Dr. J. Mkelo

Dr. J. Mkelo health is my priority Always at your service

**TANGAZO MAALUM!****ETERNAL HEALTH CARE** inakuletea ofa kabambe ya **FULL BODY CHECK-UP** kwa bei ya punguzo ya **Shil...
09/09/2024

**TANGAZO MAALUM!**

**ETERNAL HEALTH CARE** inakuletea ofa kabambe ya **FULL BODY CHECK-UP** kwa bei ya punguzo ya **Shilingi 15,000 tu!**

Pata huduma za vipimo vyote muhimu vya afya yako, ukiwemo:
✔️ Upimaji wa shinikizo la damu
✔️ Vipimo vya sukari
✔️ Ukaguzi wa moyo
✔️ Vipimo vya uzito na urefu
✔️ Upimaji wa viwango vya cholesterol
✔️ Na vipimo vingine vingi!
✔️ Vipimo vya mfumo wa uzazi
✔️ Ushauri na saa na Daktari
Afya yako ni kipaumbele chetu, hivyo basi tunakukaribisha kuchukua hatua muhimu kwa afya bora kwa gharama nafuu kabisa.

⏰ **Muda wa Ofa:** kuanzia tareh 10/9/2024 adii 24/9/2034
📍 **Mahali:** ETERNAL HEALTH CARE, DAR ES SALAAM ( MBEZI JUU )
📞 **Wasiliana nasi:** Piga simu 0678652187
Kwa maelezo zaidi au kufanya booking.

Afya ni utajiri, chukua hatua leo!

https://wa.me/message/ZGWAEFQCBP2JK1

PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni ugonjwa wa maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke. Unasababishwa na bakter...
03/08/2024

PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni ugonjwa wa maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke. Unasababishwa na bakteria wanaoweza kuenea kutoka kwenye uke na kuingia kwenye mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi, au maeneo mengine ya karibu. Hapa kuna bangalore la PID:

# # # **1. Chanzo cha PID**

- **Maambukizi ya Kijinsia:** PID mara nyingi husababishwa na maambukizi ya kijinsia k**a vile Chlamydia na Gonorrhea. Bakteria hawa wanaweza kuingia kwenye mfumo wa uzazi kupitia njia ya uke.
- **Kuingiza Vitu Ukeni:** Uwekaji wa vifaa k**a vile IUD (intrauterine device) bila usafi wa kutosha au matumizi mabaya ya vyombo vya k**e inaweza kuongeza hatari ya PID.
- **Matibabu au Taratibu za Upasuaji:** Upasuaji wa uzazi au taratibu za upasuaji katika eneo la uzazi zinaweza kusababisha PID ikiwa bakteria wataingia katika mfumo wa uzazi.
- **Ujauzito:** Baadhi ya wanawake wanaweza kupata PID wakati wa ujauzito kutokana na mabadiliko ya mfumo wa kinga.

# # # **2. Sababu za PID**

- **Bakteria:** Maambukizi ya bakteria k**a vile Chlamydia trachomatis na Neisseria gonorrhoeae ndiyo sababu kuu za PID.
- **Maambukizi Mengine:** Maambukizi ya bakteria mengine, ikiwa ni pamoja na Escherichia coli na Mycoplasma genitalium, yanaweza pia kusababisha PID.
- **Usafi Duni:** Kutumia vifaa visivyo safi au kutokutunza usafi wa maeneo ya siri kunaweza kuchangia PID.
- **Historia ya PID:** Kuwa na historia ya PID inaongeza hatari ya kupata tena maambukizi haya.

# # # **3. Madhara ya PID**

- **Utasa:** PID inaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa viungo vya uzazi, ikiwa ni pamoja na kuzuia mirija ya uzazi, hivyo kuzuia yai kukutana na mbegu za kiume na kusababisha utasa.
- **Mimba ya Mifuko ya Maziwa:** Kuwa na PID kunaongeza hatari ya kupata mimba inayotunga nje ya mji wa mimba (ectopic pregnancy), ambayo ni hali hatari inayohitaji matibabu ya haraka.
- **Maumivu ya Kudumu ya Tumbo:** Uharibifu wa viungo vya uzazi unaweza kusababisha maumivu ya kudumu ya tumbo, ambayo yanaweza kuwa makali au kuja na kuondoka.
- **Abscesses:** Mabonge yenye usaha yanaweza kutokea kwenye mirija ya uzazi au katika maeneo ya karibu, na kuhitaji matibabu ya haraka.

