Nguzo ya Wanawake

Nguzo ya Wanawake Tunatatua changamoto mbalimbali za kiafya pia tunatoa ushari kwa wanawake na watoto kwa mawasiliano zaidi tupigie 0785438612 au Whatsapp namba 0733021089

23/03/2023

*FAHAMU KUHUSU MAAMBUKIZI KWENYE VIA VYA UZAZI.*

Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.

PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (va**na) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari.

*Dalili Za PID.*
‼️Maumivu – yanayoweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga.
‼️Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya.
‼️Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi.
‼️Maumivu wakati wa kujamiiana
‼️Homa, wakati mwingine kusikia baridi
‼️Maumivu wakati wa haja ndogo, haja ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida.

*Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID, navyo ni:*
‼️Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono
‼️Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja
‼️Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja
‼️Kufanya mapenzi bila kinga
‼️Kujisafisha na sabuni zenye kemikali ndani ya uke mara kwa mara
‼️Kuwa uliwahi kupata PID kabla au magonjwa mengine ya ngono

*Madhara yatokanayo na PID pamoja na:*
‼️Mimba nje ya mirija (ectopic pregnancy). PID ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi.
‼️Ugumba. Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha kushindwa kupata ujauzito.
‼️Maumivu sugu ya nyonga. PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu kwa miaka mingi.
‼️Tubo-ovarian abscess. PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya njia ya uzazi.

*Hatua 6 za Kujikinga dhidi ya Harufu Mbaya Ukeni.*
‼️Vaa nguo za ndani za pamba, zisizobana sana.
Nguo zilizoabana zinazuia kupita kwahewa safi kuelekea ukeni na hivo kusababisha unyevunyevu ambao ni mbolea kwa bacteria na fangasi wanaoleta harufu mbaya kwenye uke. Hakikisha unabadilisha chupi kila baada ya masaa 12 inasaidia kuzuia kukua kwa bacteria wabaya.

‼️Badili Nguzo zako Kila Baada ya Kufanya Mazoezi
Nguo zenye unyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bacteria hivo hakikisha unavaa nguo zilizokauka na kubadilisha kila baada ya kutoka mazoezini.

‼️Punguza uzito k**a inawezekana
Uzito mkubwa na kitambi vinakufanya utokwe na jasho kwa wingi zaidi hasa kwenye uke. Na k**a tulivojifunza pale juu, jasho na unyevunyevu inaleta fangasi na bacteria wabaya. Chagua kula lishe nzuri na kufanya mazoezi ili kurekebisha mwili wako.

‼️Epuka Kuflash Uke Kila Mara (Douching)
Kusafisha uke kila mara hasa kwa kutumia kemikali na sabuni inaharibu mazingira ya bacteria wazuri. Bakteria hwa ni walinzi, na hivo kuacha nafasi kwa uke kushambuliwa na bacteria wabaya pamoja na fangasi wa candida.

‼️Epuka Kutumia Spray na Marashi Ukeni
Ukweli ni kwamba ngozi ya uke ni laini sana kwa hiyo inanyonya kwa urahisi kemikali zilizopo kwenye spray kuingia kwenye damu. Usiingie kwenye mtego huu, kumbuka miili yetu imeumbwa kujisafisha yenyewe, Pale unapoongeza kitu cha ziada basi unaharibu normal flora na kuharibu kinga ya mwili.

‼️Epuka Baadhi ya Vyakula Ambavyo ni Adui wa afya yako
Kuna aina nyingi ya vyakula ambavyo vianweza kukuathiri wewe k**a mwanamke kwenye swala la uzazi. Vyakula hivi vinaharibu mazingira ya uke, kuua bacteria wazuri na kubadili PH. Vyakula vyenye sukari, Pombe, ngano na vyakula vilivyosindikwa huchochea ukuaji wa fangasi wa Candida.

Kumbuka:p.i.d huwa haiambukizwi na NGONO tu Bali p.i.d huwa inasababiswa na maambukuzi ya bakteria wabaya , ndo MAANA hata bikra anaweza KUPATA maambukuzi KWA sababu maambukuzi ya bakteria wabaya, anaweza kuyapata chooni na hata pale asidi ya uke unapokuwa imeshuka.

Kingine p.i.d haisababishwi peke yake na bakteria wabaya Bali kila kimelea kinachoingia kwenye mfumo was uzazi husababisha p.i.d inaweza KUWA Fung, virus na hata plotozoa.

WOMAN CARE PACKAGE itakayokusaidia kumaliza tatizo la PID,FANGASI SUGU NA UTI.
Hivyo kuondoa changamoto k**a;
‼️Kutokwa na uchafu usio wa kawaida.
‼️ Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
‼️Harufu mbaya ukeni.
‼️Kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.
‼️Miwasho sehemu za siri.
‼️ Maumivu wakati wa choo kidogo.
‼️ Maumivu makali ya tumbo la chini kulia na kushoto

Kwa mawasiliano zaidi 0768979645
Dr Roda

AFYA KWETU NI BASHASHA 🦋

Shuhuda ya mama aliyekuwa na uvimbe👇👇
08/02/2023

Shuhuda ya mama aliyekuwa na uvimbe👇👇

*MAGONJWA YANAYOSABABISHA WANAWAKE KUWA WAGUMBA*+255785438612P.I.D(pelvic inflammatory disease) na FIBROIDS inavyotesa w...
07/02/2023

*MAGONJWA YANAYOSABABISHA WANAWAKE KUWA WAGUMBA*

+255785438612

P.I.D(pelvic inflammatory disease) na FIBROIDS inavyotesa wanawake na kuwasababishia ugumba.

