08/08/2023
FAIDA ZA NDIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU
TOFAUTI na vyakula vingine, ndizi zinafaida kubwa sana katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ndizi zina virutubisho vya aina mbalimbali k**a vile, protini, mafuta, kalishiamu, wanga, fosiforas, madini ya chuma, vitamin A,B,C na maji.
Ndizi zina faida zipi katika urembo? Chanzo cha nishati Ndizi zina uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi zaidi, tena zina nishati kubwa, sukari iliyomo katika ndizi ni chanzo kizuri sana cha nishati.
Hivyo naweza kusema kuwa ndizi ikiliwa ipasavyo itakusaidia kujenga mwili na misuli yako kwa ujumla. Husaidia kuondoa chunusi Chunusi ni miongoni mwa matatizo ambayo huwasumbua warembo wengi hususan wanawake.
Je, unafahamu kuwa ndizi mbivu zinaweza kukuondolea tatizo hilo? Kwa kuchanganya ndizi mbivu na maziwa na asali na kisha kuzisaga ili kupata urojo ambao utatumia kupaka kwenye maeneo yaliyoathirika, unaweza kuondokana kabisa na tatizo hilo.
Fanya hivyo kila siku na hakikisha unakaa na mchanganyiko huo kwa muda usiopungua dakika 30 hadi 40, kisha osha na maji ya baridi ikiwezekana yaliyopozwa na jokofu.
Ndizi katika ‘diet’ Ndizi zina nafasi kubwa sana kati kuongeza au kupunguza uzito, hivyo unaweza kutumia ikiwa unahitaji kupunguza ama kuongeza uzito wako.
Kwa wajawazito Ndizi ni chakula kizuri kwa wanawake wajawazito, kwani kina kiwango kikubwa cha ‘folic acid’ ambayo inaweza kufyonzwa kwa urahisi sana na kiumbe kilicho tumboni. Ikiwa mama mjamzito atatumia ndizi mara kwa mara ni wazi kuwa atakuwa mwenye muonekano mzuri na wa kuvutia.
Ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, presha, vidonda vya tumbo, saratani ya figo, kukosa choo
Ndizi mbivu ni tunda ambalo linafahamika na kila mtu, lakini sina hakika k**a watu wengi wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo linapatikana kirahisi sana nchini. Bei yake ni kati ya shilingi 50 na 150 tu, kiwango cha pesa ambacho kila mtu anaweza kukimudu.
Iwapo ulikuwa hujui umuhimu wa kula ndizi mbivu, leo utalazimika kubadili matizamo