# # # **4. Hitimisho**

PID ni ugonjwa unaoweza kusababisha madhara makubwa ikiwa hautatibiwa mapema. Ni muhimu kwa wanawake kuepuka tabia hatarishi k**a vile kujamiiana bila kinga na kutunza usafi wa kibinafsi ili kupunguza hatari ya maambukizi. Pia, ni muhimu kwenda hospitali mara moja ikiwa kuna dalili za PID ili kupata matibabu sahihi.

(Oral Candida Infection) kwa watoto Maambukizi ya fungus za kinywa kwa mtotoDalili kuu ni mabaka (utandu)ya weupe weupe ...
12/12/2023

(Oral Candida Infection) kwa watoto

Maambukizi ya fungus za kinywa kwa mtoto
Dalili kuu ni mabaka (utandu)ya weupe weupe au rangi ya maziwa kwenye mdomo na ulimi.

Mabaka haya huletwa na fungus aina ya candida.
Candida ni aina ya fungus ambayo hupatikana kwenye ngozi na mdomoni lakini k**a watazidi kwa kiasi kikubwa huwa ni tatizo
K**a mtoto ana afya na kinga ya kutosha hili si tatizo kwake

Kundi lipi la watoto wapo kwenye hatari ya kupata fungus wa kinywa?

👉🏼watoto wanao tumia antibiotics kwa wingi
👉🏼watoto wanaotumia corticosteroids haswa wenye asthma
👉🏼watoto wenye upungufu wa kinga za mwili
👉🏼watoto wenye uzito mdogo
👉🏼mtoto aliezaliwa na mama mwenye maambukizi ya fungus ukeni

Dalili kuu ni mtoto kulia lia sababu ya maumivu,kukosa hamu ya kula,kuvimba au kuwa na sehemu nyekundu baada ya kutoa ule utando mweupe

Ni muhimu mama mjamzito ujitibie k**a una infection yoyote kabla ya kujifungua
Mtoto pia ni muhimu apate tiba,
Mtoto mwenye uzito mdogo pia muhimu aangaliwe maana yupo kwenye risk pia ya kupata oral thrush
Kuna virutubisho vya watoto multivatimins na Omega vina faida zaidi ya 20 mwilini husaidia sana kukinga watoto na magonjwa ya mara kwa mara,mtoto mwenye shida ya kula uzito mdogo pia vinamsaidia
Kupata maelezo zaidi wasiliana nasi call 0678652187

29/09/2023

Ni kweli bia tamu lakini lini mara ya mwisho kufanya detox?
Swipe left kuona hatua za ini kufeli

Ini Ndio chujio la kwanza la mwili kila kitu unachokula Au kunywa lazima kupite kwenye ini kwanza Ndio kiingizwe mwilini

Baadhi ya vyakula na vinywaji vina athari ya muda mrefu ikiwa vitatumiwa kwa muda mrefu
Watu wengi wanywaji wa pombe ukisikia ana shida ya ini mara nyingi ni seli za ini zinabadilika na kuvimba(liver cirrhosis)

KAZI YA INI MWILINI

INI: Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. Ni kiungo ambacho kinahitaji kulindwa na kukingwa pamoja na kusafishwa mara kwa mara.

KAZI YA INI MWILINI
1. Ini lina kazi ya uchujaji wa sumu, inachuja sumu kwenye damu ambayo huingia kwa njia ya vyakula, vinywaji (bila kusahau vinywaji vikali), hewa tunayovuta, sigara, pamoja na dawa tunazotumia.

2. Vile vile, hutoa nyongo ambayo kazi yake kubwa ni kusaga mafuta na protini kutoka kwenye chakula tulacho.

3. Pia, ini hukibadilisha chakula na kufanya tupate nguvu mwilini.
Hivyo basi, tunahitaji kulilinda ini ili liweze kufanya kazi yake ya uondaji wa sumu na kusaga mafuta na protini k**a ilivyokusudiwa.

Mara nyingi imeonekana kwa mtu mwenye shida ya ini kuwa akijisikia uchovu mara kwa mara hata k**a hajafanya kazi za kuchosha.

Hii tutokea kwa kuwa ini limezidiwa na haliwezi kufanya kazi yake ya kuhakikisha mwili unapata nguvu.�

Kwa maelezo zaidi tupigie 0678652187

*JINSI YA KUHESABU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA KUFAHAMU SIKU SALAMA NA ZILE ZA HATARI UNAZOWEZA KUSHIKA MIMBA*Njia rahisi ...
13/09/2023

*JINSI YA KUHESABU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA KUFAHAMU SIKU SALAMA NA ZILE ZA HATARI UNAZOWEZA KUSHIKA MIMBA*

Njia rahisi ya kushika.. Jua kwamba Mzunguko wa Hedhi huwa tunaugawa kwenye makumi MATATU MAKUU

*1. KUMI LA KWANZA*
Ile siku ya kwanza kuona Hedhi ndani ya mwezi iwekee alama na ihesabu k**a MOJA
Mfano k**a siku zako mwezi huu umeanza kuziona tarehe 3 basi hii tarehe unaihesabu k**a MOJA... K**a umeziona tarehe 20 basi tarehe ishirini unaihesabu k**a MOJA

*Endelea kuhesabu mpaka ufike 10.. Hizi ndizo siku salama ambazo huwezi shika ijauzito.*
Tukiendelea na mfano wetu, tulisema tarehe 20 tunaihesabu k**a moja, hivyo tarehe 21 itakua mbili, tarehe 22 itakua 3, usiache kuhesabu hata period ikikata endelea tu hivyo basi tarehe 29 itakua ndio siku ya kumi. Kwa maana nyi gi e tarehe 29 ndio Mwisho wa siku salama. Ndio maana watu wakifanya mapenz siku zao za hedhi hawashiki mimba sababu zipo ndani ya siku salama kabisa..
*HIVYO BASI KUMI LA KWANZA NI LA SIKU SALAMA NA SIKU ZA HEDHI HUANGUKIA HUMU,* k**a wewe hedhi yako huwa unaenda siku nyingi basi kwenye kumi hili utakua na siku chache za kukutana na mpenz wako. *MFANO* wewe unaenda hedhi siku saba, utabakiwa na siku tatu za kukutana na mpenz wako kwenye kumi hili.. Anayekwebda siku tatu anakua na siku saba za kujidai. *Jambo la kuzingatia hii siku ya kumi k**a sio lazima iache au ishia mchana maana ni mpakani mwa kumi salama na lile la uzazi*

Tuendelee....

*2. KUMI LA PILI (KUMI LA HATARI/ KUMI LA UJAUZITO*
Hapa tunaendelea kuhesabu kuanzia pale tulipoishia ambapo tuliishia siku ya kumi amvayo iliangukia tarehe 29, hivyo hapa tunaendelea kumi na moja itayoangukia tarehe 31, kumi na mbili itaangukia tarehe 1, kumi na tatu itaangukia tarehe 2, endelea mpaka siku ya 18 ambayo itaangukia tarehe 6. Mpaka hapa hizi ni siku za hatari au Ujauzito (kwa wale mnaotaka watoto hili ndio kumi muhimu sana kwenu hasa hizo siku za kati yani 13 na 14)

*3. KUMI LA TATU NA LA MWISHO _ KUMI SALAMA LA KUJIDAI*
Kuanzia siku ya 19 mpaka pale utapoona tena siku zako haap hata Mr amwage ndoo upo salama.

Ukiona tena siku zako mzunguko unaanza moja.. Hivyo kujua una mzunguko wa siku ngapi angali mpaka ila siku unayoona tena siku zako uliishia namba ngapi kuhesabu? Wengi wana mzunguko wa siku 28 huu ndio mfupi hivyo ukiwa chini ya hapa ni tatizo.. Na wnegine wana mzunguko wa siku hadi 32 au 35.

