa na sababu kuu mbili:

- Kuziba kwa mijrija ya kupitisha mayai
- Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi au kutoa mayai isiokuwa na nguvu (lazy egg).

Mirija ya kupitisha mayai inaweza kuziba kutokana na;

- Ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambao unatokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa k**a kisonono na klamidia.
- Mirija ya mayai kujaa maji
- Utoaji mimba usio salama (unsafe abortions)
- Upasuaji maeneo ya kiunoni
- Ugonjwa wa endometriosis

Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi inaweza kutokana na;

- Umri mkubwa wa mwanamke, hasa miaka 35 – 40 na kuendelea.
- Uvutaji wa sigara
- Saratani ya Ovari
- Mionzi (radiations)
- Ugonjwa wa Polycystic ovarian disease (Ovarian Cyst)

Sababu nyingine za ugumba kwa mwanamke zinaweza kuwa;

- Makovu katika mji wa uzazi kutokana na kutoa mimba.
- Mabonge ya kizazi (uterine fibroids)
- Kuziba kwa shingo ya uzazi
- Kulegea shingo ya uzazi
- Kisukari
- Matatizo ya tezi ya shingo (hyperthyroidism)
- Kufanya mazoezi ya kupitiliza (excessive exercising)

VIPIMO VYA KUJUA UGUMBA

Vipimo mbalimbali vinapatikana ili kuwezesha kugundua chanzo cha ugumba. Licha ya uwezo wa vipimo hivi, zaidi ya asilimia 10 ya watu wenye tatizo hili chanzo kinaweza kisijulikane kabisa. Ni vizuri kwa wenzi wote wawili wenye tatizo hili kuonana na daktari kwa ajili ya ushauri na vipimo.

KWA WANAUME HUFANYIKA;

Kipimo cha manii (seminalysis) kuona k**a manii zipo za kawaida na kwa kiwango kinachoatakiwa. Manii huchukuliwa kwa kondomu maalum wakati wa kufanya mapenzi au kwa kupiga punyeto na kisha kuchunguzwa kwa darubini.

Homoni za kiume kwenye damu; kipimo hiki hupima homoni za testosterone na Follicle Stimulating Hormone(FSH) ambazo huusika katika utengenezaji wa mbegu za kiume.

KWA WANAWAKE KUNA VIPIMO VINGI HUWEZA KUFANYIKA VIKIWEMO;

- Hysterosalpingography – hutazama mirija ya uzazi (Fallopian tubes) k**a imeziba au la. Pia huonesha k**a tumbo la uzazi lina vivimbe.

- Ultrasound – kipimo hiki huonesha k**a kuna vivimbe kwenye tumbo la uzazi, pia kwenye ovari k**a kuna magonjwa yanayoweza kusababisha ugumba k**a Polycystic Ovarian Syndrome.

- Homoni za k**e katika damu – kipimo hiki hupima homoni za 'Oestrogen' na 'Follicle stimulating hormone' ambazo huusika kwenye kuandaa yai la uzazi kutoka kwenye ovari na upandikizaji kwenye mji wa uzazi.

- Endometrial biopsy – tishu za mji wa uzazi huchukuliwa kuchunguza k**a yai la uzazi limetoka. Pia huweza kuonesha k**a kuna saratani ya mji wa uzazi au vinyama kwenye mji wa uzazi.

MATIBABU YA UGUMBA

Matibabu ya ugumba huhusishwa wenzi wote wawili, mwanaume na mwanamke. Yanahitaji uvumilivu na uelewa kwani wakati mwingine yanaweza yasiwe na mafanikio haraka au kabisa k**a tunavyotarajia. Kuna njia mbalimbali za kutibu ugumba, hizi zote zikijumuisha kuondoa tatizo linalosababisha mimba ishindwe kutunga au kutumia njia za kusaidia mimba itunge.

Njia za matibabu ya ugumba hujumuisha:

UPASUAJI
Mirija iliyoziba, vivimbe kwenye mji wa uzazi au kuta za uzazi kushik**ana huweza kutibiwa kwa njia za upasuaji. Matibabu haya husaidia kuongeza uwezekano wa wenzi kupata mtoto.

DAWA
Mirija iliyoziba, vivimbe kwenye mji wa uzazi au kuta za uzazi kushik**ana huweza pia kutibiwa kwa Dawa mara nyingine. Matatizo ya ugumba yanayotokana na ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi huweza kutibiwa kwa dawa pia. Dawa hizi hutumika kuziwezesha ovari kutoa mayai ya uzazi ili yawe tayari kurutubishwa. Mara nyingi huweza kusababisha kutoa mayai mengi katika mzunguko mmoja na kusababisha ujauzito wa watoto wengi (mapacha au zaidi) pale yanaporutubishwa.

