30/05/2024
Ni mambo gani unapaswa kuzingatia unapochagua dawa kwaajili ya mteja au mgonjwa wako?...
Hili swali ni kwako ndugu Mtaalamu wa Afya hususani mfamasia au Daktari.pengine Kuna vitu mbali mbali hukufanya uchukue hatua na kumshauri mteja wako dawa au kifaa tiba Cha kutumia miongoni mwa vingi vilivyoko sokoni au katika makundi mbalimbali.
Yafuatayo ni miongoni mwa mambo ya kuzingatia:-
1.Jambo la kwanza ni uwezo wa bidhaa husika kutatua changamoto ya mteja wako.Mfano, tatizo linalomsumbua ni Malaria,basi dawa ya kutibu malaria na changamoto zinazoambatana na ugonjwa huo zitakua chaguo sahihi,lakini ziko dawa nyingi za Malaria...
2.Kuzingatia miongozo ya matibabu Ili kubaini ni dawa gani itolewe badala ya nyingine,hivyo Kuna dawa za mstari wa mbele na nyingine huweza kufuatia kulingana na hali ya ugonjwa (degree and severity of the patient).
3.Endapo dawa pendekezwa au kifaa tiba kipo Cha wazalishaji tofauti ni vema kuzingatia ufanisi,ubora, usalama,unafuu wa kutumia (friendly user product).
4.Zingatia hali ya usajili na kusudio la mtengenezaji pamoja na upatikanaji wa bidhaa na gharama (dawa au kifaa tiba kiwe ni Cha gharama anayoweza kumudu mteja).
5.Zipo sababu nyingine za kitaalamu zinazoendana na sera za ndani pamoja na vipaumbele zinazolenga kudumisha ubora wa huduma mathalani kutoa zile bidhaa zilizokaa muda mrefu,zilizo kwenye mpango wa kampeni na zinazosaidia kuongeza kipato na kuchangia upatikanaji wa huduma endelevu.
6.MUHIMU SANA zingatia usalama wa mtumiaji, bidhaa inayoweza kusababisha madhara makubwa au ulemavu ama kifo isitolewe kwa mgonjwa au mtu ambae anajulikana kuwa na shida nayo iwe mzio au muingiliano. Mteja wa namna hii mchagulie dawa isiyo na shida kutoka katika kundi tofauti na dawa zinazompa shida.Jitahidi kudodosa hili mara kwa mara unapohudumia wateja wako.
Haya ndio yangu ya Leo,ongezea mengine.nitafute kwa barua pepe jumakitenge208@gmail.com au simu +255654661842 ama tiririka hapa chini
Dawa Bora,yenye ufanisi na salama pamoja na vifaa tiba iwe kipaumbele chako mtaalamu na mwanajamii mwenzangu...Asante