29/03/2026
ποΈLEO NIPO TOFAUTI KIDOGO NA NINGEPENDA KUSHARE NANYI ELIMU YA MAISHA KUTOKA KWA MWAMBA MMOJA ANAITWA "BENJAMIN FRANKLIN"
> Powered By
---------------------------------------------------------------
Huyu ni Benjamin Franklin ni mmoja wa watu waliobadilisha dunia kupitia maarifa, nidhamu na ubunifu.
Maisha ya Benjamin Franklin yanatufundisha jambo kubwa sana:
* Mafanikio hayaji kwa bahati, yanatokana na kujijenga kila siku.
LEO TUJIFUNZE KUTOKA KWA BENJAMIN FRANKLIN
Watu wengi wanataka mafanikio, Lakini hawako tayari kulipia gharama yake.
Benjamin Franklin alitambua mapema kuwa: Maisha hayakupi unachotaka⦠yanakupa unachokifanyia kazi.
Hakuzaliwa tajiri, Hakupata nafasi yoyote kwa urahisi | Lakini aliamua kitu kimoja β KUTOKATA TAMAA.
Aliunda kanuni zake (13) na kuzifata kanuni hizo kwa nidhamu ya hali ya juu [k**a analipwa vile], summary ya kanuni kwa ujumla:
1. Jisimamie mwenyewe | Usitegemee mtu akusukume β uwe na msukumo wako ndani.
2. Tumia muda wako kwa akili | Muda ni mali. Ukipoteza muda, unapoteza maisha.
3. Jenga tabia, sio maneno | Watu wengi wanaongea sana, lakini hawafanyi - Franklin alifanya zaidi ya alivyoongea.
4. Jifunze kila siku | Elimu haimaliziki, kila siku ni darasa. na Franklin hakusubili kufundishwa alinyanyuka na kujifunza mwenywe
5. Kosa ni sehemu ya safari | Alikosea, lakini hakukata tamaa β alijifunza na kusonga mbele, aliamini kukosea sio dhambi ila kutojifunza kupitia makosa ni dhambi kubwa zaidi
π Ujumbe kupitia somo la leo - kwako:
1. Hakuna anayekuja kukuokoa, usipopambana wewe k**a wewe sahau mafanikio
2. Hakuna siku itakayokuwa βperfectβ, ila unaweza fanya imperfect day kuwa perfect
3. Ukisubiri sana, maisha yatakupita - Kumbuka muda hautokusubili ufanikiwe ndio uendelee (Muda upo kazini, usipo jitidi kwenda nao sawa hutofika pale unapohitaji/tegemea kufika)
4. Anza sasa. Hata k**a ni kidogo [Simama. Amka. Pambana. Mafanikio ni yako ukiamua]
TIPS 2 MUHIMU ZITAZOKUSAIDIA KUPATA KAZI KWA HARAKA
1. Tembelea maofisi unayoamini yanatoa nafasi za kazi zinazoendana na wewe au taaluma yako - peleka maombi hata k**a hawajatangaza nafasi za kazi kwa wakati uo
2. Tuma maombi kwenye taasisi/kampuni zilizotangaza nafasi za kazi lakini nafasi uliotaka kuomba haikujumuishwa/kuhusishwa - mfano. Bank, hospital au kampuni fulani imetangaza nafasi za manager ila wewe ni accountant unaweza tuma maombi kwa nafasi ya account hata k**a haijatangazwa kwa wakati uo (maombi ya kazi yanayowasilishwa kwa email, postal code au physical)
> π βEnergy and persistence conquer all things.β β Benjamin Franklin