Kona Ya Ushauri wa Afya

  • Home
  • Kona Ya Ushauri wa Afya

Kona Ya Ushauri wa Afya Utapata ushauri na njia za kuimarisha afya yako

Klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na bakteria zinazoitwa na sayansi k**a Chlamydia trachomatis.Vijudu...
02/10/2025

Klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na bakteria zinazoitwa na sayansi k**a Chlamydia trachomatis.

Vijududu vinavyosababisha klamidia
Ugonjwa huo huwa hauonyeshi dalili za wazi kwa karibia asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume, hivyo maambukizi mengi hushindwa kufahamika mapema.

Kulingana na wakala wa afya wa Marekani Centers for Disease Control and Prevention ndiyo ya kwanza kati ya maradhi ya zinaa yanayoripotiwa zaidi nchini humo: wataalamu wamekisia kuwa karibia watu milioni tatu huambukizwa klamidia kila mwaka, lakini kulingana na CDC, ni maambukizi 660,000 tu ndiyo ambayo huripotiwa.

Watu ambao hawajafahamu kuwa wameambukizwa klamidia wanaweza wasitafute tiba na hivyo wakaendelea kufanya ngono, bila ya kujua kuwa wanaeneza ugonjwa.

Wakati dalili zinapoanza kujitokeza wanaume husikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa usaha katika uume. Wanawake wanaweza kutokwa damu nje ya kipindi chao, maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa usaha katika uke, au maumivu chini ya kitovu.

K**a utaachwa bila kutibiwa katika wanawake, klamidia inaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya binafsi na ya jamii. Klamidia huaribu tishu za uzazi za mwanamke na kusababisha uvimbe katika fupanyonga (pelvic inflammatory disease, PID). PID inaweza kusababisha mauvimu makali sana katika fupanyonga, utasa/ugumba au utata katika ujauzito ambao unaweza kusababisha kifo.

Watoto waliozaliwa na mama aliyembukizwa klamidia huwa na hatari ya kupata upofu au maambukizi katika mapafu.

Uchunguzi wa maambukizi ya klamidia hufanyika kwa kuchunguza fupanyonga na kiwango kidogo cha majimaji kutoka katika uke au uume ambayo huchunguzwa kwa uwepo wa Chlamydia trachomatis.

Uchunguzi mpya k**a ule wa mkojo ili kufahamu uwepo wa bakteria wa klamidia umekuwa ukitumika pia ili kufanya uchunguzi rahisi zaidi wa watu ambao hawaonyeshi dalili za ugonjwa.

Klamidia inatibika kwa antibaotiki.

Hiyo Sciatic Nerve ndiyo mshipa wa fahamu mkubwa katika mwili wa binadamu unaunganisha na imeesambaa eneo kubwa la mwili...
27/04/2024

Hiyo Sciatic Nerve ndiyo mshipa wa fahamu mkubwa katika mwili wa binadamu unaunganisha na imeesambaa eneo kubwa la mwili mikononi, miguuni na uti wa mgongo...niedelee au inatosha..🤣

06/01/2024
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema uchunguzi wa Maabara ya Taifa umethibitisha uwepo wa virusi vya Marburg ambavyo vina...
22/03/2023

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema uchunguzi wa Maabara ya Taifa umethibitisha uwepo wa virusi vya Marburg ambavyo vinasababisha ugonjwa wa Marburg Virus Disease (MVD) katika Mkoa wa Kagera ambao umesababisha vifo vya Watu watano hadi sasa ambapo amesema Ugonjwa huo hauna tiba mahususi bali hutibiwa kwa dalili anazokuwa nazo Mgonjwa.

Akiongea leo Dar es salaam, Ummy amesema “Uchunguzi ambao tumeufanya katika Maabara yetu ya Taifa ya Afya ya Jamii umethibitisha uwepo wa virusi vya Marburg ambavyo vinasababisha ugonjwa unaojulikana k**a Marburg Virus Disease(MVD)” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Je,wajua??
18/12/2022

Je,wajua??

*KARIBUNI SANA WAGENI* Nikianza na Aliyeuliza juu ya mtoto wake:- Angalia nichakula gani anachopenda kisha mtafutien ung...
18/08/2022

*KARIBUNI SANA WAGENI* Nikianza na Aliyeuliza juu ya mtoto wake:- Angalia nichakula gani anachopenda kisha mtafutien unga wa lishe uliothibitishwa na Wizara ya Afya uitwao "Virutubisho" ndani yake una:-
1) *wanga*- kazi yake nikuleta nguvu mwilini.mfano Mahindi, ngano, viazi mchele.
2) *protin* kazi yake nikujenga mwili, mfano wa vyakula:- Nyama, njegere, mayai, maharage
3) *Vitamin* kazi yake kubwa ni kulinda mwili mfano Maembe, mananasi, Machungwa, zabibu.
4) *Madini* Huhusika sana katika kuuwezesha mfumo wa mwili, mfano, Chumvi, dagaa mboga za kijani, (vyanzo vya baadhi ya madin. Na faida nyingi sana ambazo vyote nilivyo kutajia hapo viko kwenye huo unga lishe, hivyo hii itakuwa nimsaada mkubwa kwa mtoto..

04/05/2022
Kwa wenye shida kuvimba viungo au joint kufa ganzi miguu na mikono..viungo kukaza
18/11/2021

Kwa wenye shida kuvimba viungo au joint kufa ganzi miguu na mikono..viungo kukaza

Thibitisha kauli hii😂😋😋😋
22/10/2021

Thibitisha kauli hii😂😋😋😋

"NINI CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA UCHAFU , HARUFU MBAYA  UKENI NA MUWASHO !!!!  "Leo naona ni bora tukazungumzia tat...
12/10/2021

"NINI CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA UCHAFU , HARUFU MBAYA UKENI NA MUWASHO !!!!

"Leo naona ni bora tukazungumzia tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni maana watu wengi hudhani kuwa na harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchafu tu na ndio maana wanaume huwachamba wake zao kuwa hawajuhi kujisafisha na kufanya wanawake kuongeza jitihada katika kujisafisha ukeni, leo napenda kuzungumzia tatizo hili linalowasumbua wanawake wengi na kuwaumiza kichwa kutokana na kwamba lina athari kubwa sana kwani hufanya ndoa zao kudumaa NK.

~Kitaalamu Hali ya mwanamke kutokwa na maji yenye rangi nyeupe au njano ni Hali ya kawaida na sio tatizo Lakini endapo maji yanatoka yapo katika Hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali au kuwasha hapo una tatizo.

~Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha au kutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nnje ya mwili pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maaambukizi ya bacteria.

~Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa hayawashi na huwa na rangi nyeupe au njano pia huwa na asidi ya LACTIN ambayo huzuia bacteria kuzaliana.

~Mwanamke hutoa kiasi cha grams 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji wa kizazi na grams 3 za ute mwepesi kila siku, kiwango hicho kinaweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi pia Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika na Kuna wakati pia huwa mzito wa rangi ya njano hautoi harufu.

VISABABISHI VYA TATIZO HILI.

Sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili.

1. BACTERIA VAGINOSIS.

Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi,kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano wa kawaida katika mazingira ya uke, wanawake wenye wapenzi wengi na wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili.

2. TRICHOMONAS.

Maambukizi haya hutokana na Aina ya protozoa wa seli moja, trichomonas mara nyingi huambukizwa kwa njia ya ngono, protozoa huyo huweza kukaa kwenye unyevu unyevu kwa Muda wa saa 24 Bila kufa hivyo kufanya taulo na chupi zisizokauka kuwa chanzo kingine cha tatizo hili.

3. YEAST INFECTION.

Kwa kawaida Kuna kiwango kidogo cha yeast (candida albicans) katika uke, huwa tunasema Kuna maambukizi pale kiwango kinapozidi Hali ambayo inatokana na kubadilika kwa Hali ya hewa ukeni (Change in the PH balance of va**na).

Maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ndoa.

Mambo ambayo huchangia tatizo hili ni:

(a) MATUMIZI YA DAWA ZA KUZUIA MIMBA,
(b) MAWAZO,
(c) UJAUZITO,
(d) KISUKARI
(d) MATUMIZI YA ANTIBIOTICS.

4. VAGINAL OR CERVICAL CANCER.

Mtu anapokua na kansa ya uke, hutokwa na maji ya harufu mbaya, hivyo ni heri uwe unafanya check up ili kujua Afya yako na Kwa kuwa cancer ya kizazi inapona hivyo ni vema ukatambua mapema uanze tiba.

5. SEXUAL TRANSMITTED DESEAS (STDs).

Kuna baadhi ya magonjwa k**a vile KASWENDE NA KISONONO yanasababishwa na ngono na kuwa chanzo cha tatizo hili.

6. POOR HYGIENE.

Tatizo la kutokwa na maji wakati mwingine husababishwa na muhusika kua mchafu yan mtu unaoga kwa siku mara moja, chupi moja ndio hiyo hiyo mwaka mzima, pads unakaa nayo saa 24, ukienda kukojoa ujitawadhi na maji masafi hivyo unategemea utakua salama kweli??? Zingatia usafi mrembo.

DALILI ZA TATIZO HILI.

Kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii hutokana na kuharibika kwa uwiano wa bacteria hivyo kuwa na madhara na uchafu hutoka wa aina tofauti hapa chini nitaelezea kila Aina ya uchafu na dalili zake.

1. UCHAFU WENYE RANGI YA KAHAWIA AU DAMU.

Huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevulugika na wakati mwingine ni dalili ya kansa ya kizazi, mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi kuumwa sana nyonga.

2. UCHAFU WENYE RANGI YA NJANO /KIJANI WENYE HARUFU MBAYA.

Endapo uchafu huo utatoka k**a povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas, maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe, dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.

3. UCHAFU MWEUPE MZITO K**A JIBINI.

Mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

4. UCHAFU MWEUPE/KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI.

Uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nnje ya uke.

5. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA TATIZO HILI NA TIBA YAKE.

Matibabu ya tatizo hili hufanyika baada ya kugundua chanzo cha tatizo na mara nyingi tiba Yake ni tiba ya dawa za antibiotics kitu ambacho si tiba nzuri zaidi kwasababu tatizo huweza kujirudia kila wakati na kusababisha matatizo zaidi hivyo tiba nzuri ni kuepuka hili tatizo kwa kufanya yafuatayo:-

👉EPUKA KUJIINGIZA VIDOLE MARA KWA MARA UKENI
👉EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA ANTIBIOTICS MARA KWA MARA
👉PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI NYINGI
👉TUMIA PADS ZENYE ANIONS NI SALAMA KWA AFYA YAKO
👉SAFISHA VIZURI NGUO ZAKO ZA NDANI NA UZIANIKE JUANI NA HATA
KUZIPIGA PASI
👉KUNYWA JUICE YA APPLE,STRAWBERRY, NANASI KWA WINGI
👉EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
👉HAKIKISHA UNAJISAFISHA KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA
👉EPUKA KUTUMIA DAWA ZA KUZUIA MIMBA
👉EPUKA KUTUMIA SABUNI AU VITU VYA MANUKATO UKENI,

NOTED : Wanawake wengi mnapenda kutumia baadhi ya dawa kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kufanya uke kunukia vizuri, au kukaza uke rafiki uke una harufu nzuri sana ambayo haipatkan kokote hivyo haihitaji kuwekwa pafyumu Wala kusafishwa kwa sabuni za kemikali kwani huwa panajisafisha hivyo ni heri ukaacha kutumia kwani madhara Yake hayaonekani sasa ila baada ya Muda huonekana.

Kwa Msaada na Ushauri Wa Matatizo Mbali Mbali Ya Afya wasiliana kwa namba 0746117684

TUMSIKIE MHESHIMIWA.....
27/09/2021

TUMSIKIE MHESHIMIWA.....

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kona Ya Ushauri wa Afya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Kona Ya Ushauri wa Afya:

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram