
20/09/2024
WANAUME NA MIMBA ISIYOTARAJIWA (UNPLANNED PREGNANCY)
MIMBA ISIYOTARAJIWA (UNPLANNED PREGNANCY)
Hii ni mimba iliyopatikana kinyume na uhitaji wa wahusika,
Inaweza kuwa mwanamke na mwanaume wakawa kwenye mahusiano ya kawaida au mahusiano ya ndoa.
Mimba aina hii hutokea wahusika wanapofanya tendo la ndoa pasipo uwepo wa kinga ya kuzuia mimba.
Taasisi ya Mkijacho ilifanya utafiti kwa kuuliza maswali kutoka kwa wanaume na wanawake kupata majibu juu ya ukweli uliopo kuhusu mapokeo ya taarifa ya mimba isiyotarajiwa kwa wanaume,
walipokeaje hilo swala na yapi yalikua majibu yao na matokeo yaliyotokea baada ya taarifa za uwepo wa mimba isiyotarajiwa.
Haya ndio baadhi ya majibu.
1)Anna Johnston,
Tulikua na uhusiano mzuri tu mpaka pale nilipojigundua mjamzito na kumpatia taarifa,
Uhusiano wetu uliishia hapo.
Alisema hayuko tayari kuitwa BABA na akaamua kuniblock.
2) Peter makaranga,
Alikua ni mwanamke mwenye kila sifa niliyoihitaji,
Ujinga wangu wa kutofikiri kabla ya kutenda ulifanya tuachane baada ya kumlazimisha kutoa mimba,nilimnunulia dawa na kumpelekea alipo.
Najutia sana nilikosa mtoto na nimemkosa yeye baada ya kumlazimisha kutoa mimba alisema hayuko tayari kuua watoto wengine zaidi,
Sahivi Ameolewa ana watoto Mimi nipo tu sina mtoto hata wa kusingiziwa ๐ข๐ข
3)Fatma Hassan,
Kwa miaka 9 alidai ananipenda sana na siku niliyomkubalia kuwa pamoja nae ndio siku niliyopata mimba,
Baada ya kumwambia kuhusu mimba alisema hayuko tayari kuitwa BABA.
Namshukuru Mungu nimelea mimba nimejifungua mtoto mzuri sana Sasa hivi anaishia kulike picha za mtoto humu mtandaoni kunitafuta pia anaogopa ๐๐๐
4)Rajab Ally,
Ukweli nilikosea sana na ninajisikia hatia hadi muda huu.
Nilikataa ujauzito usiotarajiwa,
Familia ya Binti imemuozesha binti yao na kumpa mwanaume mwingine ujauzito wangu na mpaka sasa sina haki ya kumuona mtoto wala kumtambua k**a ni mwanangu,
Ilikua hasira tu na ujana Kwa sasa namhitaji mtoto wangu sijuhi nifanyeje,
Hayo ni baadhi ya maoni ya wadau tuliowahoji lakini pia wako waliosema wanaume zao walifurahia sana na kuwapa zawadi k**a vile magari n.k
Ukweli kuhusu wanaume na mimba isiyotarajiwa (unplanned pregnancy)
Kukabiliana na mimba isiyotarajiwa (unplanned pregnancy) ni mojawapo ya kitu kinachowapa msongo wa mawazo wanawake na wengine kimewagharimu maisha yao pale walipojaribu kutoa mimba,pia wengine imewafanya kuwa na majuto makubwa maishani mwao.
Lakini pia na wanaume mara nyingi hukabiliana na msongo wa mawazo,majuto ya baadae na mfadhaiko wa akili (depression)
Bila kujali kuwa mwanamke mwenye mimba ni mkewe wa ndoa, mchumba au mchepuko.
Wanaume wengi huchanganyikiwa na kukosa utulivu pale wanaposikia wamesababisha mimba isiyotarajiwa.
Kutokana na uwepo wa sababu mbalimbali ikiwemo hofu ya uchumi,kutokua na mahusiano ya malengo na kadhalika,
Baadhi ya wanaume hupata hisia za hasira na mshangao kwanini imetokea hivyo,
Hupata maswali mengi kuhusu ukweli wa uhusika wa ubaba wao Kwa mtoto atakayezaliwa.
Huhofu kuhusu ukurasa mpya wa majukumu ya ulezi.
Huhofu kuhusu uwajibikaji na Kila kitu kuhusu mtoto atakapozaliwa.
Hali hiyo huwapelekea kukosa majibu mazuri na maamuzi mazuri juu ya hatma ya mtoto aliye tumboni kwa wakati huo.
Katika hali hiyo ya kustaajabisha na kuleta msongo wa mawazo wa muda mfupi,hujikuta katika migogoro na mara nyingi wanawake huamua kuchukua maamuzi magumu ya utoaji mimba au kuzaa na kulea peke yao.
Ikiwa wewe ni mwanaume na uko katika kipindi cha sintofahamu kuhusu mimba.
Zifuatazo ni Njia kadhaa za kukusaidia kufanya maamuzi mazuri yatakayokusaidia wewe pamoja na mwenye mimba yako.
1)KUWA MTULIVU,USICHANGANYIKIWE
Mimba isiyopangwa huleta mshtuko na hisia tofauti k**a vile hasira, usipokua makini mvurugiko huo wa hisia utakupelekea kufanya maamuzi mabaya au kuzungumza vibaya na ikakuletea athari baadae.
Hivyo basi unatakiwa kuwa mtulivu,
Tulia ujipe nafasi ya kutafakari na kuwazua k**a mtu mzima.
Epuka mambo ya kunyoosheana vidole na kumlaumu mwenzako kwasababu swala la mimba linawahusu watu wote wawili.
