Ikomboe Afya Yako

Ikomboe Afya Yako Online clinic

KUHUSU HARUFU MBAYA UKENI NA KUTOKWA NA UCHAFU UKENI!!!Kutokwa na uteute wa njano au mweupe au usio na rangi ukeni ambao...
10/05/2023

KUHUSU HARUFU MBAYA UKENI NA KUTOKWA NA UCHAFU UKENI!!!
Kutokwa na uteute wa njano au mweupe au usio na rangi ukeni ambao sio mzito sana na usio na harufu mbaya mfano wa kitu kilichooza, ni jambo la kawaida kwa mwanamke.

Hii hutokana na mfumo wa uzazi kujisafisha kwa kuondoa seli zilizokufa, tishu za mabaki ya hedhi, na masalia mengine ya hedhi. Hivyo vyote husafishika na kutolewa kupitia ukeni.

Mara nyingi uteute huo hua si mzito, hauwashi wala hautoi harufu mbaya/kali. Uteute huo hua pia na lactic acid na walinzi wengine wa mwilini ambao huua bakteria ama fangasi wabaya wanaojaribu kuvamia via vya uzazi.

Kutokwa na uteute unaowasha, wenye harufu mbaya na kali k**a vitu vilivyooza au shombo ya samaki wabichi alafu ute kua wenye rangi nyeupe na mzito k**a maziwa mgando ni dalili mbaya ya Ugonjwa wa BACTERIAL VAGINOSIS yaani mrundikano wa bakteria wabaya ukeni.

Ugonjwa huu ni janga linalokera, ngumu kuelezeka kwa sababu wanawake wahanga wengi huficha hali hiyo wakihofia kutengwa ama kuonekana na kuhisiwa vibaya.

Hata hivyo shida hii imezidi kuzua migogoro binafsi na ya kindoa na kuvunjika kwa mahusiano mengi!!!!!

CHANZO CHAKE NI NINI?
Chanzo kikuu cha ugonjwa huu ni bakteria kukua kwa wingi ukeni na via vyake. Pia kuna athari za fangasi na matumizi ya kemikali ukeni, kemikali k**a sabuni, perfume na matumizi ya bidhaa za Kubana uke zisizo tambulika kitaifa au kimataifa pamoja na tabia ya kupakaa vilainishi au mate ukeni wakati wa tendo la ndoa au wakati wa kujiridhisha kingono (kupiga punyeto).

Wanawake napenda kuwafahamisha kua uke ni kiungo mojawapo cha kipekee chenye uwezo wa kujisafisha chenyewe!!!

Hivyo kutumia sabuni, marashi au perfume ili kuondoa harufu mbaya ukeni ni kujitengenezea matatizo mengi kiafya.
Kiasili, Uke una mazingira yake halisia na bakteria wa faida (kitaalamu hujulikana k**a normal flora) ambao ni walinda na wasafisha uke ufanywao kwa utaratibu maalumu wa mwili wenyewe.

Kutumia kemikali ni kuua walinzi ukeni hivyo kinga yake hushuka na ni kubadilisha mazingira ya uke na inakua rahisi wadudu kuweza kushambulia.

DALILI ZA UGONJWA HUU
>Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
>Kutokwa na uteute wenye damu kipindi kisicho cha hedhi
>Harufu mbaya ukeni
>Kutokwa na uchafu mweupe unaonuka wakati wa tendo la ndoa
>Uteute kuwasha/miwasho

MADHARA YAKE
>Mimba kuharibika
>Kupata maradhi mbalimbali k**a U.T.I
>Kujifungua kabla ya mda
>Kujifungua mtoto mwenye ukavu macho
>Kuharibika kwa kuta za uke na mfuko wa uzazi.
>Misuli ya uke kulegea na uke kutanuka.

ANGALIZO
Wahanga wanashauriwa kufika hospitali kwa ajili ya vipimo na kuanzishiwa tiba husika.
Mara nyingi baadhi ya wahanga wa ugonjwa huu, tiba wapatazo haziwasaidii na tatizo huongezeka.

Kwa ushauri, Wakati wa kutumia dawa hizo ni vyema kuepuka vihatarishi vya kupata ugonjwa huu k**a vile;
> Kuepuka matumizi ya pedi 1 mda mrefu
>Kuepuka matumizi ya kuweka vitambaa vichafu ukeni wakati wa hedhi.
>Kuepuka matumizi ya kemikali ukeni na madawa bila kufuata ushauri wa matabibu na madaktari.
>Kuepuka kua na wapenzi wengi
>Kuepuka kuchangia vifaa vya kuogea na nguo za ndani

>Kuepuka joto hasa ukeni kwani hapo huweza kuzalisha jasho na bakteria kuweza kuzaliana
>Epuka uchafu (Kua msafi wakati wote)
>Epuka vyakula vinavyosapoti ukuaji wa bakteria mwilini k**a sukari kwa wingi, ulevi, uvutaji sigara kwani hushusha kinga ya mwili, vyakula vya kusindikwa, na mafuta mengi.

>Wanene, Wakiweza punguza unene au Ongeza usafi kwani wanene ni rahisi kutoa jasho na bakteria kuweza kuzaliana sehemu za jasho k**a usafi hautozingatiwa.

MATIBABU
●Fuata matibabu utakayopewa hospitalini
●Tumia lishe bora.
-Vyakula vyenye madini yakutosha
-Vyenye mbogamboga na matunda
Mfano machungwa hutoa sumu mwilini.

●Tumia Virutubisho lishe vyenye Ubora wa hali ya juu, Vitambulikavyo kitaifa na kimataifa.

Je, Umejaribu njia nyingi lakini bado tatizo kwako ni linabaki kua sugu na ungependa kujaribu virutubisho lishe kutatua tatizo lako?

Unaweza kututumia ujumbe Inbox au acha komenti yako, tutakusaidia!!!!

Mawasiliano ni 0675364882/0767397226

Address

Arusha

Telephone

+255758777895

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ikomboe Afya Yako posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category