26/06/2021
*MAGONJWA YA MOYO – AINA, CHANZO, DALILI, TIBA*
Magonjwa ya Moyo ni magonjwa yanayoambatana na kuathiri moyo. Mara nyingi magonjwa ya moyo yanaambatana na mishipa ya damu kuwa na tatizo ambapo moyo hushindwa kufanya kazi, moyo hutegemea damu ambayo hubeba oxygen, madini, vitamins, kinga ya mwili, joto, homoni na vingine vingi.
Kwa mwaka 2015 pekee zaidi ya watu milioni 17.7 walifariki kutokana na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu. Hii ni sawa na theluthi ya vifo vyote duniani. Zaidi ya theluthi ya vifo vyote vinavyotokana na ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu hutokea ndani ya nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati
*Aina Za Magonjwa Ya Moyo*
Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya moyo ambayo hutofautiana, japo yote huathiri moyo, nayo ni;
1. *Ugonjwa wa moyo unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu (Coronary artery disease)*
Hili ni tatizo linalowakuta watu wengi, mishipa ya damu hupasuka na kuharibika.
Hali hii hutokana na mishipa ya damu kuwa na uchafu na mafuta mengi na kufanya damu isipite vizuri
2. *Mapigo ya moyo kwenda tofauti (Heart Arrhythmias)*
Hii hutokea pale mapigo ya moyo kwenda taratibu isivyo kawaida au kwenda haraka isivyo kawaida, pia mapigo ya moyo kwenda ovyo. Hii ni hatari sana na huua sana
3. *Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure)*
Hii ni hali ya moyo kushindwa kufanya kazi yake k**a kupampu na kusambaza damu, kusambaza oxygen.
Hii inaweza kutokea kwa mtu mwenye magonjwa k**a ugonjwa wa moyo wa mishipa kuathirika, Shinikizo la damu, na magonjwa mengine.
4. *Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital heart disease)*
Haya ni magonjwa ambayo wengi huzaliwa nayo, yanaweza kuwa ni baadhi ya kasoro katika mwili k**a baadhi ya chemba za moyo kuziba au kupasuka, oxygen kupita kwa shida na vinginevyo.
5. *Ugonjwa wa valvu na misuli ya moyo (Heart Valve Disease & Cardiomyopathy (Heart Muscle Disease))*
Katika moyo kuna chemba nne nazo zinapitisha damu na oxygen kutoka kwenye mapafu, valvu hufunguka na kufunga. Valvu na misuli ikiwa imepasuka na kuharibika husababisha tatizo la moyo.
6. *Moyo kutanuka*
Hii hutokea pale damu ikiingia ndani ya moyo harafu mishipa ya kutoa damu ikiwa na tatizo ikashindwa kutoa damu nje ya moyo moyo utaanza kutanuka siku hadi siku. Kutanuka kwa moyo kunatokea usipotibu baadhi ya matatizo k**a shinikizo la damu, moyo kwenda mbio, valvu na misuli ya moyo n.k.
7. *Shinikizo la damu (B.P)*
Hili ni shinikizo la damu yako kwenye kuta za mishipa yako kwani moyo wako unasukuma damu karibu na mwili wako.
Unaweza kuwa na shinikizo la damu (shinikizo la damu) kwa miaka bila dalili yoyote.
8. *Mshtuko/ Shambulio la moyo (Heart Attack)*
Ni kifo cha sehemu ya misuli ya moyo inayosababishwa na kuzuiwa kwa usambazaji wa damu. Amana zilizo na mafuta huunda kwa wakati, na kutengeneza alama katika mishipa ya moyo wako.
Ikiwa baadhi ya misuli ya moyo inakufa, mtu hupata maumivu ya kifua na kukosekana kwa umeme kwa tishu za misuli ya moyo.
9. *Chembe ya Moyo*
Hii ni maumivu ya upande wa moyo maeneo ya kifua ambayo hutokea wakati unafanya kazi au hata k**a umekaa k**a ni yenye kukubuhu.
Maumivu haya huambatana na kutokwa jasho na kukosa hewa. Hutokana na moyo kukosa damu ya kutosha.
*Chanzo Cha Magonjwa Ya Moyo*
Magonjwa ya moyo hutokea pale ambapo moyo huathiriwa na kuharibiwa kwa vitendea kazi vyake.
Kuna mitindo mbalimbali ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata magonjwa ya moyo,nayo ni pamoja na;
✍🏻Kuwa na halemu (Cholesterol)
✍🏻 Shinikizo la damu (B.P)
✍🏻Kuvuta sigala
✍🏻Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
✍🏻Kisukari
✍🏻Kukaa sehemu kwa mda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili
✍🏻Umri
✍🏻Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
✍🏻Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
✍🏻Historia magonjwa yanayoambatana na moyo katika familia
*Dalili za Ugonjwa Wa Moyo*
Mara nyingi dalili hujionesha wakati mtu kakaa na ugonjwa kwa mda mrefu kidogo, ila kuna zingine zinatangulia na mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia. Uonapo baadhi ya dalili fanya mawasiliano haraka usaidiwe
✍🏻Moyo kwenda mbio (Moyo kudunda kwa nguvu isivyo kawaida )
✍🏻Uchovu uliopitiliza, mwili kuwa dhaifu na kuchoka haraka hata kwenye shughuri ndogo
✍🏻Maumivu ya kifua hasa yanayotembea mpaka kwenye mabega, shingo au taya
✍🏻Kushindwa kulala vizuri hasa kushtuka usingizini kuhisi k**a unakabwa na kukosa pumzi
✍🏻Tumbo kujaa, kichefuchefu na kutapika
✍🏻Kukosa pumzi au kushindwa kupumua vizuri hasa unapolala
✍🏻Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji
*Hatua za kuchukua ili Kujikinga dhidi ya Magonjwa ya Moyo*
✍🏻Fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku
✍🏻Usile vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
✍🏻Usitumie chumvi mbichi au chumvi nyingi
✍🏻Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)
✍🏻Balansi uzito wako
✍🏻Usivute sigara
✍🏻Punguza au acha kunywa pombe
✍🏻Punguza mawazo
✍🏻Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
✍🏻Lala vizuri kwa muda mzuri angalau masaa 7 hadi 9
*Tiba Ya Magonjwa Ya Moyo*
Magonjwa ya moyo yanatibika kwa hali tofauti, pia kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakikata tamaa na kuwa wabishi, hii hufanya wengi kufa kutokana na kuto kuwa makini na kile tunacho waeleza.
Tuna matibabu ya kutibu kabisa magonjwa ya moyo ambayo ni ya asili yasiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa.
Matibabu hayo hutibu kulingana na mda wa tatizo husika.
Tunamshukru Mungu kwa uumbaji wake na kutupa dawa ambazo alizileta ili kutuimarisha na kutuponya, Mungu hakuumba dawa nyingine zaidi ya mimea na vitu vingine vya asili, japo wengi hudharau.
*Kumbuka tiba ya kwanza ni Uamzi wako ambao ndio kupona kwako*
Kwa ushauri na matibabu wasiliana nasi kupitia 0789047530