TEKNILOGIA SAIDIZI ZA UZAZI (Assistive Reproductive Technologies).

Hizi ni njia za kitaalamu ambazo zinatumika kusaidia wenzi kupata ujauzito kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke. Njia hizi ni k**a 'Artificial Insermination' na 'In Vitro Fertilization'.

- Artificial Insermination; Njia hii hutumika pale ambapo mbegu za kiume zipo kwa kiasi kidogo. Mbegu za kiume hukusanywa na kuingizwa kwenye mji wa uzazi kwa njia za kitaalamu.

- In Vitro Fertilization; Njia hii hutumika hasa pale mirija ya mwanamke imeziba kabisa. Mayai na mbegu za kiume hukusanywa kitaaalamu na kisha yai kuchavushwa. Baada ya hapo yai lililochavushwa hupandikizwa kwenye mji wa uzazi.

Ugumba huathiri wanaume kwa wanawake wa kiwango kinachofanana, hivyo ni muhimu kwa wenzi wote wawili kushiriki katika matibabu.

Ugumba huathiri wenzi wengi kisaikolojia kwa kuleta hasira, majuto, msongo wa mawazo na hata kusababisha mvurugano katika mahusiano yao. Katika nchi zetu za kiafrika, wanawake wamekuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili. Ni vizuri wenzi washirikiane katika hili, kwa kupeana moyo na kufuatilia matibabu kwa pamoja. Matibabu yanaposhindwa kabisa kuleta mafanikio, wenzi wanaweza kuasili mtoto/watoto k**a watakuwa na utayari.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook Olive Health n Nutrition Clinics kupata mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya mwanadamu na tiba mbalimbali. Usikose kuweka LIKE endapo utafurahishwa na mada hizo.

JEE, UNA TATIZO LA UGUMBA?

K**a una tatizo hili na umeshindwa kulipatia ufumbuzi, wasiliana nasi.

Kwa mawasiliano nasi tuma ujumbe mfupi au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0714366766 ama 0101401678
Ongea na dr mwangi olive herbal clinic

HEALTH WELLNESS & NUTRITION

FAHAMU TATIZO LA MAUMIVU YA TUMBOMaumivu ya tumbo ni dalili inayosumbua watu wengi kwa wakati na umri tofauti. Karibu ki...
14/11/2021

FAHAMU TATIZO LA MAUMIVU YA TUMBO

Maumivu ya tumbo ni dalili inayosumbua watu wengi kwa wakati na umri tofauti. Karibu kila mtu katika maisha yake atapata namna fulani ya maumivu ya tumbo. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha maumivu ya tumbo na mara nyingi huwa sio za kutisha, hutubiwa na kupona. Mara chache husababishwa na hali ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yako. Maumivu yanaweza kuwa katika sehemu maalum ya tumbo au tumbo zima.

Sababu za Maumivu ya Tumbo
Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo.

Maumivu chini ya mbavu kulia yanaweza kusababishwa na
• Mawe kwenye mfuko wa nyongo
• Maambukizi kwenye mfuko wa nyongo (cholecystitis)
• Uvimbe wa ini
• Jipu kwenye ini
• Homa ya ini
• Saratani ya kongosho na kifuko cha nyongo

Maumivu chini ya chembe ya moyo
• Vidonda vya tumbo
• Kiungulia
• Saratani ya tumbo
• Saratani ya kongosho

Maumivu Pembeni mwa kitovu
• Mawe ya figo (kidney stones)
• Maambukizi ya figo (pyelonephritis)
• Maambukizi kidoletumbo (Acute appendicitis)

Maumivu chini ya kitovu
• Maambukizi ya mfumo wa mkojo
• Magonjwa ya zinaa k**a klamidia, PID
• Vivimbe vya mji wa uzazi
• Mimba kuharibika
• Saratani ya kibofu cha mkojo
• Premenstrual Syndrome – PMS

Sababu nyingine za maumivu ya tumbo ni;
• Irritable bowel syndrome
• Utumbo kujiziba (intestinal obstruction)
• Utumbo kujisokota (volvulus)
• Food poisoning
• Allergy ya chakula
• Ugonjwa wa Crohn (Crohn’s disease)
• Ngiri (hernia)
• Homa ya tumbo (typhoid fever)

Maumivu ya tumbo hutibiwa kutokana na sababu ya maumivu. Wakati ukielekea hospitali kwa ajili ya matibabu unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu k**a paracetamol au diclofenac japo kuwa c vizur kutumia dawa za kutuliza maumivu mara kwa mara.

