Infinite Kiumeni 2

  • Home
  • Infinite Kiumeni 2

Infinite Kiumeni 2 JIFUNZE.

Kumtongoza Mwanamke Unayempenda, Kumpata na Kuwa Naye Kimahusiano,

Kudumisha Mahusiano na Ndoa,

Kuongeza Nguvu za Kiume,

Kumridhisha Kitandani,

Maneno Matamu ya Kumsifia na

Kumfanya Mwanamke Akupende Zaidi,

Kumrudisha Ex Wako.

Unaendeleaje kiongozi...Kuanzia mwezi huu kutakuwa kuna mabadiliko kwenye masomo ya mahusiano na dawa ya nguvu za kiumeK...
02/12/2024

Unaendeleaje kiongozi...

Kuanzia mwezi huu kutakuwa kuna mabadiliko kwenye masomo ya mahusiano na dawa ya nguvu za kiume

Kutokana na ratiba na sababu zilizo nje ya uwezo wangu

Ila bado tupo pamoja hili chama kubwa linaendelea na tuendelee kuomba uzima.

Endelea kuwepo na ujifunze zaidi, na tuendelee kuenjoy!

Pia, Masomo yote yatakuwa kwenye huu ukurasa mpya Kuanzia sasa.
👇👇👇👇
https://www.facebook.com/profile.php?id=61568799883494

Follow hiyo page, hii haitatumika tena.

Ishara za Upungufu wa Homoni za Kiume…Homoni za kiume (testosterone) ni homoni muhimu sana kwa mwanaume.Ndiyo inayotusa...
30/11/2024

Ishara za Upungufu wa Homoni za Kiume…

Homoni za kiume (testosterone) ni homoni muhimu sana kwa mwanaume.

Ndiyo inayotusaidia tuwe na nguvu za kiume. Ikipungua utaona dalili hizi;
- Mudi (mood) zako zinabadilika hovyo.
Yaani, unakuwa unataka hichi sasahivi, baadaye unabadilisha.

Unakuwa hueleweki. K**a mudi za k**e. Na unakuwa unaendesha na hisia hisia sana.

- Upungufu wa nguvu za kiume.
Unajikuta huna hamu ya s*x. Uume hausimami asubuhi. Uume unakuwa legelege, unawahi kumwaga, n.k..

- Unakuwa na nyama uzembe.
Mafuta mafuta yanaongezeka mwilini mwako huku misuli ikifutika (haionekani tena).

Au unakuwa na mwili mkubwa lakini kilo unazo kidogo.

- Uchovu wa mara kwa mara.
Unakosa motisha mara kwa mara.

Hata kitandani unakuwa mzito. Ukipiga kimoja chali na unalala.

Kwahiyo, hakikisha unapandisha homoni zako za kiume.

Kula lishe sahihi, lishe ndiyo kitu cha kwanza katika kurekebisha homoni zako za kiume.

Utajifunza kuhusu lishe sahihi kupitia kitabu kipya cha “Lishe Sahihi”,

Kitakusaidia kuwa na nguvu za kiume maradufu na kusimamisha imara sana.

Ili kukipata bonyeza link hii
https://www.getvalue.co/prod/lishe_sahihi

Pia, uwe unachangamsha mwili kwa kujinyoosha na kutembea tembea au kufanya mazoezi.

Kila la Heri Kiongozi.

Nguvu Zaidi - Unastahili Kuenjoy S*x!

WhatsApp - 0759505947.

Sababu Kubwa ya Wanaume Kuogopa Wanawake Walioendelea…Yaani kuogopa mwanamke mwenye mali, au mwenye cheo kikubwa, au mw...
30/11/2024

Sababu Kubwa ya Wanaume Kuogopa Wanawake Walioendelea…

Yaani kuogopa mwanamke mwenye mali, au mwenye cheo kikubwa, au mwenye mzunguko mkubwa wa pesa.

Wanaume wengi ni waoga, na wanaona k**a watadharauliwa.

Au pengine walishadharauliwa walipokuwa kwenye hayo mahusiano.

Lakini ni k**a wamejitakia. Sababu hata hao wanawake wanapenda kuwa chini ya uongozi wa mwanaume, ila tatizo wanaume wengi ni dhaifu wakiwa nao.

Sasa, moja ya sababu inayopelekea hiyo hali ni…

… kubweteka. Hasa baada ya kuwa na mwanamke kwenye mahusiano.

Wengi hufikiri kwamba wakishapata mwanamke, inabidi atulie sasa, huku akiweka nguvu kiwango cha chini kwenye malengo yake.

