19/07/2025
Nini husababisha tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake-1
Hamu ndio mwanzo wa kila kitu. Inaanza kwanza hamu, unafuata utamu na baadae kilele. Hamu ni hisia za kutaka kufanya, hii ndio kwa lugha ya kawaida wanaita nyegezi.
Kukosa hisia ni tatizo linawaathiri wanawake wengi. Wengine tatizo limekuwepo tangu ajitambue, lakini wengine tatizo hili limetokea baadae tu.
Bahati mbaya sana wanawake wengi wamekuwa wakikaa kimya na hata wale ambao wamekuwa wakitafuta tiba, wamekuwa hawapati matibabu ambayo sio sahihi kutokana na uelewe mdogo wa masuala haya miongoni mwa Jumuia ya wataalam wa afya
Nini kina sababisha tatizo hili
Hili ni tatizo mtambuka; kuna sababu nyingi sana zinazosababisha mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa
▫️Mahusiano - Mbali na afya ya mwili na akili, uhusiano na mwenzi wako ni jambo la muhimu sana katika kufurahia tendo la ndoa. Iwapo uhusiano wenu una matatizo, ugomvi na kukosekana kwa uaminifu inaweza kuwa sababu. Hata kwa wana ndoa ambao hawana matatizo yoyote bado kuishi pamoja muda mrefu huwa inasababisha hisia kupungua hasa kwa wanawake.
▫️Uchovu na mafadhaiko - sababu zote zinazosababisha uchovu wa mwili na stress ikiwemo kazi za nyumbani, ofisini, magonjwa k**a upungufu wa damu, magonjwa ya moyo, ugonjwa wa mapafu au magonjwa ya akili zina athari kubwa sana katika hisia za mwanamke
Pia hali hiyo hutokea baada ya mama kujifungua, ambapo mama anachoka mara kwa mara kutokana na kukidhi mahitaji ya mtoto, hali ambayo hupunguza sana hamu ya tendo la ndoa.
Wanawake wa umri wa kati wanaathiriwa na mahitaji ya wazazi, watoto wao ambao wanakuwa katika umri wa kubalehe, changamoto kazini na mabadiliko ya wenzi wao.
▫️Umri na kukoma hedhi
Matatizo huwa yanatokea mara nyingi kwa wanawake wenye umri wa kati ya miaka 45 hadi 65, na kwa kiwango cha chini kwa umri chini ya miaka hiyo.
▫️Magonjwa ya akili na baadhi ya dawa ikiwemo sonona, hofu na dawa zinazotumika kutibu magonjwa hayo zinaweza kusababisha.
Inaendelea kwenye post inayofuata. .
-