Hakuna mwanamke anayeweza kujipa mimba yeye mwenyewe.
Nyote wawili mlishiriki katika kupatikana Kwa mimba hiyo.
Njia bora ya kwanza Kwa ajili ya kukabiliana na hali hii ni kuamua kuwa mtulivu na kuacha kuchanganyikiwa.
Katika kipindi cha utulivu utaweza kupata mawazo bora juu ya nini kifanyike kuhusiana na mimba isiyotarajiwa.
2)YAPIME MAAMUZI YAKO
Hata k**a umechanganyikiwa na umejaa maswali mengi kuhusu mimba isiyotarajiwa.
Unapaswa kukubaliana na ukweli kuwa mimba ni yako.
Na k**a unahisi sio ya kwako basi unapaswa kupima maamuzi yako kabla ya kufanya chochote.
Kwanini unashauriwa kupima maamuzi yako?
Kwasababu maamuzi yoyote utakayofanya huwa yana matokeo mawili.
Eidha yakawa na manufaa kwako au yakawa na hasara kwako.
Jiulize yafuatayo kabla ya kuamua.
Ni,wewe ndio unatoa ridhiki kiasi unakataa mtoto asizaliwe kwasababu hauna pesa?
Unayajua madhara anayopata mwanamke kwa utoaji mimba?
Una uhakika wa kesho yako?
Hutaki kabisa kujihusisha na mtoto wako ajaye?
Una uhakika mimba sio yako umesingiziwa?
Una uhakika hutaki mtoto?
Ni kweli huhitaji kumuoa,
Je,huwezi kushirikiana na mama mtoto katika malezi?
Maswali haya yanakusaidia kupima mawazo yako dhidi ya mimba isiyotarajiwa.
Lakini pia ni vyema kujizuia kusema maneno mabaya kipindi hiki.
Ili ujipe muda wa kutosha kupata majibu sahihi.
3)SHIRIKIANA NAE,USIKIMBIE MIMBA
Pengine mmekwishatamkiana maneno mabaya baada ya kujulikana kuwa kuna mimba isiyotarajiwa,ama pengine kabla ya kugundulika kuwa kuna mimba isiyotarajiwa mlimkwazana.
Sasa haipaswi kuendelea kuwa hivyo.
Mnapaswa kushirikiana kwa amani katika uleaji wa mimba hiyo na sio lazima muishi wote ndio mshirikiane.
Inawezakana kuwa ngumu ila jitahidi kwa ajili ya mustakabali wa afya ya mtoto.
Puuzia yaliyokwishatokea iwapo mlikwazana.
Kumbuka kuwa mimba imetengenezwa na watu wawili.
Hivyo sio busara kukimbia mimba.
Shirikianeni katika utunzaji wa mimba hadi mtoto atakapozaliwa.
Zungumzeni kuhusu mipango yenu ya sasa na baadae.
Mnajiona wapi baada ya miaka kadhaa mbele?
Kitu gani mnaweza kufanya ili kusaidiana kila mmoja?
Mtamleaje mtoto?
Mnatamani mtoto aishi katika mazingira yapi?
Mtashirikiana vipi katika malezi iwapo Kila mtu atakua na mwenza mwingine bila mtoto kuathirika?
Mnapaswa kujadili wote kwa hekima na upendo,
Kumbukeni kuzaa sio uadui hivyo haipaswi kuchukiana kipindi chote cha mimba isiyotarajiwa na hata baada ya mtoto kuzaliwa.
4) JIFUNZE KATIKA HILI.
Chochote kile kitakachotokea katika kipindi cha mimba isiyotarajiwa,
Kichukulie kwa jicho la kujifunza.
Fundisho linalopatikana katika kipindi cha mimba isiyotarajiwa ni pamoja na umakini wa kujilinda na kumlinda mwanamke kupata mimba yako,
Kulipa heshima tendo la ngono kwamba halipo tu kwa ajili ya kujifurahisha bali pia tendo hilo huweza kutoa fursa ya kiumbe kuja duniani.
Halikadhalika tukio hili linakufundisha kuhusu matumizi ya njia salama ya kondomu pamoja na Njia salama za uzazi wa mpango.
Lakini pia inakupa nafasi ya kujitambua kuhusu wewe na Yale unayotamani katika maisha yako.
Kupitia kipindi hiki unajigundua k**a kweli unahitaji kuwa baba na lini unatamani kupata mtoto.
Na mambo gani unatamani kufanikisha kabla ya kupata mtoto mwingine?
Hakikisha unajifunza ili usirudie tena kosa k**a hili.
Jukumu la kujilinda na mimba isiyotarajiwa sio la mwanamke peke yake.
-----------------
Sisi,
Ni taasisi isiyo ya kiserikali inayoelimisha,kuwezesha na kutoa usaidizi wa usimamizi kwa wajawazito pamoja na watoto chini ya umri wa miaka 5.
Tunakuambia kila mimba ina haki sawa ya kuzaliwa!
Hakuna swali lenye kukosa majibu.
Tuwasiliane Whatsapp/ujumbe iwapo unahitaji ushauri au una story ya kushea na wengine kuhusu mimba.
Tupe story yako,
Je,wewe ni mtoto uliyetokana na mimba iliyotarajiwa au isiyotarajiwa?
Je, mtoto/watoto ulionao wametokana na mimba iliyotarajiwa au isiyotarajiwa?
Je,umewahi kuwa katika hali ya kuwa na ujauzito usioutarajia?
Je,una ushauri gani Kwa mtu ambaye ana ujauzito asioutarajia?
0746465095
Mkurugenzi
๐๐