P.I.D NI NINI ?

P.I.D ni maambukizi kwenye via vya uzazi wa mwanamke. Ugonjwa huu unaweza kupelekea uharibifu mkubwa kwenye mayai,mfuko wa uzazi,mirija ya uzazi nk . Pia ugonjwa huu ni moja ya UGUMBA kwa mwanamke. Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kutotibu magonjwa ya zinaa kwa ufasaha na kuacha wale bakteria kuendelea kusambaa kwenye via vya uzazi wa mwanamke.

Je utajuaje kwamba huenda umeathirika na ugonjwa huu wa P.I.D ?

DALILI ZA P.I.D
👉Maumivu ya tumbo sehemu ya chini au ya juu upande wa kulia
👉Kutokwa kwa uchafu ukeni usio wa kawaida na harufu mbaya(wengi hudhani ni fangas kumbe sio)
👉Maumivu makali na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Kutapika na homa
👉Uchovu
👉Kutokwa kwa damu nyingi isiyokuwa na mpangilio wakati wa hedhi au wakati sio wa hedhi( hii dalili kubwa na huwa inafanana sana na fibroids)
👉Ugumba( unatafuta mtoto kwa muda mrefu na hupati)
👉Kukojoa mara kwa mara

FIBROIDS NI NINI ?
FIBROIDS ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambapo uvimbe huu unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi au nje kwenye ukuta wa kizazi

Je utajuaje k**a una fibroids ?? Hebu angalia dalili zake

DALILI ZA FIBROIDS
👉Kutokwa damu nyingi kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi au wakati wa hedhi
👉Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya(wengi wenu huwa mnakimbilia kwamba mna fangas)
👉Maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe
👉Tumbo kuuma sana chini ya kitovu
👉Hedhi zisizokua na mpangilio na damu hutoka nyingi mpaka kupelekea wengine kupungukiwa damu na kutakiwa kuongezewa damu
👉Maumivu wakati wa tendo la ndoa(hii hupelekea achukie tendo la ndoa)
👉Kukosa kwa choo kikubwa au choo kuwa kigumu(constipation. )
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Kukojoa mara kwa mara
👉Ugumba(kuchelewa au kutokupata mtoto)
👉Mimba kutoka mara kwa mara

KWANINI NIMEAMUA KUELEZEA KUHUSU P.I.D NA FIBROIDS????

JIBU:
👉Ni kwa sababu wanawake wengi wakiona dalili k**a kutokwa uchafu wanahisi ni FANGAS tu
👉 Wakiona mimba zinatoka mara kwa mara wengi hukimbilia kusema ni ushirikina au muhusika alikua anatoa mimba sana siku za nyuma wakati labda sio hivyo
👉Kingine mwanaume akiona mkewe hataki tendo la ndoa anahisi mkewe anamsaliti kumbe mwenzie anaumwa
👉 Lakini kubwa zaidi nimeeleza haya yote sababu dalili za magonjwa haya mawili yanafanana kwa ukaribu sana

Nimewasaidia wanawake wengi kutatua changamoto hizo na wakaweza kushika ujauzito🤰🤰

Kwa ushauri zaidi tupigie Kwa namba 0785438612 au tuma ujumbe WhatsApp Kwa namba hiyo

Afya kwetu ni Bashasha🦋

P. I. DMaambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni+255785438612Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke au ugonjwa wa PI...
07/02/2023

P. I. D
Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni

+255785438612

Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke au ugonjwa wa PID (pelvic inflammatory disease) ni maambukizi ya bakteria kwenye shingo ya uzazi, mirija ya fallopio, ovari na tumbo la uzazi (uterasi).
Sababu kuu ya ugonjwa huu kutokea ni maambukizi yanayosambazwa kwa kujamiiana (STI). Ugonjwa huu unaweza kuwaathiri wanawake wenye umri wowote, lakini wale wenye umri kati ya maika 15 na 24 huathirika zaidi.
Dalili huweza kujumuisha: maumivu ya nyonga au tumbo, maumivu wakati wa kujamiiana, na uchafu usio wa kawaida kutoka ukeni pamoja na homa. PID hutibiwa kwa antibiotiki, na utambuzi na matibabu ya mapema ni muhimu katika kuzuia madhara ya kupata makovu na utasa.

Vihatarishi vya ugonjwa wa PID

Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni semi ya kitabibu inayoelezea maambukizi ya shingo ya uzazi, tumbo la uzazi na mirija ya fallopio. Kwa kawaida maambukizi haya husababishwa na bakteria.
Ingawa mara nyingi ni maamkubizi yanayosambazwa kwa njia ya kujamiiana (STI), k**a vile klamidia au kisonono, wakati mwingine maambukizi haya huweza kusababishwa na bakteria wengine. PID inaweza kuwaathiri wanawake wenye umri wowote, lakini wale wenye umri kati ya miaka 15 and 24 huathirika zaidi.

Dalili za PID

Dalili huweza kujumuisha:

Maumivu kwenye nyonga na tumbo

Maumivu wakati wa kujamiiana

Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi

Kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida ukeni

Baadhi ya watu huweza kupata homa, kichefuchefu, kutapika au maumivu wakati wa kujisaidia.

Watu wengi hupona vizuri baada ya matibabu na maambukizi hayasababishi matatizo ya muda mrefu. Hata hivyo, ikiwa maambukizi hayatatibiwa, au ikiwa mtu anayapata maambukizi haya tena baada ya kutibiwa, basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata madhara zaidi. Haya huweza kujumuisha makovu kwenye tumbo la uzazi na mirija ya fallopio, ugumu wa kupata mimba, mimba kutungwa nje ya tumbo la uzazi, na maumivu ya muda mrefu ya nyonga.

Kinga

Njia muhimu ya kuzuia maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni kutumia kondomu wakati wa kujamiiana. Kondomu ni njia bora ya kuzuia kupata maambukizi yanayosambazwa kwa njia ya kujamiiana (STIs). Watu waliotambuliwa kuwa na STI wanapaswa kuwataarifu wapenzi wao ili wapimwe na kutibiwa pamoja

KWA MAELEKEZO NA USHAURI JUU YA SULUHISHO LA TATUZO LA P.I.D WASILIANA NASI KWA +255 785438612(kawaida na WhatsApp)

Afya kwetu ni Bashasha🦋

KWA NINI VINATOKA VINYAMANYAMA AU MABONGE YA DAMU WAKATI WA HEDHIKwa asili, wanawake wengi huwa wanapatwa na hali hii ya...
07/02/2023

KWA NINI VINATOKA VINYAMANYAMA AU MABONGE YA DAMU WAKATI WA HEDHI

Kwa asili, wanawake wengi huwa wanapatwa na hali hii ya mabonge wanapokuwa hedhini, ni jambo ambalo huwastusha wengi na hutufanya kuwa na maswali k**a vile •Kwa nini mwanamke anatokwa na damu iliyoganda wakati wa hedhi?
•Ni kipi hasa husababisha damu kuganda wakati wa hedhi?

Leo nipo kwa ajili ya majibu.

~~Kwa ujumla, chanzo cha kuganda kwa damu wakati wa hedhi yako hutokana na kushindwa kutoka kwa ute wenye kemikali unaozuia kuganda kwa damu kibaolojia huitwa anticoagulants......
ambapo kazi ya ute huu ni kuukinga ukuta wa kizazi usiharibike.

Wakati wa hedhi, ute mzito unakuwa kwenye ukuta wa kizazi huanza kutoka. Ute huu unaokuwa na kemikali huanza kuachiliwa ili kuzuia damu isigande wakati wa hedhi. Wanawake wengi wanaotokwa na damu ya hedhi muda mrefu hutoka na damu yenye mabonge kwa sababu damu inayotoka kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus) hutoka kwa kasi kuliko ute wenye kemikali ya kuiyeyusha isigande. Hali hii ndio husababisha damu kuganda na hedhi kutoka na mabonge ya damu kwa muda mrefu.

Visabibishi vya kupungua kwa ute huu (anticoagulants) ni uwepo wa tatizo katika kizazi mfano.

1️⃣ *Uvimbe Katika Kizazi (Uterine Fibroids)*
Uvimbe mmoja au zaidi ambao huwa sio saratani, kwa kawaida huota ndani ya kizazi cha mwanamke. Hata hivyo kwa kuwa sio saratani, huwa havionyeshi kuwa vimetulia tu. Dalili za kawaida anazozipata mwanamke mwenye uvimbe aina ya fibroids ni k**a ifuatavyo:
•Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
•Maumivu wakati wa tendo la ndoa
•Kutokwa na damu ya hedhi muda mrefu
•Tumbo kujaa gesi ama kukosa choo

2️⃣. *Matumizi ya njia za Kisasa za Uzazi Wa Mpango*

Dhumuni kuu la njia za kisasa za Uzazi wa mpango ni kuvuruga mpangilio wa homoni za mwanamke. Kivurugika kwa homoni hauharibu tu ukomavu wa mayai bali huharibu vichochezi vya homoni hasa oestrogens na progesterone ambazo ni muhimu katika kuzalisha ute, mayai na ujauzito kwa ujumla.
*JICHUNGUZE*
Ikiwa k**a unapaswa kubadilisha pedi zaidi ya mara moja kila baada ya masaa mawili au k**a mtiririko wa damu yako ya hedhi una mabonge makubwa ya damu yasiyokuwa ya kawaida, basi ina maanisha kwamba unatokwa na damu nyingi mno.
Endapo k**a utagundua kuwa mtiririko huo wa damu ulianza tu kipindi ulipoanza kutumia aina mpya ya vidonge vya mpango wa uzazi, basi unapaswa umweleze daktari wako akupe usahuri kuhusu jambo hilo.

3️⃣. *Kuporomoka Kwa Mimba (Miscarriage)*

4️⃣. Maambukizi
Aina ya kwanza ya maambukizi yanayoweza kusababisha hali hii ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi ni maambukizi katika via vya uzazi(P.I.D). Maambukizi ya aina hii huathiri viungo vya uzazi kwa mwanamke, na k**a tatizo hili litaendelea bila kufahamika vizuri, basi linaweza kusababisha uharibifu mkubwa katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.

5️⃣. *Kufanya kazi mzito nyakati za hedhi.*
Hili siyo lupelekea maumivu na mabonge zaidi bali hupelekea damu ya hedhi kutirirka k**a bomba yaani unaweza kubadili pads hata 3 hadi 4 kwa siku

Uonapo dalili za kuwa mabonge wakati wa hedhi unaweza kumuona daktari wako kwa vipimo zaidi ila k**a umegundua tayari una mojawapo ya magonjwa hapo juu au umewahi kutumia uzazi wa mpango, jitahidi kutumia vyakula au vinywaji vyenye kukusaidia kuweka homoni sawa na kuyeyusha damu ili isikwame katika mfumo wa uzazi.

Muhimu k**a umegundua una matatizo katika uzazi ni vyema kuanza dozi yako ya kusafisha NJIA za Uzazi na kuweka homoni sawa ili uendelee kuwa na mrejesho mzuri siku zote.

Yapo mengi ya kuzungumza kuhusu uzazi hatuwezi kumaliza leo,....
Ila tutakuwa na muendelezo kila siku kujuzana kupitia channel hii

Kwa ushauri zaidi tupigie 0768979645 au tuma ujumbe Kwa namba hii

Afya kwetu ni Bashasha🦋

Moja ya changamoto ambaz9 ni sugu kwa wanawake kwa sasa ni utokwaji wa mqjimaji yasiyo yakawaida hii ni kwasababu ya uwe...
07/02/2023

Moja ya changamoto ambaz9 ni sugu kwa wanawake kwa sasa ni utokwaji wa mqjimaji yasiyo yakawaida hii ni kwasababu ya uwepo wa maradhi k**a vile PID, chango la uzazi, Hormonal imbalances, maabukizi ya Fangasi ukeni, UTI Sugu

Madhara ya halii ni kupelekea ugumu wa kushindwa kufurahia tendo, maumivu wakati wa tendo, kukosa ute wa uzazi na mirija kuziba hali ambayo hupelekea Ugumba wa kudumu.

Moja ya dalili za kuwa na uchafu au majimaji yasiyo ya kawaida ukeni
Ni
🩺 Kutokwa uchafu /majimaji mithiri ya maziwa mepesi au maziwa mtindi
🩺 kutokwa majimaji mithiri ya parachichi lililoiva sana
🩺 kutokwa majimaji yenye rangi kijani au njano
🩺 kutokwa uchafu au majimaji yenye rangi ya kijivu au tope
🩺 kutokwa garufu mbaya mithiri ya shombo la samaki
🩺 kutokwa uchafu majimaji mfano wa tope wakati wa tendo
Dalili nyingine zinategemeana na hatua ya hali ilipofikia na hali ya mtu aliyopo...

Kwa msaada wa elimu , ushauri na matibabu ya uhakika juu ya hali hii unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi ili uweze kufika kituoni kwetu kwaajili ya tiba, pia kwa walioko mikoani Dawa zetu tunatuma na kuendelea kufanya follow-up hadi mgonjwa anapopata matokeo +255785438612

AFya kwetu ni Bashasha 🦋

ZIJUE FAIDA ZA MAMA KUNYONYESHA KIUSAHIHIUkweli kuhusu umuhimu wa kunyonyesha:Kunyonyesha ni moja ya njia sahihi ya kuha...
07/02/2023

ZIJUE FAIDA ZA MAMA KUNYONYESHA KIUSAHIHI

Ukweli kuhusu umuhimu wa kunyonyesha:

Kunyonyesha ni moja ya njia sahihi ya kuhakikisha mtoto anakuwa mwenye afya na kuendelea kuishi.

K**a viwango vya kunyonyesha vingekuwa vya hali ya juuduniani , takriban maisha 820 000 ya watoto yangenusurika kila mwaka, linasema shirika la afya duniani (WHO).

Unyonyeshaji wa mtoto kwa miezi 6 kuna faida nyingi za kiafya kwa mama na mtoto.

Kumnyonyesha mtoto mara anapozaliwa kwa kipindi cha saa moja, humkinga kwa maambukizi yanayowapata watoto wachanga na kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Maziwa ya mama pia ni chanzo muhimu cha nguvu na virutubisho kwa watoto wa kati ya miezi 6 hadi 23.

Maziwa ya mama yanaweza kuchangia nusu au zaidi ya nguvu za mtoto katika umri wa miaka 6 hadi 12

Watoto na vijana wadogo walionyonyeshwa wakiwa wachanga wana uwezekano mdogo wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia .

Unyonyeshaji wa mtoto humsaidia kuboresha uwezo wa utambuzi wa akili (IQ), mahudhurio ya shule , na pia huhusishwa na mapato ya juu katika maisha yake ya utu uzima.

Kunyonyeshwa kwa muda mrefu pia huchangia afya na maisha bora ya mama kwani humpunguzia hatari ya kupata saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi na matiti.

Kunyonyesha hutengeneza vichocheo vyamwili( hormone) ambazo humtuliza mama na mtoto

Juma hili linaadhimishwa huku baadhi ya wanawake duniani wakishindwa kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo kutokana na sababu mbali mbali. .

Licha ya juhudi mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanyika kuelemisha wakina mama na jamii nzima juu ya umuhimu wa kunyonyesha na maziwa ya mama kwa mtoto, baadhi ya mila na tamaduni hususan za Kiafrika zimekuwa na changangoto kubwa ya kuelewa na kukubali umuhimu wa kunyonyesha kutokana na kukosa elimu ya kunyonyesha.

Miongoni mwa changamoto zinachangia wanawake kushindwa kuwanyonyesha watoto wao ni pamoja na kazi, magonjwa pamoja na tamaduni nyingi zisizomruhusu mwanamke kunyonyesha maeneo ya umma.

Hivi karibuni mwanamke mmoja nchini Kenya alifukuzwa kwenye mgahawa jijini Nairobi alipokuwa akimnyonyesha mwanae ndani ya mgahawa huo.

👉Aidha baadhi yao wamekuwa na imani potofu kuhusu suala zima la kunyonyesha na faida zake. Hili limechangia pakubwa katika kudhoofisha jitihada za kuhakikisha kila mama mwenye mtoto mchanga anamyonyesha ipasavyo.

Baadhi ya imani potofu kuhusu kunyonyesha:

Maziwa ya kwanza ya mama si mazuri kwa mtoto yanapaswa kumwagwa

Kunyonyesha humfanya mama anenepe kupindukia

maziwa ya mama pekee hayawezi kumridhisha mtoto wa umri wa miezi 0 hadi sita.

Baadhi ya vyakula si vizuri kwa wanawake wanaonyonyesha

Ni lazima mtoto mchanga anywe maji mara baada ya kuzaliwa

Maziwa ya mama humfanya mtoto ajihisi mwenye kiu

Baadhi ya wanawake hudai wanaponyonyesha matiti yao husinyaa na kuanguka.

Shirika la watoto la Save the Children linasema kuwa watoto wenye utapiamlo unaochangiwa na kutonyonyeshwa ipasavyo unakadiriwa kusabisha vifo vya watoto 2.7 kila mwaka.

Wataalam wanasema mguso wa mwili kwa mwili pamoja na kunyonya husaidia kuchochea uzalishaji wa maziwa ya mama , yakiwemo maziwa ya mwanzo kabisa ya mama baada ya kujifungua ambayo hutambuliwa k**a''chanjo ya kwanza'' , yenye virutubisho vingi pamoja na kinga ya ya mwili.

KWA USHAURI ZAIDI TUPIGIE 0785438612 AU TUMA UJUMBE WHATSAPP KWA NAMBA HII

AFya kwetu ni Bashasha🦋

Kwa ushauri zaidi tupigie Kwa namba 0785438612 au tuna ujumbe Whatsapp Kwa namba hiiAfya kwetu ni Bashasha 🦋
07/02/2023

Kwa ushauri zaidi tupigie Kwa namba 0785438612 au tuna ujumbe Whatsapp Kwa namba hii

Afya kwetu ni Bashasha 🦋

Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana k**a ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli l...
07/02/2023

Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana k**a ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

👉🏼 *_HAYA NI MOTEO YA TISSUE MPYA ZINAZO OTA K**A NYAMANYAMA MPYA SEHU AMBAYO HAIKUPASWA KUOTA NYAMANYAMA_*
Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.

Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa k**a maji tu na kurudi tena kuwa mgumu. *(MAANA YA WAZI NI KUWA HAIMAANISHI KUWA UKIGUNDULIKA LEO KUWA UNA FIBROIDS BASI HAIMAANISHI KUWA UNA KANSA YAANI SARATANI HAPANA)*

Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: *‘UTERINE FIBROIDS* ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’.

Hujulikana pia k**a ‘LEIOMYOMA ’ katika lugha ya kidaktari.

*_👉🏼👌🏼LEIOMYOMA huwapata wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 kwa wanawake na ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu._*

Chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu au vichochezi vya kutokea huu uvimbe ni pamoja na;

🧎🏽‍♂️😩 Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini.

😩🤰🏽 Ujauzito. *_(yaani kipindi cha ujauzito kuna hormone huwa na tendency ya kuongezeka zaidi hivyo kuchochea uvimbe kuota kwenye kizazi, lakini bado hii haimaanishi kuwa ujauzito ni sababu ya kupata fibroids maana bado pia sababu hii ona asilimia chache sana kulinganisha na sababu zingine)_*

🥴🤦🏽‍♂️. Uzito na unene kupita kiasi. Hii ni kwakuwa mtu mwenye uzito mwingi kuna baadhi ya mifumo hushindwa kufanya kazi zake kiusahihi na mrundikano wa sumu nyingi mwilini hupelekea pia kuwa uzito mwingi, pia uzito unahusanishwa na baadhi ya vichocheo vinavyohamasisha kukuwa kwa fibroids.

*🧬🦠 GENETICS DISORDERS* Jenetic zenye hitilafu au kurithi vinasaba kimakosa (mfano kurithi vinasaba vyenye kujenga upande wa maumbile na hormones za kiume zaidi huchangia kupelekea uvimbe kwenye kizazi.

🧎🏽‍♂️♻️ Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu.

🤱🏽🧎🏽‍♂️ Sababu za kurithi.
🥴🧎🏽‍♂️. Lishe isiyo sawa hasa wale wanaopendelea vyakula vya wanga sana na mkaango wa haraka pia na mafuta ya wanyama hasa nyama nyekundu inahusanishwa na kupelekea ama kuchochea tatizo la fibroids.