Wenye mzunguko wa siku 28 ni kawaida kuingia Hedhi mara mbili ndani ya mwezi... *mfano* K**a umeingia mwezini tarehe moha ya mwezi january inamaana kufikia tarehe 28 utakua umemaliza mzunguko tarehe 29 utegemee kuingia tena.

*KUMBUKA NJIA HII NI SALAMA KABISA NA HAITAKUHARIBU MFUMO WA HOMONI*
Kwa maswali wasiliana nasi 0678652187

*KWA WOTE AMBAO WANA UMRI KATI YA MIAKA 40-90, HAYA HAPA MAPENDEKEZO RAHISI NA YENYE UMUHIMU KWAKO.***ANGALIA DAIMA:*1. ...
08/09/2023

*KWA WOTE AMBAO WANA UMRI KATI YA MIAKA 40-90, HAYA HAPA MAPENDEKEZO RAHISI NA YENYE UMUHIMU KWAKO.*

**ANGALIA DAIMA:*
1. Shinikizo la damu yako
2. Sukari ya damu yako
3. Triglycerides zako (aina ya mafuta yaliyomo mwilini)
4. Cholesterol yako (aina ya mafuta yaitwayo lehemu)

*PUNGUZA:*
1. Chumvi
2. Sukari
3. Unga uliokobolewa
4. Bidhaa zitokanazo na maziwa
5. Bidhaa zilizosindikwa

*CHAKULA KINACHOHITAJIKA:*
1. Mboga
2. Kunde
3. Maharage
4. Karanga
5. Mayai
6. Mafuta yaliyokamuliwa katika hali ya baridi (mzeituni, nazi,…)
7. Matunda

*MAMBO MATATU UNAYOPASWA KUJARIBU KUSAHAU:*
1. Umri wako
2. Mambo yaliyopita
3. Malalamiko/manung’uniko yako

*MAMBO MATATU MUHIMU UNAYOHITAJI KUYATHAMINI:*
1. Familia yako
2. Marafiki zako
3. Mawazo yako Chanya
4. Nyumba safi na yenye kukaribisha/kukuvutia .

*MAMBO MATATU YA MSINGI UNAYOHITAJI KUYAKUBALI:*
1. Daima tabasamu/cheka
2. Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara kwa kasi yako mwenyewe
3. Pima na kuudhibiti uzito wako

*MITINDO SITA MUHIMU YA MAISHA UNAYOHITAJI KUIFANYIA MAZOEZI:*
1. Usingoje hadi uwe na kiu ndipo unywe maji.
2. Usingoje hadi uwe mchovu ndipo upumzike.
3. Usingoje hadi uwe mgonjwa ndipo ufanye uchunguzi wa kimatibabu.
4. Usingojee miujiza ili umtumaini Mungu.
5. Usipoteze kamwe kujiamini kwako.
6. Kaa na mtazamo Chanya kila wakati na uwe na tumaini la kesho lilo bora zaidi…

*IKIWA UPO KATIKA UMRI HUU (MIAKA 40-90), TAFADHALI CHUKUA TAHADHARI.

04/09/2023

𝗭𝗢𝗘𝗭𝗜 𝗟𝗔 𝗨𝗖𝗛𝗨𝗡𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗞𝗜𝗔𝗙𝗬𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗪𝗔𝗧𝗨 𝗪𝗢𝗧𝗘.

*WHATSAPP +225 678 652 187
*

𝗨𝗻𝗮𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘆𝗼𝘆𝗼𝘁𝗲 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝗮𝗳𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗮𝘆𝗼𝗸𝘂𝘀𝘂𝗺𝗯𝘂𝗮, 𝗮𝘂 𝗶𝗻𝗮𝘆𝗼𝗸𝘂𝗸𝗮𝗯𝗶𝗹𝗶 𝗮𝘂 𝗸𝘂𝗸𝘂𝗸𝗼𝘀𝗲𝘀𝗵𝗮 𝘂𝘀𝗶𝗻𝗴𝗶𝘇𝗶 𝗮𝘂 𝗸𝘂𝗸𝘂𝗽𝗮 𝗺𝗮𝘄𝗮𝘇𝗼?

𝗨𝗺𝗲𝘄𝗮𝗵𝗶 𝗸𝘂𝗳𝗮𝗻𝘆𝗮 𝘂𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗸𝗶𝗻𝗮 𝘄𝗮 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗹𝗮𝗸𝗼?

𝗞𝘄𝗮 𝘀𝗮𝘀𝗮 𝘁𝗮𝗮𝘀𝗶𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗘𝘁𝗲𝗿𝗻𝗮𝗹 𝗶𝗻𝘁𝗲𝗿𝗻𝗮𝘁𝗶𝗼𝗻𝗮𝗹 𝗵𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵𝗰𝗮𝗿𝗲 𝗶𝗻𝗮𝘆𝗼𝗷𝗶𝗵𝘂𝘀𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗻𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝘂𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗴'𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗶𝗺𝗲𝗮𝗻𝘇𝗮 𝘇𝗼𝗲𝘇𝗶 𝗹𝗮 𝘂𝘁𝗼𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝘃𝗶𝗽𝗶𝗺𝗼 𝗸𝘄𝗮 𝗴𝗵𝗮𝗿𝗮𝗺𝗮 𝗻𝗮𝗳𝘂𝘂 𝘀𝗮𝗻𝗮.

𝗨𝘁𝗮𝗳𝗮𝗻𝘆𝗶𝘄𝗮 𝘂𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝘃𝗶𝗽𝗶𝗺𝗼 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝗮𝗲𝗻𝗲𝗼 𝗵𝗮𝘆𝗮;
•𝗠𝗳𝘂𝗺𝗼 𝘄𝗮 𝗱𝗮𝗺𝘂/𝗺𝗶𝘀𝗵𝗶𝗽𝗮 𝘆𝗮 𝗱𝗮𝗺𝘂(𝗠𝗼𝘆𝗼 𝗻𝗮 𝘂𝗯𝗼𝗻𝗴𝗼)
•𝗠𝗶𝗳𝘂𝗽𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗿𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗠𝗶𝗳𝘂𝗽𝗮
•𝗠𝗳𝘂𝗺𝗼 𝘄𝗮 𝘂𝘆𝗲𝘆𝘂𝘀𝗵𝗮𝗷𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗺𝗲𝗻𝗴'𝗲𝗻𝘆𝗼 𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮
•𝗔𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝘂𝘇𝗮𝘇𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝗸𝗶𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗺𝗮
•𝗔𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗡𝗴𝗼𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗿𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗡𝗴𝗼𝘇𝗶
•𝗠𝗳𝘂𝗺𝗼 𝘄𝗮 𝗳𝗮𝗵𝗮𝗺𝘂
•𝗝𝗶𝗰𝗵𝗼 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗿𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗰𝗵𝗼
•𝗔𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝘂𝘇𝗮𝘇𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝗸𝗶𝗻𝗮𝗯𝗮𝗯𝗮
•𝗠𝗳𝘂𝗺𝗼 𝘄𝗮 𝘂𝗽𝘂𝗺𝘂𝗮𝗷𝗶.

𝗭𝗮𝗶𝗱𝗶 𝘆𝗮 𝘄𝗮𝘁𝘂 200 𝗺𝗽𝗮𝗸𝗮 𝘀𝗮𝘀𝗮 𝘄𝗮𝗺𝗲𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝗵𝗶𝗶 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗮𝘁𝗶𝘄𝗮 𝘂𝗳𝘂𝗺𝗯𝘂𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝘆𝗮𝗻𝗮𝘆𝗼𝘄𝗮𝗸𝗮𝗯𝗶𝗹𝗶.

𝗕𝗮𝗮𝗱𝗮 𝘆𝗮 𝘂𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗶 𝘂𝘁𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗷𝘂𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝘇𝗼 𝗖𝗵𝗮 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗹𝗮𝗸𝗼, 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗹𝗲𝗻𝘆𝗲𝘄𝗲 𝗻𝗮 𝘂𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝗻𝘆𝗲𝗺𝗲𝗹𝗲𝘇𝗶.

𝗣𝗶𝗮 𝘂𝘁𝗮𝗸𝘂𝘁𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝘄𝗮𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺𝘂 𝘄𝗮𝘁𝗮𝗸𝗮𝗼 𝗸𝘂𝘀𝗶𝗺𝗮𝗺𝗶𝗮, 𝗸𝘂𝗸𝘂𝘀𝗵𝗮𝘂𝗿𝗶, 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗸𝘂𝘀𝗮𝗶𝗱𝗶𝗮

WASILIANA NASI WHATSAPP /☎️ +225 678 652 187

ETERNAL FOLIC ACID....Eternal folic acid ni aina virutubisho ambavyo vimetokana na mimea  asili ya Alfafa na GreenAlgae ...
20/08/2023

ETERNAL FOLIC ACID....Eternal folic acid ni aina virutubisho ambavyo vimetokana na mimea asili ya Alfafa na GreenAlgae pamoja na lishe inayo undea na madini k**a folic Acid,iron, calcium virutubisho hivi Husaidia kukinga mwili dhini ya magonjwa na kuhimarisha huzalishaji was seli za mwili
FOLIC ACID....Hibi virutubisho vyenye asilia ya vitamin B husaidia kulinda mwili dhidi ya homa na kuhimarisha Kinga ya mwili ,pia husaidia wakina mama wenye homa ,wajawazito,wanaonyonyesha,wanaotarajia kupata mtoto na Kwa wale wenye shida ya kuharibika au kutoka Kwa mimba

KAZI YA ETERNAL FOLIC ACID
*Husaidia kuondoa homa na maumivu ya viungo
*Husaidia kuhimarisha biungo vya uzazi aswa Kwa wakina mama wenye tatizo la mimba kuharibika
*Inahimarisha uhai wa seli za mwili
*Husaidia ku control hormones Kwa wanawakee

WATUMIAJI
*Wakina mama wajawazito
*Wakina mama wanao tarajia kupata mtoto
*Wazee
*Wenye shida ya moyo
*Wakina mama wanao nyonyesha
*Wanao sumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara Kwa mara
*Wenye Upungufu wa Kinga mwilini
Kwa maelezo zaidi piga Whatsapp 0678652187

🩺Dr.Mkelo

K**a ni wewe una kisukari Au kuna mtu unaemjua ana kisukari ni vizuri ajue/ujue upo kundi lipi, hakikisha unapitia kwa u...
03/09/2022

K**a ni wewe una kisukari Au kuna mtu unaemjua ana kisukari ni vizuri ajue/ujue upo kundi lipi, hakikisha unapitia kwa umakini taratibu kuona makundi yote 6 na kuyaelewa Kisha jitathimini wewe upo kundi gani ikisha chukua hatua

1.Kundi la kwanza wengi hulalamika madhara ya kisukari bila kujua

2.Kundi la pili wengi hawakubali matokeo ingawaje vipimo vinasoma sukari iko juu.Kundi hili huwa hawataki kusikia neno dawa mpaka waumwe sana

3.Kundi la tatu huwa wanaupokea ugonjwa wanaukubali,lakini huwa hawataki kuacha vitu vinavyosababisha kisukari k**a pombe,sigara,vyakula,unene

4.Kundi la nne wengi hujisalimisha sababu ya macho kupata hitilafu,nguvu za kiume kuisha kabisa,ganzi,shinikizo la damu

5.Kundi la tano hawa cha kushangaza huanzia miaka 45,wana historia ya kuwa na kisukari miaka 5-10 na zaidi kwa kupuuzia ugonjwa wa kisukari,hawafatilii baada ya kugundulika na sukari huendelea na maisha k**a kawaida

6.Kundi la sita wengi huwa wamekata tamaa,hata ndugu mnapo hangaika kwa niaba yao wao uhisi k**a mnajisumbua,huwa ni wakali na wakaidi wa kufata masharti

FUNZO
1.Ugonjwa wa kisukari unachukua miaka 5-10 kujitengeneza mpaka kugundulika

2.Jenga tabia ya kula vizuri na kupima afya ili uchukue hatua mapema

3.Ugonjwa wa kisukari haupotezewi ukipuuza ilo utakuja kujitambua ukiwa na madhara makubwa

4.Madhara ya kisukari hayaponi ila ugonjwa wenyewe unaweza kuudhibiti,usiogope kisukari ogopa madhara yake

Wasiliana nami mapema nikusaidie naitwa Dr Mkelo waweza kunipigia simu 0787917753

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr. J. Mkelo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Dr. J. Mkelo:

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram