
28/02/2024
Afya ni kuwa na hali nzuri kimwili, kiakili, kijamii, kiroho, kiutu na kisaikolojia bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote.
Kulingana na WHO (World Health Organization – Shirika la Afya Duniani) Afya ni hali ya ustawi kamili wa kimwili, kiakili na kijamii. Sio tu ukosefu wa magonjwa au udhaifu.
Afya njema ni njia ya afya ambayo inasisitiza uzuiaji wa magonjwa na kuongeza muda wa maisha kinyume na kusisitiza kutibu magonjwa
Ili kuwa na afya bora ni vyema kuzingatia kanuni na taratibu bora za afya. K**a mlo kamili (kukiwemo na virutubisho vyote vya chakula), usafi wa mwili, usafi wa mazingira na kuwa na afya ya kiroho (kuishi kwa mapenzi ya Mungu k**a kupendana, kuthaminiana na kuacha dhambi.)
Ipende afya yako na vilevile jali afya ya familia yako. Itawasaidia kuepukana na magonjwa.