05/03/2026
Jinsi Ya Kuepuka Ugonjwa Wa Kisukari:
Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kujikinga na ugonjwa wa kisukari;
1) Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa siku.
2) Epuka kula chakula kingi kupita kiasi.
3) Epuka kula chakula chenye mafuta mengi au sukari nyingi.
4) Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.
5) Pima sukari katika damu mara kwa mara, angalau mara moja kwa mwaka.
6) Epuka matumizi ya pombe za aina zote.
7) Epuka matumizi ya sigara , bidhaa nyingine za tumbaku na madawa ya kulevya.
Jinsi Ya Kuishi Na Ugonjwa Wa Kisukari:
Ili kuishi na ugonjwa wa kisukari, mgonjwa anashauriwa kufanya mambo yafuatayo;
a) Dhibiti Ulaji Wako.
1) Kula mlo kamili uliotayarishwa kutokana na angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula.
2) Kula vyakula vya nafaka k**a ulezi, mtama, uwele, ma nafaka zisizokoboewa kwa mfano dona, ngano, au shairi.
3) Kula mboga mboga kwa wingi kwa mfano mchicha, matembele, karoti, majani ya maboga, kisamvu, mlenda nk.
4) Kula kiasi kidogo cha vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi katika mlo.
5) Kula vyakula vya jamii ya kunde k**a mboga (sehemu ya mlo) kwa mfano maharagwe, njegere, mbaazi, kunde, choroko, nk.
6) Kula matunda kwa kiasi mfano ndizi au chungwa moja au kipande cha papai au embe kubwa katika kila mlo.
7) Kunywa maji kwa wingi.
8) Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi k**a jamu, asali, chokoleti, p**i, bazooka, aiskrimu, na juisi bandia.
9) Epuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi.
10) Epuka unywaji wa pombe.
b) Fanya Mazoezi Mara Kwa Mara Angalau Nusu Saa Kwa Siku.
c) Tunza Miguu Yako Kwa Makini.
1) Epuka kuvaa viatu au soksi zinazo bana.
2) Epuka kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu ambacho huweza kusababisha kuanguka na kuumia.
3) Osha miguu yako kwa maji safi na kausha vizuri hususan katikati ya vidole.
4) Usitembee bila kuvaa viatu.
5) Vaa viatu vya wazi na vyenye kisigino kifupi.
6) Epuka kijiumiza, na unapokua na kidonda tibu mapema.
d) Epuka Msongo Wa Mawazo.
1) Zingatia afya ya kinywa
2) Usafi wa mwili.
3) Taarifa na elimu kuhusu kisukari.
4) Masharti ya dawa na ulaji.
5) Kuhudhulia kliniki k**a inavyoshauriwa.
Piga 0746633559