Mr.Afya

Mr.Afya Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mr.Afya, Medical and health, .

VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE.Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vi...
12/11/2021

VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE.

Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus.

Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, k**a ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine k**a kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.

AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO

Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)

Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa

2. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) – Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;

Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu k**a asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
Kuwa na mawazo mengi
Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
Kunywa pombe na vinywaji vikali
Uvutaji wa sigara
Kuto kula mlo kwa mpangilio

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili k**a;

1.Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa
k**a ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula

2.Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo

3.Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa

4.Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu

5.Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu

6.Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito

7.Kushindwa kupumua vizuri

JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO

*Kunywa maji mengi

*Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo

*Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)

*Usivute sigara

*Punguza au acha kunywa pombe

*Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali

*Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9

MADHARA YA VIDONDA TUMBO

Saratan ya utumbo

Kupungua kwa kinga ya mwili

Kupungua uzito

Kupungua kuvu za kiume
Kwa Msaada Zaidi Wasiliana Nasi Kwa SIMU/UJUMBE MFUPI/WHATSAPP NAMBA 0716473449

NAMNA YA KUJILINDA NA U.T.I NA FANGASI.1. Tumia viini lishe na virutubisho i.e food supplements.2. Kunywa maji mengi ang...
22/10/2021

NAMNA YA KUJILINDA NA U.T.I NA FANGASI.

1. Tumia viini lishe na virutubisho i.e food supplements.

2. Kunywa maji mengi angalau glasi nane kwa siku.

3. Epuka matumizi ya pombe na kahawa.

4. Kunywa maji kabla ya kufanya mapenzi na kojoa baada ya kufanya mapenzi.

5. Jitawaze kuanzia mbele kwenda nyuma.

6. Kata makucha marefu kwa sababu unavyokwenda chooni kujitawaza huwa baadhi ya uchafu unabaki kwenye makucha na ndio chanzo cha wanawake wengi kuwa na U.T.I inayojirudia mara kwa mara.

7. Tumia pads zilizothibishwa na tbs ukiwa kwenye period au tumia pads za kufua

8. Epuka kujipulizia pafyumu kwenye sehemu za siri.

9. Vaa nguo za ndani za pamba na epuka nguo zinazobana sana. kupata suluhisho la tatizo hili bonyeza link hapa chini kisha bonyeza link ya kuwasiliana nasi upate nafasi ya kujiunga na kikundi chetu cha elimu

16/09/2021

Address


477

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mr.Afya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram