Mifupa clinic

  • Home
  • Mifupa clinic

Mifupa clinic Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mifupa clinic, Medical and health, ilala, .

SABABU YA MAUMIVU YA MGONGO NA KIUNO:Maumivu ya mgongo ni ile hali ya kuhisi maumivu au kutojiskia vizuri/kawaida katika...
19/07/2022

SABABU YA MAUMIVU YA MGONGO NA KIUNO:
Maumivu ya mgongo ni ile hali ya kuhisi maumivu au kutojiskia vizuri/kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo wako (eneo lililopo kati ya kiuno na shingo).
Maumivu haya yanatofautiana baina ya mtu na mtu na pia yanategemea sana wapi ilipo shida katika mgongo wako; nini kisababishi na kiungo kilichoathiriwa (kilichoumizwa/jeruhiwa).
Vivyo hivyo dalili nazo hutegemea na kisababishi na hivyo baadhi ya watu huwa na dalili zinazofanana huku wengine wakiwa na dalili za aina mbali mbali kuanzia mamivu ya mgongo, kushindwa kufanya shughuli za kawaida za kila siku kutokana na maumivu, homa na kutetemeka, kupungua uzito (hasa baada ya ajali/magonjwa ya mifupa), kupungua nguvu katika misuli ya miguu, miguu kuwaka moto/kuchomwa chomwa mithili ya sindano au miiba, ganzi kwenye miguu hadi kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa.
Aina kuu za maumivu ya mgongo:
Mara nyingi, maumivu ya mgongo hujitokeza katika aina kuu mbili ambayo ni:
1. (Maumivu yanayosambaa) Maumivu yasiyohama (yapo katika eneo la mgongo husika hajalishi unafanya nini - localized pain). Mara nyingi maumivu ya namna hii ni yale yanayokuwa yametokana na kujeruhiwa kwa misuli/mifupa ya mgongo kwa ajali au kupigwa eneo la mgongoni. Au, ni yale yanoyotokanana mkao mbaya usiozingatia afya ya mgongo [anagalia mako mzuri katika somo “post” iliyopita –MKAO MZURI (NI UPI)?] hivyo kusababisha kuchanika kwa misuli ya ndani ya mgongo na kusababisha maumivu!!
2. Mamivu yanayosambaaa na kuangazia maeneo mengine ya mwili wako mbali na mgongo k**a vile miguu. Maumivu haya hutokana na mgandamizo katika mfumo wa fahamu/neva kutoka kwenye mifupa, uvimbe au kuumizwa kwa uti wa mgongo/neva zinazochomozea mgongoni baada ya ajali au kujeruhiwa mgongo wako kwa kupigwa/kuanguka. Mfano: shida ipo mgongoni ila unahisi ganzi kwenye m(i)guu au m(i)guu kuwaka moto).
Visababishi vya maumivu ya mgongo:
1 (Ubebaji wa mizigo) Moja ya visababishi vikuu vya maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama ni kichocheo cha kupata maumivu ya mgongo.
2. Mkao: nyumbani, kazini, shuleni, n.k wakati unafanya shughuli zako za kila siku, una nafasi kubwa katika kuongeza au kupunguza hatari ya kupata maumivu ya mgongo [anagalia mako mzuri katika somo –MKAO MZURI (NI UPI)?].
3. Ubebaji wa mizigo mizito (kufikia kilo 5 au zaidi) usiozingatia afya ya mgongo. [Somo la namna ya kubeba mizigo mizito (kufikia kilo tano au zaidi) litakujieni hivi karibuni].
4. Kulalia godoro laini na lililobonyea/linalobonyea katikati wakati wa kulaa. Hii husababisha misuli ya mgongo kuvutika kupita kiasi wakati umelala na kupelekea kuchanika hivyo kuishia (Godoro la kubonyea) katika kupata maumivu ya mgongo na ambayo hudumu kwa muda mrefu (wote) utakokuwa unalalia godoro hilo au hata zaidi.
5. Kujeruhi(wa) mgongo wako kunakotokana na ajali, michezo, kuanguka, kupigwa, n.k au uvimbe (kansa) katika uti wa mgongo.
6. Ujauzito/uzito wa kupita kiasi (kitambi): wengi wanashtuka wanaposikia kuwa uzito (kitambi) husababisha maumivu ya mgongo, ila akina mama wajawazito wanafahamu! Kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimam. Kuelemewa kwa misuli/mfupa hii husababisha mabadliko ya mwili katika kutafuta namna ya kufidia hali hiyo… mwisho ni maumivu!!!
7. Msongo wa mawazo (stress): msongo wa mawazo humfanya mtu kukaa katika mkao mbaya akiwaza na kuwazua hivyo kuishia katika kupata maumivu ya mgongo k**a nilvyotangulia kusema hapo juu.
8. Magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo k**a vile TB ya mifupa ya mgongo na misuli ya pembeni mwa mifupa hiyo na kusababisha maumivu katika eneo husika.
9. Kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgogo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ajali.
10. (Msongo wa mawazo) Umri wa uzeeni: kadri mtu anavyozidi kuukaribia uzee ndivyo kunavyozidi kutokea mabdiliko katika mifumo yote ya mwili ikiwemo ile ya mifupa-na-misuli hivyo kuleta matatizo mengine ya kimfumo yakiwemo maumivu ya mgongo na mengineyo.[Wanawake huwaathiriwa mpema katika uzee wao kuliko wanaume kutokana na mfumo wa vichocheo (homoni) vya miili yao kupungua kwa haraka zaidi baada ya miaka kati ya 45-55 ya umri wao wa kuishi).
TIBA YAKE
Tumia bidhaa na tiba lishe uondokane kabisa na tatizo Hili
Kwa mawasiliano piga 0657151811

