01/01/2021
~ JE WAJUA? MATATIZO YANAYOPELEKEA MAUMIVU YA VIUNGO - JOINT TEARS & WEAR°.
~
ARTHRITIS NI NINI ?
~
Matatizo ya viungo,miguu kuwaka moto , maumivu ya kiuno na mgongo , yamekua yakiwasumbua watu wengi hasa wenye uzito mkubwa , wanaofanya mazoezi na wazee wenye umri kuanzia 55+.
~
Hii ni kwasababu umri unavyozidi kwenda mwili unashindwa kuzalisha ute ute katika viungio vya mifupa na hivyo kupelekea misuguano ya mifupa Na Kusababisha maumivu makali sana na kupelekea mtu kushindwa Kukaa , Kuinuka , Kukimbia au Hata Kutembea Kabisa!!
~
- Mara Nyingi Ugonjwa Huu Huitwa ARTHRITIS , Unasababishwa na hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa.
~
Inaweza kuwa cartilage inalika,upungufu wa synovial fluid (Maji Maji Katika Maungio ) , maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo Mbali Mbali , Ikiwemo Uzito mkubwa.
~
Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo hilo moja.
~
Chanzo Cha Arthritis Ni Nini...?
~
Ili Upate Kuelewa Vyema Chanzo cha ugonjwa huu,hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana( Maungio).
~
Mfano Goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:
~
Maungio ya mifupa - Ligaments;
~
-Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja , hii ni k**a utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje , ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
~
Cartilage ; Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja,Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
~
Capsule ; Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote , ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane.
~
Synovial fluid : Huu ni ute ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.
~
K**a nilivyoeleza hapo juu kuwa kuna aina zaidi ya 100 za ugonjwa huu wa joints au arthritis.
~
Katika mada yetu ya leo tutatazama aina k**a nne hivi za ugonjwa huu,tukielezea chanzo cha kila aina....
~
1. Osteoarthritis.
- Hii ni aina ya arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote...
~
Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa , Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka.
~
- Cartilage ni kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla ( shock absorber ), Cartilage hii inapopoteza ubora wake , tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu.
~
Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana sana.
~
- Athari za ugonjwa huanza taratibu na kuongezeka zaidi na Mgonjwa ataanza kupata maumivu kwenye joint baada ya kufanya shuguli fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu.
~
Joints zitaanza kukaza siku hadi siku , Hasa wakati wa asubuhi unapotaka kuanza shughuli zako za kawaida.
Na siku zinavyosogea ndivyo utakavyoona ni vigumu zaidi kukitumia kiungo chako , Mara nyingine utaona uvimbe kwenye joint.
~
Osteoarthritis - Hushambulia zaidi nyonga,mikono , Magoti na Uti wa Mgongo.
~
2. Rheumatoid arthritis.- Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili unapopungua , viungo huanza kushambuliwa , ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha uvimbe na maumivu.
~
Hali hii isipodhibitiwa,huweza kusababisha ulemavu . Ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho , Ngozi , Mapafu , Midomo , Damu na Mishipa ya Damu.
~
Huu ni ugonjwa ambao zaidi ni wa wanawake na huwatokea zaidi wawapo kati ya umri wa miaka 40 hadi 60.
~
Mgonjwa atasikia maumivu na kuona uvimbe kwenye joints za pande zote za mwili ;
~
Yaani k**a ni magoti yote mawili yatashambuliwa na Viungo vinavyo shambuliwa zaidi ni Vidole , Viwiko vya mikono na miguu.
- Athari zake huonekana zaidi asubuhi unapoamka na maumivu yanaweza kudumu kwa muda wa hadi nusu saa.
Muathirika wa ugonjwa huu hujisikia mchovu muda wote , hukosa hamu ya kula na hupungua uzito , Ugonjwa huu huweza kukua zaidi na Kusababisha matatizo katika viungo vyote vya mwili.
~
Matatizo yanayoweza kujitokeza ugonjwa ukikua ni k**a yafuatayo:
– Macho kuwa na ukavu , maumivu , wekundu , kutopenda mwanga na kutoona vizuri.
– Midomo , Ukavu au kukauka kwa lips za midomo,maumivu na maambukizi ya fizi.
– Ngozi,Vijinundu chini ya ngozi kwenye maeneo yenye mifupa
-- Mapafu,Kushindwa kupumua vizuri.
– Mishipa Ya Damu,Uharibifu wa mishipa ya damu.
– Damu , Upungufu wa chembechembe nyekundu za damu.
3. Infectious arthritis (septic arthritic).
- Aina hii ya arthritis inatokana na maambukizi ya bacteria kwenye synovial fluid. Maambukizi haya yanaweza kuwa pia ni ya fungus au virusi.
~
Wadudu kutoka sehemu nyingine ya mwili iliyo karibu na maungio ya mifupa huweza kusambaa kupitia mfumo wa damu hadi kwenye joint na kuleta maambukizi.
~
Mara nyingi mtu mwenye aina nyingine ya arthritis ndiye anayepata maambukizi ya namna hii , Mgonjwa ataanza kwanza kupata homa , maumivu na uvimbe kwenye joint.
~
Maeneo ambayo hushambuliwa zaidi na aina hii ya arthritis ni Magoti , Mabega , Kiwiko cha mkono , Kiganja (wrist) na vidole na mara nyingi ni eneo moja tu ndilo litakaloshambuliwa.
~
4. Juvenile rheumatoid arthritis (JRA).
- Ni ugonjwa ambao huwapata zaidi vijana walio na umri ulio chini ya miaka 16 na unakuja kwa namna nyingi.
Kuna aina kuu tatu za ugonjwa huu:
~
I. Pauciarticular JRA.
- ~
~Huu ndiyo unaoonekana zaidi na hauna madhara makubwa ukilinganisha na aina nyingine,Mtoto atasikia maumivu kwenye joints zinazofikia nne.
II. Polyarticular JRA.
- Huu hushambulia joints nyingi zaidi , zaidi ya nne na maumivu yake ni makali zaidi.
Kadri siku zinavyo ongezeka, ndivyo maumivu yatakavyozidi.
III. Systemic JRA.
- Huu huonekana kwa nadra ambapo maumivu hujitokeza kwenye maeneo mengi na madhara yake kuwa makubwa zaidi,
Mtoto ataanza kusikia homa za vipindi ambapo huzidi zaidi nyakati za jioni.
~
Hali hii inaweza kumtokea mtoto kwa muda mfupi au kwa wengine kwa muda mrefu sana.
Mtoto atapata mauvimu kwenye maungio ya mifupa (joints) , uvimbe kwenye maungio hayo na kukak**aa kwa viungo.
Mtoto huyu atakosa hamu ya kula hivyo kumfanya akonde.
Ugonjwa ukizidi , mtoto anaweza kudumaa (kushindwa kukua), ukuaji wa mifupa yake kuathirika na kupata matatizo ya macho (uveitis).
Changamoto Kubwa Ya Matatizo Ya Joints Huwapata Wana Michezo , Wanyanyua Vyuma (Body Builder) ,Watu Wanaofanya Kazi Ngumu,Mafundi ,Watoto Wadogo Wenye Umri wa Kuanza Kutembea , Magari , Wabeba Mizigo Na Madereva Wa Masafa Marefu Pamoja Na Wafanyakazi Wa Mahofisini Wanao Fanya Kazi Za Kukaa Zaidi.
"Lipo Suluhisho Pekee la Kumaliza Matatizo Yote Haya Kwa Haraka Sana
~
📷 Tatizo Lako linapona kabisa. Wasiliana Nasi kwa kupiga Simu namba 0629214933