Wakati inabidi uendelee na kasi zaidi. Na sio kifedha tu, bali kiakili na kiujasiri.

Mfano, wanaume wengi baada ya kuoa, huwa wanakaa nyumbani muda mwingi na kupumzika. Bila kujua taratibu anaingia kwenye kubweteka.

Badala ya kutoka nje, kufanya vitu alivyokuwa anapenda (hobby), kwenda sehemu za tofauti, kujifunza vitu vipya, ashindane na wanaume wenzake kwenye kitu fulani nje ya kazi/ biashara.

Vitu ambavyo vitamfanya ajiamini zaidi.

Kuwa na chachu ya kuwa mfalme, na utaona utofauti.

Hata mke wako akikuambia amepandishwa cheo amekuwa waziri mkuu, huogopi. Kwasababu unajijua wewe ndiyo mfalme wa nchi yako.

Kwahiyo, usibweteke kiongozi. Kuwa na mwanamke sio mwisho, bali ndiyo mwanzo.

Share na Rafiki Yako Ajifunze!

Je, na wewe unaogopa mwanamke aliyekuzidi kipato?

Nakusaidia;
- Kupata Mwanamke Sahihi
- Kumfanya akupende, kumteka kimapenzi na akupe penzi
- Kumtawala na kumuongoza mwanamke utakavyo
- Kupata Nguvu za kiume uweze kumridhisha

Ili Kupata Huduma WhatsApp - 0759505947.

K**a Mke Wako Amepata Mshahara Mkubwa na Uchumi Wake Unaongezeka, Fanya Hivi…Sio mshahara tu, bali inaweza kuwa mzunguk...
30/11/2024

K**a Mke Wako Amepata Mshahara Mkubwa na Uchumi Wake Unaongezeka, Fanya Hivi…

Sio mshahara tu, bali inaweza kuwa mzunguko wake wa pesa umeongezeka kwenye biashara,

Au, amepandishwa cheo na akapewa gari wakati wewe huna,

Au, amepata hadhi kubwa sana.

Mara nyingi hivyo vitu huwa vinateteresha wanaume. Lakini, kwasababu wewe unasoma hapa, utakuwa wa tofauti.

Hivyo vitu vichukulie k**a vitu vya kusaidia kuinua uchumi wa familia unayojenga.

Achana na akili za kichoyo. Mwambie mke wako pia, aache akili za kichoyo.

Achana na akili za kimasikini. Bali muwe na akili za kimaendeleo.

USIOGOPE mke wako akipata hizo nafasi. Bali ndiyo uzidishe uongozi wako.

Huo ndiyo muda wa kudhihirisha ujasiri wako. Hivyo, kuwa JASIRI kupitiliza. Zaidi ya awali.

Huku ukiwa unamsoma tabia zake za k**e.

Mpe uhuru, lakini, jione upo juu yake.

Jione wewe ni mfalme katika himaya yako, hivyo hata apande cheo kiasi gani, au awe na hela kiasi gani, bado inabidi awe chini ya mfalme.

Jione wewe ni raisi wa nchi yako. Hata awe tajiri kiasi gani, bado inabidi afuate uongozi wako, bado inabidi alipe kodi kwako.

Na sio kwamba ndiyo uanze kuwa dikteta. Ila, uwe k**a mfalme. Uwe raisi.

Ukifanya hivyo, maisha yatakuwa rahisi sana. Na utaweza kuishi naye hata k**a ana hela kiasi gani.

Kumbuka, mfalme hajipendekezi.

Share na Rafiki Yako Ajifunze!

Je, unaogopa mke wako akipanda cheo, akiongezewa mshahara, au akiwa na hela mpaka unamkataza?

Nakusaidia;
- Kupata Mwanamke Sahihi
- Kumfanya akupende, kumteka kimapenzi na akupe penzi
- Kumtawala na kumuongoza mwanamke utakavyo
- Kupata Nguvu za kiume uweze kumridhisha

Ili Kupata Huduma WhatsApp - 0759505947.

Sababu Mojawapo ya Kwanini Unaogopa Kumpoteza Mwanamke Unayempenda…Aitha umeshamuoa, au ndiyo unaanza kudate naye au ku...
30/11/2024

Sababu Mojawapo ya Kwanini Unaogopa Kumpoteza Mwanamke Unayempenda…

Aitha umeshamuoa, au ndiyo unaanza kudate naye au kumtongoza, jitahidi usiogope kumpoteza.