MAUMIVU YA VIUNGO (JOINTS PAINS)Tunapokuwa na baadhi ya vitendea kazi k**a vile magari, pikipiki, baiskeli,na mengineyo ...
19/07/2022

MAUMIVU YA VIUNGO (JOINTS PAINS)

Tunapokuwa na baadhi ya vitendea kazi k**a vile magari, pikipiki, baiskeli,na mengineyo yanakuwa na vifaa vinavyozunguka lakini yameundwa kwa kutumia vyuma endapo ukilisikia lina pinga kelele sehemu ambapo kumeuganishwa kwa kutumia oil/griss pamoja na vitu vigine hii humanisha kuwa sehemu hiyo kuna upungufu wa oil kuna msuguano kati ya chuma na chuma ndo maana utasukia makelele na kukimbiza usafiri wako gereji au kwa fundi ili kulirekebisha.
Tumeona kwa baadhi ya vifaa kuwa vimeundwa kwa vyuma na ili kuhakikisha hicho chuma kinazungungaka kwa ulaini ni lazima kuwepo na oils na vitu vingine je kwa binadamu tunazingatia au tunaangalia vitu gani maana binadamu hajaumbwa kwa kutumia vyuma bali kwa kutumia mifupa, hivyo ni muhimu kupata elimu ya mifupa na maungio kwa ujumla kuanzia uti wa mgongo hadi kwenye miguu, pingili za uti wa mgongo.

VISABABISHI VINAVYOHARIBU VIUNGO

• UZITO ULIOPITILIZA. Uzito wa mwili wa binadamu hulemea kwenye uti wa mgongo hivyo mtu anapokuwa na uzito ulio mkubwa Zaidi ni kirahisi sana huyu mtu kupata maumivu ya mgongo na hadi kwenye maungio kwa ujumla hasa na magoti kwa sababu miguu huzidiwa uzito ulioko juu na kuyafanya magoti kusangika au kumaliza ute ute uliko kwenye joints kwa haraka Zaidi.

• VITI (SIT) VYA KUKALIA HASA VYA MAOFISINI NA KWENYE MAGARI. Zamani maofisini kulikuwa na viti vya mbao maarufu k**a office chair kwa utafiti unaonyesha kuwa viti vya maofisini vya kisasa na za kwenye magari mtu anapokaa lazina kiti chenyewe kimfanya ajikuje tu bila hata ya yeye kulazimishwa kujikuja sasa jiulize , ofisini unaukuja mgongo, kwenye gari unaukuja mgongo, na wengine hadi nyumbani kuna makochi au viti vya kumfanya tena aukuje mgongo je ndani ya miaka mitatu na kuendelea kwa nini usipate maumivu ya mgongo?

• KIFUA KIKUU(TB), kwa ufupi maradhi k**a ya TB hukimbilia kwenye mifupa hasa kwenye maungio au joints na kwenda kudhoofisha gegedu (cartilage) na kupelekea mifupa kusagana kati ya mfupa na mfupa

• TEZI DUME. Nyoga, mgongo na tezi dume viko karibu sana endapo mtu atapata madhara ya tezi dume k**a vile kansa au madhara ya aina yoyote ni kirahisi sana kupata maumivu ya nyonga au mgongo hii huwapata sana wanaume lakini siyo kila anaepata maumivu ya nyonga na mgongo basi ana tezi dume no ni muhimu kufanya uchunguzi/vipimo..

• UPUNGUFU WA MADINI YA CALCIUM. Na hii ni tatizo kubwa mno maana calcium ndo kichochezi kikuu cha kuhakikisha mifupa ikon a ubora wake ulio Imara Zaidi kwa upande wa wanawake hupoteza calcium nyingi pale anapoanza kuja kwenye hedhi hadi pale anapoja kubeba mimba mtoto nae anahitaji calcium kutoka kwa mama yake hivyo ndo maana wamama wengi walio na umri ambao umeenda enda kidogo huteseka sana na miguu kuwaka moto hasa kwenye magoti kwa sababu hupoteza calcium kwa wingi Zaidi.

MADHARA YAPI MTU MWENYE MAUMIVU YA MGONGO, MAGOTI NA VIUNGO KWA UJUMLA HUKABIRIANA NAYO.
K**a magari na vifaa vingine vinavyo zunguka kwa kutumia vilaishi mbalimbali pale vinapokosa ubora wa kulainishwa au vinapopata changamoto mbalimbli huleta shida katika utendaji kazi wake na kila tatizo huwa linatengemeana na kiasi gani limeathiri. hata katika upande wa mifupa kwa mwanadamu na joints kwa ujumla pale inapokosa ubora mwathirika hupatwa na moja ya changamoto k**a zifuatazo;

i. Kukosa uwezo wa kihisia. Asilimia kubwa mtu anapopatwa na changamoto za mifupa au kwenye maungio ya aina yoyote swala la tendo la ndoa au kihisia kimapenzi hupotea na muda mwingine hujawa na hasira za ajabu ajabu bila kujari au bila hata yay eye mwenye kujua k**a ana hasira.

ii. Ulemavu. Kadiri mtu anapokuwa anaendelea kuzeeka k**a tayari ana maumivu ya viungo ni kirahisi kabisa kuja kuwa mlemavu wa viungo na wengine hushidwa kutembea au kuinama hasa pale anapofikia umri wa kuanzia miaka ya 50+ na wengine huanza kutembelea fimbo kumbe ni tatizo tu la kutokuwa na mifupa imara na iliyopoteza ubaora wake.

iii. Kansa ya mifupa au wepesi wa uzito wa mifupa. Mfupa au mifupa inatakiwa kuwa na uzito ulio standard lakini kuligana na changamoto za hapa na pale pamoja na utumiaji wa madini ya fluoride kwa wingi kutoka kwenye dawa za meno na kwenye maji na kutokupata vitamin D ya kutosha kutoka kwenye vyakula mbalimbali mifupa ya mwanadamu huadhirika na inakuwa kirahisi kuvujika n ahata ikivunjika vi vigumu au huchukua muda mrefu kujiunga na kuwa mhanga wa ugonjwa wa mifupa.

SULUHISHO LA KUIMARISHA VIUNGO.
Hakuna maumivu yasiyokuwa na mwisho wake lakini hadi uamue kuwa umechoshwa na maumivu kwenye afya ya mwili wako k**a niya ipo ya kujiboresha ipo hivyo usikate tamaa kuendelea kusoma nakala hii hadi mwisho, hivyo kampuni imeandaa program ambayo inahakikisha ukiwa na niya ya kuitumia utaachana na hali ya maumivu hata k**a ukiwa uzito uliozidi inakufanya kuwa na uzito ulio sawa na urefu

a. Inakusaidia kukupa calcium asili kwa ajili ya kulida mifupa kuwa imara na kwa wanawake inawaogezea kiwango kibwa cha calcium maana huwa wanapoteza calium nyingi kipindi cha hedhi na pale wanapojifungua .

b. Inaongeza maji maji (lubricant) kwenye joints ili kuepusha msuguano kati ya mfupa na mfupa na kuondoa tatizo la miguu kuwaka moto na kujihisi vizuri na kuwasaidia wachezaji na wanajeshi kwani kazi zao nyingi huetemea joint hasa pale wanapokuja kusitaafu tatizo la miguu huwaadama kwa kasi kubwa.

c. Inazarisha seli za kwenye mwisho wa mfupa maarufu k**a cartilage au gegedu.

Inaimarisha na kuondoa changamoto ya miguu kujaa maji au kuvimba pamoja na kufa ngazi kwa mikono na miguu.

piga 0657151811

19/07/2022
19/07/2022

Address

Ilala

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mifupa clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Mifupa clinic:

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram