
15/04/2025
*SI KILA MEZA UNATAKIWA KUKAA.*
_Kuna meza unakaa, wanakudharau._
_Kuna meza unakaa, wanakutumia tu._
Kuna meza unakaa, unajikuta wewe ndo unatafuta “approval” kila dakika.
Hey, meza zingine si zako na si vibaya kuondoka.
SI KILA MEZA UNATAKIWA KUKAA.
Kuna meza unakaa, wanakudharau.
Kuna meza unakaa, wanakutumia tu.
Kuna meza unakaa, unajikuta wewe ndo unatafuta “approval” kila dakika
Hey, meza zingine si zako na si vibaya kuondoka.
Watu wengi wanajikuta wamejaa rohoni, lakini wamefilisika kiuzoefu. Wanatolewa roho polepole kwenye *“Friendship” na mahusiano ya kuonewa. Na bado wanakaa tu, kwa sababu hawataki kuonekana “Wamefail.”
Lakini hebu jiulize K**a meza haina heshima, haina nafasi ya ndoto zako, na inakula utu wako ni kweli bado unataka uketi hapo?
Sio kila rejection ni hasara.Wengine wakikuacha, ni Mungu anakutenganisha na vitu visivyo "match frequency yako.
Ukiendelea kung'ang'ania penzi linalokuumiza,
Utaacha kulipenda jambo linalokuponya.
Ukiendelea kupambana kuwa karibu na watu wanaokuchoma, Utawatenga wale wanaotaka kukujenga.
Usiogope kuondoka meza isiyo yako. Labda kuna meza bora imeandaliwa Kwa ajili Yako, Ila huwezi kuiona k**a ukiendelea kukaa chini ya miguu ya watu.
Jitambue kabla haujatumiwa.