Kwasababu itapelekea kumpoteza.

Mara nyingi, uoga wa kumpoteza unatokana na…

… kujiona hustahili kuwa na mwanamke k**a huyo.
… kujiona huna hadhi ya kuwa na mwanamke k**a huyo.
… kujiona k**a hutoweza kumtunza na kuwa na mwanamke k**a huyo.

Yaani … hujiamini katika uwezo wako wa kuwa naye.

Kwahiyo, anza kujiaminisha kwamba unastahili kuwa na mwanamke unayempenda.

Jiaminishe unaweza kuwa naye.

Mara nyingi tatizo hili hutokana na kukosa uzoefu, lakini, kitabu cha “Shortcut ya Kumpata Mwanamke Unayempenda” kitakusaidia.

Kitakusaidia uweze kujiamini, uweze kujiona unaweza kuwa naye, uweze kumtunza na kumfanya akupende, na kitakusaidia kukupa uzoefu hivyo itakuwa rahisi.

Bonyeza link hii kukipata kitabu chako sasa
https://www.getvalue.co/prod/shortcut_ya_kumpata_mwanamke_unayempenda

Share na Rafiki Yako Ajifunze!

Je, una wasiwasi juu ya mrembo uliyenaye?

Nakusaidia;
- Kupata Mwanamke Sahihi
- Kumfanya akupende, kumteka kimapenzi na akupe penzi
- Kumtawala na kumuongoza mwanamke utakavyo
- Kupata Nguvu za kiume uweze kumridhisha

Ili Kupata Huduma WhatsApp - 0759505947.

Sababu za Kukosa Hamu ya Tendo…Unaweza kuwa na uwezo na una nguvu za kiume lakini, ukakosa hamu ya tendo.Mara nyingi hu...
29/11/2024

Sababu za Kukosa Hamu ya Tendo…

Unaweza kuwa na uwezo na una nguvu za kiume lakini, ukakosa hamu ya tendo.

Mara nyingi husababishwa na kupungua kwa homoni za kiume. Na kupelekea kukosa msukumo wa kufanya tendo.

Pia, ile hali ya kushindwa kurudia tendo, au kukosa hamu baada ya kupiga hamu husababishwa na upungufu wa homoni za kiume.

Sababu zingine zinazochangia kukosa hamu ni pamoja na;
- Migogoro ya kifamilia.
Migogoro na mke wako.
Migogoro na rafiki na jamaa zako.

- Hali ya kiuchumi.
Pamoja na madeni.

Hupelekea kuwa na stress kiasi kwamba hata homoni za kiume zinashuka.

- Kutoridhika na maisha yako.
Huna mke unayemtaka, ila upo naye basi tu. Na kwa ndani humtamani.

Hupendi kazi yako.

Na unachukia hali yako ya kimaisha kiujumla.

- Uliwahi kufeli/ kuzingua kwenye s*x.
Hivyo, ile historia bado inakuandama.

Suluhisho ni kujifunza kuhusu s*x na kusahau sehemu uliyozingua.

- Lishe mbovu.
Lishe ambayo haikusaidii kutunza afya yako pamoja na afya ya uzazi.

Uzuri ni kwamba, katika yote hayo unaweza kupata suluhisho. Usikate tamaa.

Tatua changamoto iliyopo, usikae kulalamika na usiendelee kuteseka na tatizo la kukosa hamu.

Kila la Heri Kiongozi.

Nguvu Zaidi - Unastahili Kuenjoy S*x!

WhatsApp - 0759505947.

Faida za Kumkatalia Mwanamke Baadhi ya Vitu…Yaani, sio kila kitu unamkubalia. Au unafanya vitu kulingana na matakwa yak...
29/11/2024

Faida za Kumkatalia Mwanamke Baadhi ya Vitu…

Yaani, sio kila kitu unamkubalia. Au unafanya vitu kulingana na matakwa yake.

Vitu vingine unamkatalia, vingine unamkatalia makusudi ili tu kumpa drama.

Wanawake wengi wamezoea kulelewa kimayai, na kupewa vitu au kukubaliwa karibia kila kitu, hivyo ukikataa utakuwa wa tofauti.

Miongoni mwa faida utakazopata ni;
- Mwanamke kuendelea kubaki na wewe.
Atalalamika kwamba humfanyii hichi, au humsikilizi, lakini hatokuacha.

- Upendo wake utaongezeka kwako.
Kwasababu atakuona ni wa tofauti, na sio k**a wengine.