Ukifika hospitali mtaalamu wa afya atachukua historia ya ugonjwa wako na kisha kufanya uchunguzi

Kuna njia mbalimbali za matibabu za matatizo yanayosababisha maumivu ya tumbo, ikijumuisha dawa za kunywa au kuchoma na upasuaji. Kitaalamu tunashauri kutumia food suppliments kwasababu hazina chemical ambazo husababisha matatizo mengne katika mwili

ASANTE KWA KUCHUKUA MDA WAKO KUPITIA MAKALA HII.. KWA ELIMU ZAIDI
NIPIGIE KUPITIA HII NAMBA

0714366766 ama 0101401678
Dr MWANGI Olive Health n Nutrition Clinics

HEALTH WELLNESS & NUTRITION

Dr MwangiOlive herbal n Nutrition Clinics0722 401 678/0714366766Call/whatsappClinics open dailyMon-sat8.00am-6.00pm     ...
31/10/2021

Dr Mwangi
Olive herbal n Nutrition Clinics
0722 401 678/0714366766
Call/whatsapp

Clinics open daily
Mon-sat
8.00am-6.00pm

Your health is our concern

FACTS AND FICTION ABOUT VAGINA'S depth, squirting,  smell, and color of the skin   Dr mwangi from olive herbal clinic wi...
28/10/2021

FACTS AND FICTION ABOUT VAGINA'S
depth, squirting, smell, and color of the skin

Dr mwangi from olive herbal clinic will continue answering the most asked questions from quiz 6 -11

0714366766 or 0722401678

6. Does the cl****is get bigger, too?

Yes! When you’re aroused, your cl****is will swell and retract, meaning that it hides under its hood. Your cl****is won’t change in size as drastically as a p***s does when sexually stimulated, but there’s definitely an increase in size.

7. Do all lady parts look the same?

Nope, not at all. Your va**na, l***a, cl****is, and all other parts of your genitalia are unique. Your l***a may be asymmetrical, or your cl****is may be small. The skin in this area may even be lighter or darker than your overall skin color.

Although there may be average sizes and shapes, everyone’s ge****ls really are different!

8. Why is the skin down there darker than the rest of me?

It’s completely normal for the skin of your ge****ls to be a different color than the rest of you. For example, some women have brown or reddish l***a, while others may have pink or purplish l***a.

Your ge****ls may also become darker when you’re aroused. The blood flow to the area can cause swelling and the color of your cl****is and inner lips (l***a minora) to change.

But, keep in mind, if your va**na is a chronic purple color, you may be dealing with a yeast infection or chronic irritation of the v***a known as a lichen simplex. If you’re worried about the color of your va**na, it’s worth making an appointment with Dr mwangi olive health

9. Is p***c hair really necessary?

Whether you have p***c hair comes down to personal preference. It’s not actually necessary to the health of your va**na.

But there are certain risks from removing p***c hair, depending on the method. For example, you may experience symptoms like razor burn, cuts, or itching if the hair isn’t removed properly.

10. Should I do**he to keep things clean?

Although douching remains a common practice olive health herbal clinic doctors recommend that you don’t do**he. Your va**na cleans itself naturally, so there’s no need to go the extra mile.

Douching can actually strip your va**na of the natural, healthy microbes, as well as temporarily change the natural acidity and cause buildup of harmful bacteria. That means your va**na is left susceptible to va**nal infections and sexually transmitted infections (STIs).

11. Does it smell differently at different times of the month?

It’s totally understandable why you might freak out if there’s an odor coming from your va**na. But the truth is, it’s actually normal for a va**na to have some odor.

For example, Dr mwangi olive health explains you may notice a smell after changing your diet — garlic, tuna, and dietary supplements can have that effect. It’s also natural for va**nal odor to change in intensity and smell throughout menstruation.

But if there’s a persistent and foul odor, or if there’s also a thick or greenish discharge, see your doctor right away. You may have an infection or a bacterial imbalance. Your doctor can prescribe medication to help treat the smell and underlying condition.

The bottom line

The va**na’s depth, smell, and color of the skin, among other things, aren’t the same for everyone. But if you’re concerned about your va**na, such as discoloration or a foul odor, Visit they’ll be able to assure you if everything is normal, or start you on a treatment plan if there are any medical issues.

Either way, it’s important to remember that everyone’s va**na is different — and that’s OK!
DR mwangi Olive Health n Nutrition Clinics 0714366766 or 0722401678

HEALTH WELLNESS & NUTRITION

Address


Opening Hours

Monday 08:00 - 06:00
Tuesday 08:00 - 06:00
Wednesday 08:00 - 06:00
Thursday 08:00 - 06:00
Friday 08:00 - 06:00
Saturday 09:00 - 01:00

Telephone

+254714366766

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Olive Health n Nutrition Clinics posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Olive Health n Nutrition Clinics:

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram