Dr.habelnoah

Dr.habelnoah unaswali changamoto uliza jambo jema katika maisha ni kuuliza ili kujifunza

13/05/2026

Endapo mtoto wako hawezi kufanya mambo yafuatayo anapokuwa na umri wa miezi miwili, muone daktari kwa ushauri zaidi ⁣
▫️Hashtuki unapotokea mlio mkubwa ⁣
▫️Hafuatishi vitu kwa macho yake, ⁣
▫️Hawezi kutabasamu⁣
▫️Hapeleki mikono yake mdomoni⁣
▫️Hawezi kuinia kichwa chake anapokuwa anacheza⁣


#

Endapo mtoto wako hawezi kufanya mambo yafuatayo anapokuwa na umri wa miezi miwili, muone daktari kwa ushauri zaidi ⁣▫️H...
13/05/2026

Endapo mtoto wako hawezi kufanya mambo yafuatayo anapokuwa na umri wa miezi miwili, muone daktari kwa ushauri zaidi ⁣
▫️Hashtuki unapotokea mlio mkubwa ⁣
▫️Hafuatishi vitu kwa macho yake, ⁣
▫️Hawezi kutabasamu⁣
▫️Hapeleki mikono yake mdomoni⁣
▫️Hawezi kuinia kichwa chake anapokuwa anacheza⁣

13/05/2026

BY DR.HABELNOAH
MESIC HOSPITAL
ARUSHA TZ

Fahamu kuhusu tatizo la hangover na suluhisho lake

Kuna pombe au vilevi vya aina tofauti k**a vile bia, wine, pombe kali. Watu wengi hupenda kujiburudisha kwa kunywa vinywaji hivi na kati yao kuna ambao wanajikuta baada ya kunywa kwa kupitiliza wamepata hali ya kutapika, kichwa kuuma, kizunguzungu, usingizi mkali, uchovu wa mwili n.k, hali ambayo ni maarufu k**a “Hangover”.

Hali hii inaweza kuanza masaa machache baada ya kuacha kunywa kilevi hadi masaa 24. Kikubwa kinachosababisha hali hii ni kuwa na kiasi kikubwa kupitiliza cha kilevi mwilini. Hii inatokana na kwamba kiasi cha kilevi kinacho tolewa mwilini hakibaliki kadiri ya kiasi cha kilevi ambacho mtu atatumia (Zero order kinetics).

Inamaana k**a litre 1 moja ya kilevi inatolewa ndani ya saa moja, kwahivyo endapo mtu atakunywa litre 5 za kilevi ndani ya saa moja bado kiasi ambacho kitatolewa mwilini kitabaki kuwa litre moja ndani ya saa moja. Hali hii inasababisha ulimbikaji wa pombe mwilini. Ulimbikaji huu huongeza kasi katika athari za pombe mwilini. Hali ambayo inafahamika k**a “hangover”

Uwezo wa mwili kukabiliana na kiasi cha kilevi ambacho mtu amekunywa inatofautiana kati ya mtu hadi mtu kulingana na:

Kiasi cha pombe ambacho mtu anakunywa mara kwa mara. Endapo mtu hunywa pombe mara kwa mara, uwezo wa mwili wake kukabiliana na pombe huongezeka.
Vinasaba vya mtu ambavyo vinaamua kiasi na aina za protini za umeng’enyuaji zinazotengenezwa.
Magonjwa ambayo yaweza sababisha kupungua au kuongezeka kwa kiasi cha uondoaji wa pombe.
Utumiaji wa pombe na dawa ambazo zinaathiri mlorongo wa umeng’enyuaji wa pombe.

Je, ninawezaje kuondoa hali ya “Hangover”?
Hali hii ya hangover huisha pale ambapo mwili umeweza kutoa pombe kufikia kiasi kidogo hivyo mwili unahitaji muda kuendelea kuondoa pombe ili uweze kurejea hali ya kawaida. Katika muda huu unaweza kufanya yafuatayo ili kuusaidia mwili kuondoa pombe hii:

1. Kunywa maji ya kutosha.
2. Kula chakula chenye vitamin B complex vinavyohitajika katoka umeng’enyuaji wa pombe k**a vile nyama aina nyingi( ng’ombe, mbuzi, kuku, samaki), mayai, maziwa, viazi, maharagwe n.k
3. Kula /kunywa vitu vyenye sukari

12/05/2026

Jinsi mtoto anavyoongezeka uzito.

▫️Kama mtoto wako ana pata maziwa ya kutosha na anashiba vizuri, katika miezi mitatu ya mwanzo mtoto anaongezeka gram 28 kila siku (yaani anaongeza zaidi ya gram 800 kwa mwezi.)

▫️Kuanzia miezi minne mpaka miezi sita mwanao anapaswa kuongeza kuanzia gram 450 mpaka gram 750 kwa mwezi.

▪️Kwa ujumla kuanzia miezi minne mpaka sita mtoto anapaswa kuwa na uzito mara mbili ya uzito aliozaliwa nao.

▫️Mtoto wa kiume huwa na uzito mara tatu ya uzito aliozaliwa nao anapokuwa na miezi 12, wakati mtoto wa k**e huwa na uzito mara ya uzito aliozaliwa nao anapokuwa na miezi 15.

▫️Kuanzia mwaka wa pili, mtoto anaongeza kilogram 2 kila mwaka mpaka anapokuwa na miaka mitano. Katika kipindi hiki ukuaji wa mtoto unatokea pole pole sana.

Wakati mwingine watoto wengi wanapokuwa na umri kati ya miezi mitatu mpaka sita huwa wanakuwa na uzito mkubwa kuliko umri wao. Hii inaweza kuwatia hofu wazazi pamoja na madaktari wake. Hata hivyo haushauriwi kumpunguzia nyonyo mtoto katika umri, kwa sababu mara nyingi uzito wao huwa unashuka wanapofikisha umri wa miezi 18.

Tuko pamoja!?

12/05/2026

Kwa nini usitumie pamba kutoa nta kwenye masikio?⁣⁣
⁣⁣
Inawezekana ukawa miongoni mwa watu wengi wanao amini kuwa nta inayotoka katika masikio ni uchafu. Na inawezekana una mazoea ya kusafisha masikio yako kwa kutumia pamba.⁣⁣
⁣⁣
Nisikilize, iwapo una mazoea ya kusafisha masikio kwa kutumia hizo pamba acha mara moja. Unahatarisha afya ya masikio yako.⁣⁣
⁣⁣
Je nta inayotoka kwenye masikio ina faida zozote?⁣⁣
Ndio nta inayotoka kwenye masikio ina faida. Na wala sio uchafu k**a inavyodhaniwa na watu wengi.Faida hizo ni k**a ifuatavyo⁣⁣
⁣⁣
▫️Husaidia kuzuia hatari ya kupata maambukizi kwenye masikio⁣⁣
⁣⁣
▫️Husaidia kuzuia wadudu kuingia kwenye masikio (harufu ya nta ya masikio hufukuza wadudu wasiingie kwenye masikio)⁣⁣
⁣⁣
▫️Husaidia kulinda sikio lako lisikauke(nta hufanya sikio kuwa na unyenyevu wakati wote)⁣⁣
⁣⁣
Kwa nini usitumie pamba kwenye masikio?⁣⁣
Kuweka pamba kwenye masikio kuna madhara mbalimbali k**a ifuatavyo. ⁣⁣
⁣⁣
1.Kuongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye masikio⁣⁣
2.Kuongeza hatari ya kuwa kiwizi ⁣⁣
3.Kutoboa ngoma ya sikio⁣⁣
⁣⁣
Ufanye nini?⁣⁣
Iwapo unahisi sikio lako linatoa uchafu usio kuwa wa kawaida ni vizuri kwenda kwenye kituo cha afya ambako utapata ushauri wa kitaalam na matibabu.⁣⁣
⁣⁣IMEANDIKWA NA DR.HABELNOAH
MESIC HOSPITAL

12/05/2026

Every day, nurses save lives and play a critical role in improving people’s health, preventing disease and responding to emergencies around the world.

On Tuesday’s International Nurses Day, join us in thanking nurses for their unwavering dedication, compassion and resilience.

Want to celebrate a nurse who’s made a difference in your life? Tag them in the comments. 💙

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr.habelnoah posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category