- Ni rahisi kukuheshimu.
Kwasababu anajua inabidi awe anakuheshimu ili uwe unamkubalia vitu.

La sivyo, asipokuheshimu anajua atakataliwa.

Hizo faida zitasaidia awe anakupenda zaidi na aendelee kudumu na wewe.

Hivyo, usiwe mlaini laini kwa kufuata matakwa yote ya mwanamke.

Hata k**a ni mama yako. Sasahivi umeshakua.

Share na Rafiki Yako Ajifunze!

Je, huwa unapenda kumfurahisha kwa kumtimizia mahitaji yake yote?

Nakusaidia;
- Kupata Mwanamke Sahihi
- Kumfanya akupende, kumteka kimapenzi na akupe penzi
- Kumtawala na kumuongoza mwanamke utakavyo
- Kupata Nguvu za kiume uweze kumridhisha

Ili Kupata Huduma WhatsApp - 0759505947.

Mwanamke wa Hivi Atakurudisha Nyuma Kwenye Maendeleo Yako. Muepuke…Unapojenga maisha yako, ni vyema uangalie unajenga n...
29/11/2024

Mwanamke wa Hivi Atakurudisha Nyuma Kwenye Maendeleo Yako. Muepuke…

Unapojenga maisha yako, ni vyema uangalie unajenga na nani.

Sio kila mwanamke anastahili kuwa sehemu ya maisha yako. Hivyo, mwanamke mwenye tabia za hivi muepuke;
- Mwenye dharau.
Hata k**a anakupa utamu, na s*x yake ni nzuri, lakini akiwa na dharau hafai.

Atakufanya ujione mdogo. Hiyo itakuathiri kimawazo hata kazini kwako.

K**a anadharau watu wengine, basi tambua, ipo siku na wewe atakudharau.

- Anakuelemea kimahitaji.
Yaani unajua hali yako, naye anajua hali yako lakini bado anataka umpe mahitaji mengi. Au haridhiki kabisa.

Au, hana msaada wowote hata wa kimawazo na yupo yupo tu, mpaka unajiona k**a anakurudisha nyuma.

- Anakukosoa muda wote.
Hataki kufuata uongozi wako. Muda wote mnabishana. Hata ukimuambia kitu cha kawaida, anabisha na kukosoa.

Anakosoa mipango yako. Anakulinganisha na wanaume wengine. Huyo hafai. Atakurudisha nyuma.

- Hakupi kipaumbele.
Yaani unaona kabisa wewe sio kipaumbele chake.

Aitha hana hisia na wewe k**a zamani au hajawahi kukupenda.

K**a ni hisia zimepungua, basi tumia kitabu cha “Shortcut ya Kumpata Mwanamke Unayempenda” ili kumrudisha akupende k**a zamani.

Bonyeza link hii kukipata
https://www.getvalue.co/prod/shortcut_ya_kumpata_mwanamke_unayempenda

- Hakupi amani.
Hakufanyi ujisikie mwepesi ili uende ukafanye harakati zako kwa nguvu zaidi.

Ukiwa naye unajihisi ni mzigo mwingine. Basi huyo atakurudisha nyuma sana.

Share na Rafiki Yako Ajifunze!

Je, mwanamke wako anakuongezea Thamani? Anakusaidia katika maendeleo yako?

Nakusaidia;
- Kupata Mwanamke Sahihi
- Kumfanya akupende, kumteka kimapenzi na akupe penzi
- Kumtawala na kumuongoza mwanamke utakavyo
- Kupata Nguvu za kiume uweze kumridhisha

Ili Kupata Huduma WhatsApp - 0759505947.

Jamii Inavyoharibu Watoto wa Kiume…Kwa asilimia nyingi, jamii inachangia katika hili janga la wanaume dhaifu.Huwa inaan...
29/11/2024

Jamii Inavyoharibu Watoto wa Kiume…

Kwa asilimia nyingi, jamii inachangia katika hili janga la wanaume dhaifu.

Huwa inaanzia tangia tukiwa wadogo.

Wanaume tumeumbwa kujenga, kujaribu vitu vipya, kutoka na kwenda kuteka sehemu mpya, na kufanya mambo ambayo ni hatari kwa kiasi fulani.

Lakini, sikuhizi watoto wa kiume wanawekwa ndani tu na wazazi, wakionekana nje, jamii inasema anazurura tu.

Ni kweli asizurure, lakini atembee kwa malengo, na sio kukaa ndani tu muda wote. Hicho ni kipengele cha wanawake.

Mtoto wa kiume achakarike kutafuta pesa, hata k**a ni kidogo ila inamjenga. Kuliko kukaa ndani kusubiri wazazi/ walezi walete au kusubiri amalize shule/ chuo.

Pia, jamii imekuwa ikimpa attention mwanaume ambaye ni dhaifu kwa kubadilisha mawazo yake au ni mnyenyekevu kupitiliza.

Utaona anasifiwa sana. Na wavulana wataiga hiyo tabia wakiamini ndiyo kinachotakiwa.

Wanasifiwa lakini sifa zinaishia juu juu. Huku mwanaume jasiri na asiyeendeshwa ndiye anafaidi mema ya nchi.

Au, unakuta mvulana anaiga yale ya kwenye muvi ambazo jamii nzima inaangalia.

Akiona ni jamii nzima inaangalia hizo muvi, naye anaamini kwamba hicho ndiyo kitu sahihi cha kufanya. Kumbe anajichimbia shimo la maumivu.

Muvi zinapotosha sehemu nyingi, hasa kwenye kipengele cha jinsi ya kuishi na mwanamke.

Lakini, kwasababu zimefanywa ni kitu cha kawaida, basi inaonekana ndiyo njia pekee.

K**a una mtoto wa kiume, nenda naye hata kazini kwako kipindi hayupo shule. Usimuache akae tu nyumbani.

Utamsaidia kufungua akili yake.

Usikubali jamii ikuambie “mtoto wako ametulia” huku yupo ndani tu na hajafunguka kiakili ya utafutaji, hizo sifa hazina maana.

Share na Rafiki Yako Ajifunze!

Je, unamchangamsha mtoto wako wa kiume? Au unamuweka ndani tu?

Nakusaidia;
- Kupata Mwanamke Sahihi
- Kumfanya akupende, kumteka kimapenzi na akupe penzi
- Kumtawala na kumuongoza mwanamke utakavyo
- Kupata Nguvu za kiume uweze kumridhisha

Ili Kupata Huduma WhatsApp - 0759505947.

Mtindo wa Maisha Unavyosababisha Tatizo la Nguvu za Kiume…Mtindo wa maisha (lifestyle) ni moja ya kichocheo kikubwa cha...
28/11/2024

Mtindo wa Maisha Unavyosababisha Tatizo la Nguvu za Kiume…

Mtindo wa maisha (lifestyle) ni moja ya kichocheo kikubwa cha tatizo la nguvu za kiume ukiachana na sababu za kiafya.

Mtindo wa maisha pia, unaathiri afya ya mtu kiujumla ikiwemo afya ya uzazi na nguvu za kiume.

Mtindo wa maisha ni jinsi unavyoendesha maisha yako kuanzia asubuhi unapoamka mpaka jioni unapolala.

Kwahiyo, sio ngumu k**a ukiichukulia kwa siku na sio kuangalia kwa mwezi.

Yaani, unatengeneza ratiba nzuri kwa siku na sio kwa mwezi maana itakuwekea presha kubwa mpaka ushindwe kufuata.

Mtindo wa maisha unaoleta tatizo la nguvu za kiume ni;
- Kubweteka muda mwingi.
- Kutokula lishe sahihi, kula vyakula vinavyoshusha nguvu za kiume.
- Kuendelea na uraibu unaokusumbua, k**a vile kujichua, au video za X.

Hivyobasi, ili kutatua changamoto inayokusumbua, anza kuangalia hivyo vipengele.

Na k**a unajiuliza chakula gani kitakusaidia, basi hiki kitabu cha “Lishe Sahihi” kitakusaidia kurekebisha mtindo wa maisha kwenye upande wa msosi ili ukupatie nguvu za kiume.

Bonyeza link hii ili kupata kitabu chako cha “Lishe Sahihi”
https://www.getvalue.co/prod/lishe_sahihi

Kila la Heri Kiongozi.

Nguvu Zaidi - Unastahili Kuenjoy S*x!

WhatsApp - 0759505947.

Usiangalie Marafiki Zake wa Kiume Tu, Bali Hata wa K**e K**a Hivi…Mara nyingi huwa tunasema usimruhusu mke wako awe na ...
28/11/2024

Usiangalie Marafiki Zake wa Kiume Tu, Bali Hata wa K**e K**a Hivi…

Mara nyingi huwa tunasema usimruhusu mke wako awe na marafiki wa kiume, au usiwe na mwanamke mwenye marafiki wengi wa kiume,

Lakini, ni vyema kuchunguza na marafiki zake wa k**e.

Marafiki zake wa k**e wana mchango mkubwa mahusiano yenu yaweje kwasababu wanawake wanajali sana maoni ya marafiki zao wa k**e.

Hivyo, ukiona ana marafiki wasio eleweka, basi tambua utapambana na drama zisizo na msingi.

Mfano, k**a ana marafiki ambao ni single mother, basi tegemea ushauri wao utakuwa wa kisingle mother,

Hata k**a wanachakarika na wana pesa, lakini hawatokuwa na ushauri wa amani ndani ya nyumba.

Hata Harmonize amesema, “bora ugali dagaa kwenye amani kuliko wali nyama vitani”.

Bora mwanamke asiye na hela ila kuna amani kuliko mwanamke mwenye hela ila kuna vita.

Vilevile, k**a marafiki zake ni wamama wenye ndoa zao muda mrefu na wametunza watoto wao huku wakiwa na waume zao,

Basi tarajia hata ninyi mtadumu.

Kwasababu, watu wanaompa ushauri wanajua jinsi ya kudumu na mwanaume na sio kutanga tanga.

Kwahiyo, usiishie kuangalia kuhusu marafiki wa kiume, pia angalia kuhusu rafiki zake wa k**e.

Rafiki zake wa k**e ni k**a utabiri wa mtafika wapi.

Share na Rafiki Yako Ajifunze!

Je, huwa unaangalia marafiki zake wa k**e?

Nakusaidia;
- Kupata Mwanamke Sahihi
- Kumfanya akupende, kumteka kimapenzi na akupe penzi
- Kumtawala na kumuongoza mwanamke utakavyo
- Kupata Nguvu za kiume uweze kumridhisha

Ili Kupata Huduma WhatsApp - 0759505947.

Mwanamke Unayempenda Akikuacha Fanya Hivi…Hii inauma sana, maana unakuwa ulishaweka mipango juu yake, na umeona atakufa...
28/11/2024

Mwanamke Unayempenda Akikuacha Fanya Hivi…

Hii inauma sana, maana unakuwa ulishaweka mipango juu yake, na umeona atakufaa maishani.

Pengine unajua hakufai maishani, ila alikuwa anakufanya ujisikie raha na s*x ilikuwa tamu sana,

Na sasahivi amekuacha. Hatua nzuri za kuchukua ni hizi;
- Usimlilie abaki.
Usimng’ang’anie. Yeye ni mtu mzima na anajielewa anapofanya maamuzi yake.

Mwache aende. Ukimlazimisha abaki ataendelea kukusaliti ndani kwako.

- Relax.
Tafuta njia nyingine za kujipooza kwa muda. Lakini sio vilevi, punyeto au video za X.

Ungana na familia yako. Hautakuwa na furaha, lakini kaa nao wanatakupa faraja.

Ungana na marafiki zako, watakupa faraja.

- Fanya kitu.
Fanya kitu cha kukuweka bize. Fanya kitu cha kukuondoa mawazo yako. Fanya kitu na usikae tu. La sivyo mawazo na maumivu yatakusumbua sana.

Fanya kitu ulichokuwa unatamani kufanya. Ione k**a nafasi yako ya kufanya hivyo.

- Weka nguvu kwenye malengo.
Yeye kukuacha ni k**a baraka kwako.

Kwasababu utapata muda zaidi wa kuweka nguvu kwenye malengo yako.

Yale maumivu na hasira za kuachwa/ kusalitiwa yaweke kwenye kufanya malengo yako.

- Jifunze juu ya mahusiano.
Hata ukitimiza malengo yako, ukawa na pesa, lakini k**a hujifunzi juu ya mahusiano utaishia kwenye maumivu yaleyale.

Mpaka utajiona unakata tamaa ya mahusiano.

Na kikubwa ni kwamba … usichukie wanawake woote kwasababu ya maumivu uliyopitia.

Bali jifunze jinsi ya kuishi nao.

Share na Rafiki Yako Ajifunze!

Je, maumivu ya kuachwa bado yanakutesa?

Nakusaidia;
- Kupata Mwanamke Sahihi
- Kumfanya akupende, awe na hisia na wewe na akupe penzi
- Kumtawala na kumuongoza mwanamke utakavyo
- Kupata Nguvu za kiume uweze kumridhisha

Ili Kupata Huduma WhatsApp - 0759505947.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Infinite Kiumeni 2 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Infinite Kiumeni 2:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Practice
  • Claim ownership or report listing
  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share