
21/07/2025
KUNA UKUU(UMALKIA/UFALME) UTAUKOSA KWA SABABU TU YA KIBURI CHAKO.
Kuna watu wengi wamekosa kuwa wakuu kwa sababu tu ya viburi walivyonavyo yaani kuwa Waziri mkuu,Rais ,wabunge,mawakili Wa kimataifa, wasimamizi Wa makampuni makubwa,wakuu Wa mikoa na ukuu Wa aina yoyote wa kifalme.
Tukirejea katika biblia Vashti aliukosa UMALKIA kwa sababu tu ya kiburi chake alipoitwa na mfalme Ahasuero alikataa kwenda.
ESTA 1:11-12
Ukuu wako unaweza ukaondolewa kwako kwa sababu ya kiburi chako,Kuna nafasi ulistahili ukae wewe k**a mtawala ila umezikosa kutokana TU na kiburi chako
Kuna kibali Cha sauti Yako umekikosa kwa sababu tu ya kiburi chako,Kuna mtu ana mawazo mazuri,hoja nzuri, ila yameshindwa kufika kwa mfalme kutokana TU na kiburi chake.
Kuna nafasi ya utawala ambayo ulistahili wewe ila imeondolewa TU kwako kwa sababu ya kiburi chako.tukirejea TU kwenye hii habari ya Vashti aliukosa UMALKIA kwa sababu ya kiburi chake na kupewa ESTA kuwa malkia
ESTA 2:17
Uzuri wako Wa sura usikufanye uwe na kiburi, maana Mungu atainua wazuri kuliko wewe kuishika nafasi Yako(UMALKIA/UFALME) Wako.Uzuri Wa Vashti haukuonekana kwa mfalme baada ya yeye kukataa amri ya mfalme Ahasuero.Mungu akamuinua ESTA mzuri zaidi na aliyejawa hekima.
Tuache kiburi maana Kuna ukuu tuliyoubeba ila tumebakia kwenye ngazi za kuwa mabalozi Wa nyumba kumi,wenyeviti Wa vitongoji, na wenyeviti Wa vijiji wakati kiuhalisia sisi ni mawaziri wakuu na wafalme.
fikra, ishi kwa raha, mwanasaikolojia Elia Nnko