♻️🎊. SUMU NA TAKA MBALIMBALI (k**a nilivyoelezea kwenye sababu ya uzito mwingi)

🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️🫵🫵🫵🫵🫵🥴
*DALILI ZINAZOONESHA UVIMBE KWENYE KIZAZI NI PAMOJA NA HIZI ZIFUATAZO JAPO MAELEZO MENGINE NITATUMA KWENYE PARAGRAPH INAYOFUATA;*

👉🏼😩. Kupata damu nyingi wakati wa hedhi.
👉🏼😩. Maumivu makala wakati wa siku za hedhi.
👉🏼😩. Kuvimba miguu.
👉🏼😩. kuhisi una ujauzito.
👉🏼😩. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
6. Kuhisi kuvimbiwa.
7. Kupata haja ndogo kwa taabu.
8. Kutokwa na uchafu ukeni.
9. Kupata choo kigumu au kufunga choo.
10. Maumivu nyuma ya mgongo.
11. Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto.
12. Upungufu wa damu.
13. Maumivu ya kichwa.
14. Uzazi wa shida.
15. Kutopata ujauzito.
16. Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo.
👉🏼😩Maumivu ya nyonga.
👉🏼😩 Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage).

Aina za Uvimbe kwenye kizazi

Kuna aina kuu nne za Fibroids

*♻️. INTRAMURAL FIBROIDS:-* _Hutokea kwenye kuta za mji wa mimba (uterus). Wanawake wengi hupatwa na aina hii ya uvimbe kwa kiasi kikubwa kesi nyingi za uvimbe kwenye kizazi huwa ni zile za aina hii ambayo ni intramural_

*♻️. SUBSEROSAL FIBROIDS:*
*_Hii hukua nje ya kuta za mji wa mimba na hukua na kuwa kubwa sana._*

*♻️. SUBMUCOSAL FIBROIDS:*
*_Hutokea kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za mji wa uzazi._*

*♻️. CERVICAL FIBROIDS:* Hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).

Kwa ushauri zaidi tupigie Kwa namba 0785438612 au tuna ujumbe Whatsapp Kwa namba hii

Afya kwetu ni Bashasha🦋

Kwa ushauri zaidi piga namba 0785438612 au tuna ujumbe WhatsApp Kwa namba hiiAfya kwetu ni Bashasha 🦋
07/02/2023

Kwa ushauri zaidi piga namba 0785438612 au tuna ujumbe WhatsApp Kwa namba hii

Afya kwetu ni Bashasha 🦋

Tatizo la uvimbe kwenye kizazi (fibroids)      0785438612/0785438612ni kubwa na linawatokea wanawake wengi sana. Inakadi...
07/02/2023

Tatizo la uvimbe kwenye kizazi (fibroids)

0785438612/0785438612

ni kubwa na linawatokea wanawake wengi sana. Inakadiriwa kwamba 75% ya wanawake hupata tatizo hili la fibroids katika kipindi flani cha maisha yao. Kwa mujibu wa jarida la New England Journal of Medicine, kila mwaka zaidi ya wanawake 200,000 wanafanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi chote (hysterectomy) kutokana na tatizo hili la fibroids.

Fibroids ni nini?
Fibroids ni uvimbe usio wa saratani ambao hujitokeza kwenye kuta za mfuko wa mimbauitwao uterusi. Uvimbe huu husababisha kubadilika kwa shape na size ya kizazi na pia dalili zingine mbaya. Wanawake wengi huanza kupata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na uwepo wa uvimbe kwenye kizazi(fibroids . Ni jambo la msingi zaidi kwa wanawake wote kuchukua hatua katika kuzuia kutokea kwa fibroids.

Tafiti mbalimbali zinaonesha kwamba kuzuia au kutibu tatizo la kupanda kwa presha ya damu husaidia kupunguza hatari ya kupata uvimbe kwenye kizazi (fibroids). Utafiti uliofanyika katika chuo kikuu cha Havard unasema kuna uhusiano mkubwa kati ya presha ya damu na hatari ya kupata uvimbe kwenye kizazi(fibroids) kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi.

Unajuaje k**a tayari una uvimbe kwenye kizazi (fibroids)
Je fibroids inaweza kusababisha kuvuja damu, maumivu ya mgongo na dalili zingine mbaya? Inawezekana kabisa lakini siyo kila mwanamke mwenye fibroids hupata dalili hizi, lakini pia uwepo wa dalili hizi siyo lazima kwamba una fibroids.

Unaweza kuwa na tatizo lingine la kiafya, ushauri mzuri ni kuonana na dactari haraka ili kupata vipimo. Zifuatazo ni dalili zinazojitokeza kwa wanawake wengi zaidi wenye uvimbe kwenye kizazi

Kupata Hedhi inayochukua siku nyingi kuanzia 7 na zaidi
Hedhi nzito
Kujiskia umeshiba mda mwingi
Maumivu ya nyonga
Kupata mkojo mara kwa mara na kushindwa kutoa mkojo wote kwenye kibofu.
Kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu
Kupata maumivu wakati watendo la ndoa
Maumivu chini ya mgongo na kwenye miguu.
Madhara mbalimbali ya uzazi k**a ugumba na mimba kutoka.
Uvimbe kwenye kizazi(fibroids) wakati wa ujauzito
Wakati mwingine mwanamke anaweza kupata fibroids akiwa kwenye ujauzito, ni dalili gani zinaweza kujionesha? Uvimbe kwenye kizazi(fibroids) inaweza kusababisha shida wakati wa kujifungua na kupelekea mwanamke kujifungua kwa upasuaji.

Inaweza kupelekea ugumba pia k**a tatizo ni kubwa sana kutokana na ugumu kwa yai kurutubishwa na kisha kujishikiza kwenye ukuta wa uterus.

Kwa wanawake ambao bado hawajazaa hushauriwa kutumia dawa ili kupunguza ukubwa wa uvimbe kabla ya kupata ujauzito. K**a tatizo ni kubwa zaidi basi upasuaji hufanyika kabla ya kushika mimba. Kumbuka ni vizuri kufanya vipimo kabla hujaamua kushika ujauzito, hii itakusaidia kupunguza hatari ya kumpoteza mtoto.

Fibroids huweza kuongezeka ukubwa wakati wa ujauzito kutokana na kiasi kikubwa cha homoni ya estrogen. Kuvuja damu na maumivu ya tumbo pia huweza kutokea kutokana na uvimbe kupoteza damu yake. Kwahiyo madaktari wa wanawake hupendekeza mgonjwa kufanyiwa ultrasound mara kwa mara ili kufatilia maendeleo ya uvimbe.

Aina za uvimbe kwenye kizazi(fibroids)
Jina la kitabibu la fibroids ni leiomyoma au myoma. Ukubwa, mahali ulipo uvimbe na pia idadi ya vimbe hizi inachangia zaidi kwenye uwepo wa dalili mbaya aatakazopata mwanamke. Inawezekana kabisa kuwa na aina zaidi ya moja ya fibroid katika mda mmoja k**a zitatokea mahali tofauti tofauti kwenye uzazi wa mwanamke. Aina kuu za uvimbe kwenye kizazi(fibroids) ni k**a zifuatazo

Intramural fibroids; ni aina maarufu zaidi na zinawatokea zaid wanakwake. Aina hii ya fibroid hukua na kumea kwenye misuli ya ukuta wa uterus. Kadiri zinavokua basi husababisha kupanuka au kuvutika kwa kizazi na kusababisha dalili k**a hedhi ya muda mrefu inayoambatana na maumivu ya nyonga.

Subserosal fibroids: aina hii ya fibroids hukua nje ya ukuta wa mfuko wa mimba, wakati mwingine kuelekea kwenye kibofu cha mkojo. Aina hii ya fibroids huweza kusababisha maumivu ya chi ya mgongo kutokana na kwamba uvimbe huu unasukuma neva za uti wa mgongo na kusababisha presha kubwa kwenye eneo la chini ya mgongo.

Submucosal fibroids: aina hii ya fibroid hukua karibu na ukuta wa kizazi. Inaweza kusababisha bleed ya muda mrefu na shida kwenye kushika ujauzito.

Cervical fibroids: hizi hukua kwenye tishu za mlango wa kizazi ambao huitwa cervix. Hutokea mara chache sana ukilinganisha na aina zingine za fibroids.

Vihatarishi gani vinaongeza uwezekano wa kupata fibroids?
Mambo yafuatayo yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata uvimbe kwenye kizazi

Kurithi: k**a mama au dada yako aliwahi kuugua tatizo hili basi wewe pia utakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe huu.
Umri: uvimbe kwenye kizazi (fibroids) hutokea zaidi kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi kuanzia miaka 35 mpaka 40.
Lishe: matumizi ya vyakula vya wanga na sukari kupita kiasi huongeza hatari ya kupata fibroids
Uzito mkubwa na kitambi: wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wako kwenye hatari zaidi ya kupata fibroids .
Wanawake wenye shinikizo kubwa la damu
Matumizi ya njia za kupanga uzazi: k**a vidonge huongeza ukuaji wa fibroids kwani vidonge hivi huweza kupandisha homoni ya estrogen kwa wingi
Kubalehe mapema: wanawake wanaobalehe mapema na kuanza kupata hedhi chini ya miaka 10 wako kwenye hatari zaidi ya kuugua fibroids na
Wenye matatizo ya tezi ya Thairodi
Hatua saba za kuepuka na kutibu uvimbe kwenye kizazi (fibroids)
Hatua ya kwanza: Epuka vyakula vyote vinavyoongeza ukubwa wa tatizo: vyakula vya kupiga chini ni k**a vifuatavyo.
Vyakula vyenye mafuta mabaya na vilivyosindikwa: mfano nyama zilizosindikwa , baga na suausage huongeza mpambano (inflammation) na aleji. pia vyakula vilivyosindikwa vina kiasi kingi cha kemikali zinazowekwa ili kuongeza ladha hivo unapofanya uchaguzi wa nyama basi hakikisha unakula nyama kutoka kwa mnyama aliyefugwa kwa kula majani na siyo nafaka.
Maziwa yaliyosindikwa na kuhifadhiwa kwenye makopo: maziwa haya yana homoni nyingi za steroids na kemikali pia ambazo zinabadili ufanyaji kazi wa homoni zako za mwili na hivo kuongeza ukuaji wa fibroids.
Sukari: matumizi ya sukari kwa wingi iwe imesindikwa au ya asili huongeza mpambano kati ya tishu za mwili na kinga ya mwili na hivo kusababisha kuvimba au kututumka kwa tishu . hii huongeza maumivu na kupunguza uwezo wa kinga ya mwili. Unaweza kusoma vizuri uhusiano kati ya kuvurugika kwa homoni, kuongezeka uzito na uvimbe kwa kubonyeza hapa.
Wanga iliyokobolewa sana; katika kupambana na tatizo la uvimbe kwenye kizazi basi hakikisha unapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vyakula vyenye wanga kwa wingi maana vyakula hivi hupandisha insulin nyingi kwenye damu na kuongeza hatari ya kupata uvimbe
Pombe na vinywaji vyenye caffeine. Matumizi makubwa ya pombe huongeza mcharuko au kututumka kwa tishu kwenye mwili . pombe pia huzorotesha kinga ya mwili na kusababisha uzito mkubwa na kuvurugika kwa homoni, unaweza kusoma makala yetu kuusu kuvurugika kwa homoni za k**e na suluhisho lake jikoni kwa kubonyeza hapa.
Hatua ya pili : Kula kwa wingi vyakula vya kukusaidia kutibu na kupunguza makali ya uvimbe.: vyakula hivi ni k**a.
Vyakula vilivyoandaliwa pasipo matumizi ya kemikali (organic foods), sababu ni k**a tulivoona hapo juu kwamba kemikali hizi zilizosheheni kwenye dawa za kuua wadudu zinaharibu mpangilio wa homoni na kusababisha seli za mwili kukua ovyo bila mpangilio. Kuhusu matunda na mbogamboga basi hakikisha unaosha kwa maji ya uvuguvugu yaliyochangnywa na vinegar hii husaidia kutoa kemikali za sumu zilizoganda kwa juu.
Mbogamboga za kijani : mboga za kijani zina viambata vinavyoondoa sumu kwenye mwili . pia mbogamboga za kijani zina Vitamin K kwa wingi sana ambazo husaidia katika kuganda kwa damu na hivo kusaidia kwenye bleeding.
Vyakula vyenye beta carotene kwa wingi na madini ya chuma: Mwili una uwezo wa kubadilisha beta carotene kuwa Vitamin A , na kazi ya vitamin A ni kujenga seli mpya zilizokufa na hivo kusaidia wenye fibroids.
Baadhi ya vyakula vyenye beta carotene kwa wingi ni Nyanya, karoti na spinach. Kutokana na kwamba fibroid husababisha wanawake kupoteza damu nyingi kwa wakati fulani hivo ni muhimu kutumia vyakula k**a maini, fogo, moyo ili kuongeza uzajishaji wa madini chuma ambayo husaidia katika utengenezwaji wa seli mpya nyekundu za damu.
Hatua ya tatu: Jaribu kutumia baadhi ya virutubisho kwa ajili ya kupungeza ukubwa wa uvimbe; hakikisha unapata ushauri wa daktari kabla ya kuanza kutumia virutubisho hivi,
Mafuta ya samaki(fish oil) au mafuta ya flaxseed, kijiko kimoja kwa siku inaweza kusaidia kpunguza mcharuko kwenye mwili na hivo kusaidia kupunguza uvimbe kwenye kizazi
Vidonge vya vitamin B complex: hii husaidia kurekebisha kiwango cha homoni ya estrogen kwenye mwili na hivo kupunguza ukuaji wa uvimbe
4. Hatua ya nne. Kunywa chai tiba(herbal tea) unaweza utembelea kwenye stoo yetu ili kuweka oda: chai tiba zipo aina nyingi baadhi ya chai hizi ni Pine pollen na Kuding tea, chai hizi husaidia kubalansi homoni zako na hivo kusaidia katika kutibu uvimbe.

5.Hatua ya tano, Tumia mafuta ya castor: unapopakaaa mafuta ya castor kwenye tumbo lako husaidia kuongeza usafirrishaji wa damu na hivo kurahisisha utolewaji wa sumu haraka kwenye mwili. Watafiti wengi wa tiba wanaamini kwamba mrundikano wa sumu ndio unaopelekea kukua kwa fibroids. Jaribu pia detox package yetu ndani ya siku 30 ili kusafisha sumu kwenye mwili.

6. Hatua ya sita: Jiepushe na mzingira hatarishi yenye sumu : mazingira yenye sumu mbalimbali k**a za kuua wadudu kwenye mazao, kemikali kwenye vyakula vya viwandani kuzuia ili visiharbike, kemikali za kuua magugu, na kemikali kwenye sabuni na mafuta , vyote hivi huchangia kukua kwa uvimbe kwenye kizazi (fibroids) kwa kuharibu mpangilio wa homoni. Na mwisho kabisa

7. Hatua ya saba: Fanya mazoezi ya kutosha walau mara 3 kwa week: Mazoezi husaidia kuzuia kutokea kwa uvimbe kwenye kizazi. Mazoezi hurekebisha presha ya damu, kuimarisha kinga, na kubalansi homoni zako

Muhimu kwa Wagonjwa wa Fibroids
Kwa mwanamke mwenye uvimbe kwenye kizazi(fibroids), tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi na kurekebisha homoni zake. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 6 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake k**a vimbe, maambukizi ya bacteria, PID na kuziba kwa mirija ya uzazi.

Kwa ushauri zaidi tupigie 0785438612 au tuna ujumbe WhatsApp Kwa namba hii

Afya kwetu ni Bashasha🦋

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255785438612

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nguzo ya Wanawake posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram