eHealthtz

eHealthtz Linda Afya Yako

03/04/2023

*PELVIC INFLAMMATORY DISEASE (PID)*
-Ni maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke yaani uterus, Fallopian tube, o***y na parametrium.

*💥 HUSABABISHWA NA WADUDU WAJULIKANAO K**A:*
🖍️Gonococci
🖍️Chlamydia
Hawa wawili ndo visababishi vikubwa vya PID, na vinginevyo K**a vile:
🖍️ Staphylococcus
🖍️ Streptococcus
🖍️ Coliforms
🖍️ Mycoplasma
🖍️Colistridium perfringens

🔷Kwa Asilimia Kubwa huenezwa Kwa njia ya tendo la ndoa.
🔷Njia zingine ni k**a:
👉 Wakati wa ukuwekewa kitanzi cha uzazi wa mpango
👉 Wakati wa kutoa mimba
👉 Wakati wa kujifungua mtoto
👉 Wakati wa Upasuaji wa endometrium

*💥 DALILI ZA PID NI HIZI HAPA💥*
🖍️Kutoka uchafu usio wa kawaida ukeni, wenye rangi ya maziwa mtindi yaani mweupe
🖍️ Muwasho ukeni
🖍️ Maumivu makali ya Tumbo, chini ya kitovu
🖍️ Harufu mbaya ukeni
🖍️ Hedhi isiyoeleweka yaani Mara mbili ndani ya mwezi mmoja
🖍️ Maumivu makali wakati wa hedhi
🖍️ Maumivu wakati wa kufanya mapenzi
🖍️Kutoka damu baada ya tendo
🖍️ Kichefuchefu
🖍️Kukosa hamu ya chakula
🖍️ Kuchokachoka
🖍️ Maumivu ya kiuno na mgongo

*🔷WATU WALIOPO KWENYE HATALI YAKUPATA PID NI🔷*
👉Watu waliofikia umri wa kufanya mapenzi
👉Watu wenye mahusiano na mpenzi zaidi ya moja
👉Wenye upungufu wa Kinga ya mwili
👉Wenye historia ya kuwa na PID
👉Wenye kuingiziwa vitanzi

*🔷 MADHARA YA PID NI🔷*
🖍️Ugumba/kushindwa kubeba mimba
🖍️Mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi
🖍️ Maumivu ya muda mrefu
🖍️ Kutungwa kwa usaha
🖍️Mimba kuharibika
🖍️Kukosa hamu ya tendo la ndoa
🖍️ Maumivu wakati wa tendo la ndoa
🖍️Mirija ya uzazi kuziba
🖍️Kupata saratani ya shingo la kizazi
🖍️Kuvurugika kwa mfumo wa homoni

*DALILI ZA HORMONAL IMBALANCE*
🖍️ Kukosa hedhi kabsa
🖍️ Kuingia hedhi Mara mbili ndani ya mwezi mmoja
🖍️ Maumivu makali wakati wa hedhi
🖍️ Kupata hedhi ya mabonge mabonge K**a maini
🖍️Hasira za Mara kwa mara wakati wa hedhi
🖍️ Kuchoka choka kusiko kawaida
🖍️ Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
🖍️Kukosa hamu ya tendo la ndoa
🖍️Uke kuwa mkavu isiyo kawaida
🖍️ Maumivu makali ya mgongo na kiuno
🖍️Kushindwa kubeba mimba

*✅KARIBU SANA TUJENGE AFYA BORA,*
*Hata kwa wale wenye PID sugu na wametumia madawa mengi bila mafanikio tunawasaidia wanapona kabsa.*

*✅ Wasiliana nami mapema ili nikusaidie kabla Tatizo halijawa kubwa Sana*

*🖍️tuNatoa huduma ya ushauri bure🤝🤝🤝*
*Pia tuNatoa tiba ya magonjwa mbalimbali sugu na yasiyo sugu. Karibu sana.*

* Ni Bora Zaidi #*

*Wasiliana Nasi kupitia 0687347027 whatsapp only*

JE WAJUA : UFAHAMU UGONJWA WA MENINGITIS Meningitis huweza kutokea kwa sababu ya maambukizo au bila maambukizo. Kuna vir...
15/02/2023

JE WAJUA : UFAHAMU UGONJWA WA MENINGITIS
Meningitis huweza kutokea kwa sababu ya maambukizo au bila maambukizo. Kuna virusi, bakteria, fungi, na vimelea wa aina nyingi wanaoweza kuleta meningitis. Magonjwa yanayoweza kusababisha uvimbe mwilini bila maambukizo (k**a systemic lupus erythematosus na Bahcet’s disease) yanaweza kusababisha aseptic meningitis (meningitis isiyotokana na bakteria.) Baadhi ya madawa huweza kusababisha aseptic meningitis, k**a ibuprofen au antibiotic iitwayo trimethoprim-sulfamethoxazole.

Dalili Za Meningitis
Dalili za kawaida za meningitis huwa:
Kuumwa kichwa Homa kali Shingo kuk**aa Maumivu machoni ukiona mwanga (photophobia).

Ishara ambazo tabibu atazitazama wakati wa uchunguzi wa meningitis ni pamoja na ishara za Kernig na Brudzinski. Ishara ya Kernig hutazamwa ifuatavyo: Mgonjwa akiwa amelalia mgongo, mguu unakunjwa nyuzi 90 sehemu ya nyonga na goti kukunjwa nyuzi 90. Ikiwa mgonjwa atapata shida sana wakati wa kunyoosha goti lililokunjwa huku nyonga ikiwa bado imekunjwa nyuzi 90, hiyo ni ishara ya meningitis. Ishara ya Brudzinski hutazamwa ifuatavyo: Mgonjwa akiwa amelalia mgongo na miguu ikiwa imenyooshwa kitandani, tabibu atakinyanyua kichwa mbele sehemu ya shingo. K**a tendo hili litaifanya miguu kunyanyuka na kujikunja kwenye magoti, hii ni ishara ya meningitis.

Dalili za homa ya uti wa mgongo huweza kutokea ghafla na hufanana na mafua (flu.) Kwa mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 2, zinaweza kuwa:
Homa kali ya ghafla Kukak**aa shingo Maumivu makali ya kichwa yasiyo ya kawaida Maumivu ya kichwa yanayoambatana na kichefuchefu na kutapika Kifafa Kutopenda mwanga Kukosa hamu ya kula au kiu Mabadiliko katika tabia, k**a kuchanganyikiwa, kukosa usingizi na shida kuamka asubuhi.

Dalili kwa watoto wadogo hazijitambulishi vizuri na zinaweza kuwa:
Homa kali Kulia kila wakati Kusinzia muda mrefu zaidi Kutocheza kuchoka kukataa kula uvimbe utosini Kukak**aa kwa shingo na mwili



Aina Za Meningitis


Meningitis inaweza kuwa kali (acute meningitis) – ambapo ugonjwa unakuja ghafla na kudumu muda mfupi – au sugu (chronic) ambapo ugonjwa huanza taratibu na kudumu muda mrefu. Meningitis inayotokana na maambukizo ni pamoja na bacterial meningitis (kutokana na maambukizo ya bakteria), viral meningitis ( kutokana na maambukizo ya virusi ) na parasitic meningitis (kutokana na maambukizo ya vimelea).

Meningitis ya kuambukiza mara nyingi hutokana na kuwepo ndani ya jamii. Ni mara chache sana mgonjwa hupata bacterial na fungal meningitis kutokana na shughuli za kwenye mahospitali au za tiba.

Chanzo kikuu cha meningitis ni virusi ikifuatiwa na bakteria. Mara chache sana meningitis husababishwa na fungus. Maambukizo ya bakteria yanaweza kuwa hatarishi sana kwa maisha ya mgonjwa.



Homa Ya Uti Wa Mgongo Kutokana Na Bakteria – Bacterial meningitis

Bakteria wanaoiingia ndani ya mfumo wa damu na kusafiri hadi kwenye ubongo na uti wa mgongo husababisha homa kali ya uti wa mgongo. Lakini ugonjwa unaweza kutokea pale bakteria wanaposhambulia meninges moja kwa moja. Hili linaweza kutokea baada ya maambukizo kwenye sikio au pua, mvunjiko kwenye fuvu, na, mara chache baada ya upasuaji.

Kuna koo za bakteria wanaoweza kuleta meningitis kali, na hasa:

Streptococcus pneumoniae (pneumococcus). Bakteria huyu ndicho chanzo kikuu cha homa ya uti wa mgongo inayotokana na bakteria kwa vichanga, watoto wadogo na watu wazima. Kwa kawaida huleta pneumonia au maambukizi kwenye masikio au pua. Chanjo yaweza kusaidia kuzuia aina hii ya meningitis.
Neisseria meningitidis (meningococcus). Bakteria huyu ni moja ya wale wanaoongoza katika kuleta bacterial meningitis. Bakteria huyu huleta maambukizo kwenye sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji lakini pia anaweza kuleta meningococcal meningitis akiingia ndani ya mfumo wa damu. Wanaweza kuambukiza kwa haraka na huathiri zaidi vijana wa umri mdogo na wa kati. Wanaweza kuleta mlipuko kwenye mabweni ya shule na kambi za jeshi. Chanjo husaidia kuzuia ugonjwa huu

Haemophilus influenzae (haemophilus). Bakteria aitwaye Haemophilus influenzae type b (Hib) alikuwa ni kiongozi wa bacterial meningitis hapo zamani kwa watoto wadogo. Lakini baadaye sindano za Hib zimepunguza sana ugonjwa wa aina hii.
Listeria monocytogenes (listeria). Bakteria hawa hupatikana ndani ya chakula ambacho hakikuchukuliwa tahadhari za kutosha kuua bakteria (unpasteurized cheeses, hot dogs and lunchmeats.) Wanawake wenye mimba, vichanga, wazee na watu wenye kinga ndogo za mwili, ndiyo wahanga wakuu.



Homa Ya Uti Wa Mgongo Kutokana Na Virusi – Viral meningitis

Homa ya uti wa mgongo kutokana na virusi kwa kawaida huwa si kali sana na mara nyingi mgonjwa hupona mwenyewe. Virusi k**a herpes simplex virus, HIV, mumps, West Nile virus na wengine huweza kusababisha homa ya uti wa mgongo.

Chronic meningitis

Viumbe wakuao taratibu (k**a fungi na Mycobacterium tuberculosis) ambao hushambulia ngozi laini na majimaji yanayozunguka ubongo husababisha meningitis sugu. Meningitis sugu hukua katika kipindi cha wiki mbili au zaidi. Dalili za chronic meningitis ni – maumivu ya kichwa, homa, kutapika na kichwa kuwa kizito.



Fungal meningitis

Homa ya uti wa mgongo kutokana na fangasi haionekani mara nyingi na husababisha meningitis sugu. Hufanana sana na meningitis kali ya bakteria. Meningitis ya fangasi haiambukizi kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Aina ya fangasi waitwao Cryptococcal meningitis ndiyo inayoonekana zaidi na huathiri zaidi watu wenye upungufu wa kinga za mwili, k**a UKIMWI. Huweza kuwa tishio kwa maisha k**a tiba ya fangasi haitatolewa.



Vyanzo Vingine Vya Homa Ya Uti Wa Mgongo

Homa ya uti wa mgongo huweza kusababishwa na vyanzo vingine ambavyo si vya maambukizo, k**a kudhurika kutokana na dawa, mzio wa madawa, aina fulani za saratani na magonjwa k**a sarcoidosis.

Mazingira Hatarishi Kwa Meningitis


Mazingira hatari kwa homa ya uti wa mgongo ni pamoja na:
Kuruka sindano. Hatari hutokea pale mtu ye yote anapokosa kukamilisha sindano za utotoni au ukubwani alizoandikiwa. Mara nyingi viral meningitis hutokea kwa watoto wenye umri wa pungufu ya miaka 5. Bacterial meningitis ni kwa wale wenye umri chini ya miaka 20.
Kuishi kwenye jumuia. Watoto wa shule waishio kwenye mabweni, wanajeshi, watoto kwenye maeneo ya kulelea watoto wapo kwenye hatari kubwa ya kupata meningococcal meningitis. Hii huenda ni kwa sababu bakteria huyu huenezwa kwa njia ya upumuaji, na kuenea kwa haraka kwenye makundi makubwa.
Ujauzito. Ujauzito huongeza hatari ya listeriosis – maambukizi ya bakteria wa listeria, ambao wanaweza kasababisha meningitis. Listeriosis huongeza uwezekano wa mimba kutoka, kuzaa mtoto aliyefariki na kuzaa kabla ya muda.
Upugufu wa kinga za mwili. UKIMWI, unywaji wa pombe, kisukari na vitu vingine vinavyochangia kupungua kwa kinga za mwili hukuweka kwenye hatari ya homa ya uti wa mgongo. Kuondolewa bandama pia kunachangia

Madhara Ya Kudumu Ya Homa Ya Uti Wa Mgongo


Madhara huweza kuwa makubwa. Kadiri wewe au mtoto wako anavyokaa muda mrefu zaidi bila tiba, ndivyo uwezekano wa kupata kifafa na uharibifu wa kudumu wa neva unavyoongezeka, ikiwa ni pamoja na:
Kupoteza uwezo wa kusikia Kupoteza kumbukumbu Kupoteza uwezo wa kujifunza Uharibifu wa ubongo Kifafa Figo kushindwa kufanya kazi Kifo





Namna Ya Kujikinga


Bakteria na virusi waletao homa ya uti wa mgongo wanaweza kuenezwa kupitia kukohoa, kupiga chafya, kubusiana na kushirikiana vyombo, mswaki au sigara.

Hatua zifuatazo zinaweza kusaidia:
Kuosha mikono. Osha mikono yako kwa makini kuzuia kuenea kwa vijidudu. Wafundishe watoto wako kuosha mikono ipaswavyo kila wakati, hasa kabla ya kula, baada ya kujisaidia, baada ya kuwa kwenye makundi ya watu na baada ya kuchezea wanyama. Usafi. Usishiriki vinywaji, chakula, mirija, miswaki na mtu mwingine. Wafundishe watoto kutoshiriki vitu hivi. Kutunza afya. Linda kinga za mwili wako kwa kupata muda wa kutosha wa kujipumzisha, kufanya mazoezi mara kwa mara, na kula chakula bora chenye matunda mengi, mboga na nafaka nzima. Kuziba mdomo. Unapokohoa au kupiga chafya ziba mdomo wako na pua. K**a ni mjamzito, kuwa mwangalifu na chakula. Jilinde kwa kupika nyama kwa moto mkali (74C). Kuwa makini na jibini.

Kila unapokula hakikisha unatumia matundaLike &share
15/02/2023

Kila unapokula hakikisha unatumia matunda
Like &share

JE WAJUA : FAHAMU VYAKULA VYENYE URIC ACID NYINGIAsidi ya Uric ni taka mwili inayopatikana kwenye damu. Inaundwa wakati ...
13/02/2023

JE WAJUA : FAHAMU VYAKULA VYENYE URIC ACID NYINGI
Asidi ya Uric ni taka mwili inayopatikana kwenye damu. Inaundwa wakati mwili unavunja kemikali zinazoitwa purines. Asidi nyingi ya uric huyeyuka katika damu, hupita kwenye figo na kutoka mwilini kupitia kwenye mkojo. Chakula na vinywaji vyenye purines pia huongeza kiwango cha asidi ya mkojo.
Baadhi ya vyakula vyenye purine nyingi ni pamoja na :
*Nyama nyekundu.
*Nyama za viungo k**a ini.
*Chakula na vinywaji k**a pombe (hasa bia,).

Ikiwa asidi ya uric nyingi hubakia katika mwili, hali inayoitwa hyperuricemia itatokea. Hyperuricemia inaweza kusababisha mawe(crystal)ndani ya mkojo (au urate) kuundwa. Mawe haya yanaweza kukaa kwenye viungo na kusababisha gout, aina ya arthritis ambayo inaweza kuwa na maumivu makali sana. Wanaweza pia kukaa kwenye figo na kuunda mawe kwenye figo .

Mimi naitwa Dr. elly karibu kwa ushauri sahihi wa afya yako pamoja na matibabu sahihi

K**a una swali au unahitaji ushauri na matibabu karibu sana ndugu yangu
namba yangu whatsapp 👉👉+255687347027
eHealthtz "Linda afya Yako"

Lengo la ehealthtz ni kuhakikisha watu wote tunakuwa na afya njema ili tumtukuze Mungu kwa nguvu na uwezo

JE WAJUA;UFAHAMU UGONJWA WA GOUT Gout Ni Nini? Gout ni namna moja ya Arthritis, ugonjwa ambao hushambulia joints (sehemu...
13/02/2023

JE WAJUA;UFAHAMU UGONJWA WA GOUT

Gout Ni Nini?


Gout ni namna moja ya Arthritis, ugonjwa ambao hushambulia joints (sehemu za maungio ya mifupa). Huu ndiyo ugonjwa wa joints ambao huwashambulia sana na kuwapa maumivu makali wanaume. Wanawake pia huweza kuathirika na ugonjwa huu hasa baada ya kukoma hedhi. Ugonjwa huu huleta maumivu makali ya ghafla, hasa kwenye sehemu linapoanzia dole gumba la mguu. Dalili za ugonjwa huanza kuonekana pale uric acid, tindikali ambayo huzalishwa na mwili katika ufanyaji kazi wake (ambayo haina manufaa kwa mwili) inapobakia katika viungo vya mwili na katika majimaji ya mwili. Uric acid iliyoganda (tophi) huweza kujikusanya na kubaki chini ya ngozi inayozunguka joints, huweza pia kujikusanya ndani ya figo na kusababisha kidney stones (namna ya kokoto ndogo ndani ya figo).

Gout inaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye maungio ya mifupa na figo. Endapo hatua za kuutibu ugonjwa huu hazitachukuliwa kwa muda mrefu (miaka 10 au zaidi), madhara ya kudumu humtokea mgonjwa.



Chanzo Cha Gout Ni Nini?


Gout hutokea kimsingi pale tindikali aina ya uric (uric acid) inapozidi kiwango katika mwili wa binadamu hali ambayo kitaalamu huitwa hyperuricemia. Tindikali hii ni matokeo ya kuvunjwavunjwa na mwili kwa aina fulani za chakula k**a nyama, nyama ya kuku na chakula cha baharini. Tindikali hii kwa kawaida huchanganyika na damu na mwisho hutolewa nje ya mwili pamoja na mkojo kupitia figo. Tindikali hii ikitengenezwa kwa wingi mno au isipotolewa nje ya mwili kwa kiwango kinachostahili, ile inayobakia huganda na kukaa kwenye maeneo ya joints na kusababisha maumivu kwenye joints hizo na maeneo yaliyo karibu. Kuna mazingira ambayo hupelekea hali hii ya uzidifu wa tindikali ya uric katika mwili na mwishowe gout kutokea nayo ni:

Vitu vinavyokunakufanya uwe kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu.

Mtindo wa maisha: Unywaji wa pombe huzuia utolewaji wa uric acid nje ya mwili na ulaji wa chakula chenye purine kwa wingi husababisha kiwango cha tindikali ya uric kuwa kikubwa mwilini.
Madini ya lead: Kuwa karibu na madini haya kwa muda mrefu kumeonyesha kuhusika na aina fulani za gout.
Madawa: Baadhi ya madawa yameonekana kuongeza kiwango cha uric acid mwilini.
Unene: Unene umedhihirika kuongeza hatari ya kupatwa na gout.
Matatizo ya kiafya: K**a figo hazifanyi kazi vizuri kiwango cha uric acid mwilini kitapanda. Matatizo mengine ya kiafya yanayochangia ni high blood pressure (hypertension), kisukari na hypothyroidism.

Dalili Za Gout
Gout ina tabia ya kuleta maumivu makali ya ghafla, uvimbe na wekundu mara nyingi kwenye joint moja, na hasa maungio ya kwenye dole gumba.

Maumivu ya gout hutokea ghafla, mara nyingi yatakuamsha usiku katikati ya usingizi ukihisi dole gumba linawaka moto. Eneo hilo huwa la moto, lililovimba na hata uzito wa shuka kuuona kuwa mkubwa sana usiovumilika.

Ugonjwa huanza kwa kuleta maumivu makali kwenye maungio ya mifupa na mara nyingine kuambatana na uvimbe. Pamoja na kuwa gout mara nyingi hushambulia maungio makubwa ya dole gumba la mguu, huweza pia kushambulia maungio ya mikono, ankles, viwiko vya mikono na vidole.


Tiba Ya Gout


Matatizo yaliyo mengi ya gout huondolewa kwa kutumia dawa. Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs), colchicine au corticosteroids hutumika kuondoa maumivu kwenye eneo lililoathirika na gout.

Dawa nyingine hutumiwa ili kupunguza uzalishaji wa uric acid (xanthine oxidase inhibitors), mfano allopurinol au kuzisaidia figo ziweze kuondoa tindikali ya uric kutoka katika mwili (probenecid).

Mtindo wa maisha unaweza kusaidia katika kupunguza makali ya ugonjwa huu au kuzuia usikupate. Yafaa kufanya yafuatayo:

– Kunywa maji mengi, lita 2-4 kwa siku

– Kutokunywa pombe

– Kuweka uzito wa mwili kwenye kiwango kinachofaa

– Kupata mlo uliokamilika (balanced diet)

– Kutotumia vyakula vyenye purines kwa wingi (vinavyozalisha uric acid kwa wingi). Vyakula vya kukwepa ni k**a figo za ng’ombe, maharage na njegele zilizokaushwa, nyama pori, uyoga na maini.

Mimi naitwa Dr. elly karibu katika kujifunza na kujua habari zote zinazohusu afya

K**a una swali au unahitaji ushauri na matibabu
namba yangu whatsapp 👉👉+255687347027
eHealthtz "Linda afya Yako"

MFUMO WA CHAKULA ILI KUPUNGUZA BLOOD PRESSURE DASH inasimama kwa Njia za Chakula za Kuzuia Shinikizo la damu  (shinikizo...
12/02/2023

MFUMO WA CHAKULA ILI KUPUNGUZA BLOOD PRESSURE

DASH inasimama kwa Njia za Chakula za Kuzuia Shinikizo la damu (shinikizo la juu la damu). Lishe ni rahisi:

Kula matunda zaidi, mboga mboga, na vyakula vya maziwa vyenye mafuta kidogo
Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi , cholesterol na mafuta ya trans
Kula zaidi vyakula vya nafaka nzima, samaki, kuku na karanga
Punguza sodiamu, peremende, vinywaji vyenye sukari na nyama nyekundu
Katika tafiti za utafiti, watu ambao walikuwa kwenye lishe ya DASH walipunguza shinikizo la damu ndani ya wiki 2.

Lishe nyingine -- DASH-Sodiamu -- hutaka kupunguza sodiamu hadi miligramu 1,500 kwa siku (karibu 2/3 kijiko cha chai). Uchunguzi wa watu kwenye mpango wa DASH-Sodiamu ulipunguza shinikizo lao la damu pia.

Kuanzisha Lishe ya DASH
Lishe ya DASH inahitaji idadi fulani ya huduma kila siku kutoka kwa vikundi anuwai vya chakula. Idadi ya huduma unayohitaji inaweza kutofautiana, kulingana na kalori ngapi unahitaji kwa siku.

Unaweza kufanya mabadiliko ya taratibu. Kwa mfano, anza kwa kujiwekea kikomo hadi miligramu 2,400 za sodiamu kwa siku (takriban kijiko 1 cha chai). Kisha, baada ya mwili wako kuzoea lishe, punguza hadi miligramu 1,500 za sodiamu kwa siku (karibu 2/3 kijiko cha chai). Kiasi hiki kinajumuisha sodiamu yote inayoliwa, ikiwa ni pamoja na sodiamu katika bidhaa za chakula na vile vile unavyopika au kuongeza kwenye jedwali.

Vidokezo vya Dash Diet

Ongeza sehemu ya mboga wakati wa chakula cha mchana na chakula cha jioni.
Ongeza sehemu ya matunda kwenye milo yako au k**a vitafunio. Matunda ya makopo na yaliyokaushwa ni rahisi kutumia, lakini hakikisha kuwa hayana sukari iliyoongezwa.
Tumia nusu tu ya chakula chako cha kawaida cha siagi, majarini, au mavazi ya saladi, na tumia vitoweo visivyo na mafuta kidogo au visivyo na mafuta .
Kunywa bidhaa za maziwa zilizo na mafuta kidogo au skim wakati wowote ambao kwa kawaida ungetumia mafuta kamili au cream.
Punguza nyama hadi wakia 6 kwa siku. Fanya baadhi ya milo kuwa mboga.
Ongeza mboga zaidi na maharagwe kavu kwenye lishe yako.
Badala ya kula chipsi au peremende, kula pretzels au njugu zisizo na chumvi, zabibu kavu, mtindi usio na mafuta kidogo na usio na mafuta, mtindi uliogandishwa, popcorn zisizo na chumvi zisizo na siagi, na mboga mbichi.
Soma lebo za vyakula ili kuchagua bidhaa ambazo ni chini ya sodiamu.

JE WAJUA: UGONJWA WA RHEUMATOID ARTHRITIS Rhematoid arthritis (RA) ni ugonjwa wa kinga za mwili (autoimmune disease) amb...
12/02/2023

JE WAJUA: UGONJWA WA RHEUMATOID ARTHRITIS

Rhematoid arthritis (RA) ni ugonjwa wa kinga za mwili (autoimmune disease) ambapo kinga za mwili – ambazo kazi yake ni kuulinda mwili kwa kushambulia vitu vinavyouvamia mwili kutoka nje k**a bakteria na virusi – kwa bahati mbaya hushambulia maungio ya mifupa. Hii huleta madhara ambayo husababisha tishu ambazo zinatanda kwenye maungio ya mifupa kwa ndani (synovium) kuongezeka unene, na kusababisha kuvimba na maumivu kwenye maungio ya mifupa. Synovium hutengeneza ukano (ute) ambao hulainisha maungio ya mifupa na kuisaidia kufanya miondoko kiulaini

Hatua zipaswazo zisipochukuliwa kuidhibiti hali hiyo, gegedu huweza kuharibiwa pamoja na mifupa yenyewe. Hatimaye, gegedu huisha kabisa, na nafasi kati ya mifupa huwa ndogo. Maungio ya mifupa inaweza kuwa legelege, isiyo imara, kuleta maumivu na kusababisha kushindwa kucheza. Umbo la maungio hayo ya mifupa huweza kuharibika. Umbo la maungio ya mifupa haliwezi kukarabatiwa.

Kwa baadhi ya watu, ugonjwa huu huweza kuharibu idadi kubwa ya mifumo ya mwili, ikiwa ni pamoja na; ngozi, macho, mapafu, moyo na mishipa ya damu.

Chanzo Cha Rheumatoid Arthritis
Rhematoid arthritis hutokea pale kinga za mwili zinapoishambulia synovium – utando wa ngozi laini unaozunguka maungio ya mifupa.

Mashambulio hayo husababisha synovium kuwa nene, ambayo baadaye huharibu gegedu na mfupa ndani ya maungio hayo.

kupata zaidi RA, na hasa wanawake.

Madhara Ya Rheumatoid Arthritis


Rheumatoid arthritis inaongeza hatari ya kupata:
Osteoporosis Rheumatoid nodules Kukauka macho na midomo. Maambukizi. Abnormal body composition. Matatizo ya moyo. Magonjwa ya mapafu. Lymphoma.



Dalili Za Rheumatoid Arthritis


Dalili za rheumatoid arthritis ni pamoja na:

Maumivu, joto na kuvimba kwenye maungio ya mifupa
Kukak**aa kwa maungio hasa asubuhi au baada ya kujipumzisha
Uchovu, homa na kukonda
Wekundu
Kuchechemea
Kubadilika kwa umbo la eneo la maungio ya mifupa
Kupungua kwa kukunjuka kwa maungio
Kupungua damu



Rheumatoid arthritis katika hatua za mwanzo huathiri maungio madogo – hasa maungio ya vidole na mikono na vidole vya miguu na miguu.

Ugonjwa unapoongezeka, huenea kwenye viwiko, magoti, vifundo vya miguu, vifundo vya mikono, nyonga na mabega. Mara nyingi, dalili hutokea kwenye viungo vya pande zote kwa wakati mmoja.

Rheumatoid arthritis inagundulika kwa kuchunguza vitu vingi, vikiwemo:

Eneo la joint na uwiano wake na viungo vingine, na hasa joints za mikono
Kukak**aa kwa joints asubuhi
Vijiuvimbe chini ya ngozi (rheumatoid nodules)
Matokeo ya vipimo vya X-Ray na damu


Tiba Ya Rheumatoid Arthritis
Malengo ya kutibu ugonjwa wa rheumatoid arthritis ni :
Kuondoa maumivu Kuondoa dalili Kuzuia uharibifu wa maungio ya mifupa na viungo vingine Kuboresha utendaji kazi wa viungo Kuondoa madhara ya kudumu

Kufikia malengo haya, dakatari atatoa tiba kulingana na hali ya mgonjwa.

Mazoezi. Mazoezi yana faida sana kwa mgonjwa wa RA na huchukuliwa k**a kipengele cha kwanza katika tiba yake. Mpango wa mazoezi uhusishe mazoezi laini ya aerobics, mazoezi ya kukomaza misuli na mazoezi ya mnyumbuliko.

Virutubishi. Utafiti umeonyesha kuwa matumizi ya tumeric na omega-3 oil yanasaidia kuondoa maumivu ya RA na kukak**aa misuli asubuhi.

Mimi naitwa Dr. elly karibu katika kujifunza na kujua habari zote zinazohusu afya

K**a una swali au unahitaji ushauri na matibabu
namba yangu whatsapp 👉👉+255687347027
eHealthtz "Linda afya Yako"

JE WAJAUA :FAHAMU MAGONJWA YA TISHU UNGANISHI ( CONNECTIVE TISSUES DISEASE)Ugonjwa wa tishu unganishi hurejelea kundi la...
12/02/2023

JE WAJAUA :FAHAMU MAGONJWA YA TISHU UNGANISHI ( CONNECTIVE TISSUES DISEASE)

Ugonjwa wa tishu unganishi hurejelea kundi la matatizo yanayohusisha tishu zenye protini nyingi zinazosaidia viungo na sehemu nyingine za mwili. Mifano ya tishu zinazounganishwa ni mafuta, mfupa, na cartilage. Matatizo haya mara nyingi huhusisha viungo, misuli na ngozi , lakini yanaweza pia kuhusisha viungo vingine na mifumo ya viungo, ikiwa ni pamoja na macho , moyo , mapafu , figo , njia ya utumbo na mishipa ya damu. Kuna shida zaidi ya 200 zinazoathiri kiunganishi. Sababu na dalili maalum hutofautiana na aina tofauti.

Matatizo ya Kurithi ya Tishu Unganishi
Baadhi ya magonjwa ya tishu-unganishi -- mara nyingi huitwa matatizo ya kurithi ya tishu-unganishi (HDCTs) -- ni matokeo ya mabadiliko katika jeni fulani. Mengi ya haya ni nadra sana. Zifuatazo ni baadhi ya zile za kawaida zaidi.

Ugonjwa wa Ehlers-Danlos (EDS). Kwa kweli kundi la zaidi ya matatizo 10, EDS ina sifa ya viungo vinavyonyumbulika kupita kiasi, ngozi iliyonyooka, na ukuaji usio wa kawaida wa tishu za kovu. Dalili zinaweza kuanzia polepole hadi kulemaza. Kulingana na aina maalum ya EDS, dalili zingine zinaweza kujumuisha:

Mgongo uliopinda
Mishipa dhaifu ya damu
Fizi zinazotoka damu
Matatizo na mapafu, vali za moyo , au usagaji chakula
Imependekezwa

Epidermolysis bullosa (EB). Watu walio na ugonjwa wa EB wana ngozi ambayo ni tete sana hivi kwamba inachanika au malengelenge kutokana na nundu kidogo, kujikwaa au hata msuguano wa nguo. Baadhi ya aina za EB zinaweza kuhusisha njia ya usagaji chakula, njia ya upumuaji, misuli, au kibofu . Husababishwa na kasoro za protini kadhaa kwenye ngozi, EB kawaida huonekana wakati wa kuzaliwa.

Ugonjwa wa Marfan . Ugonjwa wa Marfan huathiri mifupa, mishipa, macho , moyo, na mishipa ya damu. Watu walio na ugonjwa wa Marfan huwa warefu na wana mifupa mirefu sana na vidole na vidole vyembamba vya "k**a buibui". Matatizo mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya macho kutokana na uwekaji usio wa kawaida wa lenzi ya jicho na kupanuka kwa aorta ( ateri kubwa zaidi mwilini), ambayo inaweza kusababisha kupasuka mbaya. Ugonjwa wa Marfan husababishwa na mabadiliko katika jeni ambayo inadhibiti muundo wa protini inayoitwa fibrillin-1.

Osteogenesis imperfecta. Osteogenesis imperfecta ni hali ya mifupa brittle, misuli chini ya misuli, na viungo lex na mishipa. Kuna aina kadhaa za hali hii. Dalili maalum hutegemea aina maalum na zinaweza kujumuisha:

Ngozi nyembamba
Mgongo uliopinda
Matatizo ya kupumua
Kupoteza kusikia
Meno ambayo huvunjika kwa urahisi
Ugonjwa hutokea wakati mabadiliko katika jeni mbili zinazohusika na aina ya 1 ya collagen hupunguza kiasi au ubora wa protini. Aina ya 1 collagen ni muhimu kwa muundo wa mfupa na ngozi.

Magonjwa ya Autoimmune
Kwa aina nyingine za ugonjwa wa tishu zinazojumuisha, sababu haijulikani. Katika baadhi ya matukio, watafiti wanaamini kuwa ugonjwa huo unaweza kusababishwa na kitu fulani katika mazingira ya watu ambao wanaweza kuathiriwa na maumbile. Katika magonjwa haya, mfumo wa kinga ya mwili kwa kawaida hutoa kingamwili zinazolenga tishu za mwili kwa mashambulizi.

Magonjwa haya ni pamoja na yafuatayo .

Polymyositis na dermatomyositis. Hizi ni magonjwa mawili yanayohusiana ambayo kuna kuvimba kwa misuli (polymyositis) na ngozi (dermatomyositis). Dalili za magonjwa yote mawili zinaweza kujumuisha:

Udhaifu wa misuli
Uchovu
Ugumu wa kumeza
Upungufu wa pumzi
Homa
Kupungua uzito

Watu wenye dermatomyositis wanaweza pia kuwa na ushiriki wa ngozi karibu na macho na mikono.

Rheumatoid arthritis (RA). Rheumatoid arthritis ni ugonjwa ambao mfumo wa kinga hushambulia utando mwembamba (unaoitwa synovium) unaozunguka viungo, na kusababisha maumivu, ukak**avu, joto na uvimbe wa viungo, na kuvimba kwa mwili mzima. Dalili zingine zinaweza kujumuisha:

Uchovu
Upungufu wa damu
Homa
Kupoteza hamu ya kula
RA inaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa viungo na ulemavu.

Scleroderma. Scleroderma ni neno la kikundi cha magonjwa ambayo husababisha ngozi nene, kubana, mkusanyiko wa tishu zenye kovu, na uharibifu wa chombo. Matatizo haya yapo katika makundi mawili ya jumla: scleroderma ya ndani na sclerosis ya utaratibu .

Scleroderma ya ndani imefungwa kwenye ngozi na, wakati mwingine, misuli iliyo chini yake. Ugonjwa wa sclerosis pia unahusisha mishipa ya damu na viungo vikuu.

Ugonjwa wa Sjögren . Ugonjwa wa Sjögren ni ugonjwa sugu ambao mfumo wa kinga hushambulia tezi zinazotoa unyevu, k**a vile za macho na mdomo. Madhara yanaweza kuanzia kutokuwa na raha kidogo hadi kudhoofisha. Ingawa macho kavu na mdomo ndio dalili kuu za ugonjwa wa Sjögren, watu wengi pia hupata uchovu mwingi na maumivu ya viungo . Hali hiyo pia huongeza hatari ya limfoma na inaweza kusababisha matatizo katika figo , mapafu, mishipa ya damu, mfumo wa usagaji chakula na matatizo ya neva.

Systematic lupus erythematosus. Systematic wa lupus erythematosus (SLE au tu lupus) ni ugonjwa unaojulikana na kuvimba kwa viungo, ngozi, na viungo vya ndani. Dalili zinaweza kujumuisha:

Upele wa umbo la kipepeo kwenye mashavu na daraja la pua
Sensitivity kwa mwanga wa jua
Vidonda vya mdomo
Kupoteza nywele
Maji yanayozunguka moyo na/au mapafu
Matatizo ya figo
Anemia au matatizo mengine ya seli za damu
Matatizo ya kumbukumbu na mkusanyiko au matatizo mengine ya mfumo wa neva

Ugonjwa wa Vasculitis . Vasculitis ni neno la jumla kwa zaidi ya hali 20 tofauti zinazojulikana na kuvimba kwa mishipa ya damu. Hizi zinaweza kuathiri mtiririko wa damu kwa viungo na tishu nyingine za mwili. Vasculitis inaweza kuhusisha yoyote ya mishipa ya damu.

Ugonjwa wa tishu zinazojumuisha. Watu wenye MCTD wana sifa fulani za magonjwa kadhaa, ikiwa ni pamoja na lupus, scleroderma, polymyositis au dermatomyositis, na arthritis ya baridi yabisi. Wakati hii inatokea, mara nyingi madaktari hufanya uchunguzi wa ugonjwa wa mchanganyiko wa tishu.

Ingawa watu wengi walio na ugonjwa wa tishu mchanganyiko wana dalili kidogo, wengine wanaweza kupata matatizo ya kutishia maisha

Mimi naitwa Dr. elly karibu katika kujifunza na kujua habari zote zinazohusu afya

K**a una swali au unahitaji ushauri na matibabu
namba yangu whatsapp 👉👉+255687347027
eHealthtz "Linda afya Yako"

JE WAJUA: UFAHAMU UGONJWA  WA CANDIDIASIS Kuna aina nyingi sana za fungus wanaoishi ndani ya mwili wa binadamu. Moja ya ...
10/02/2023

JE WAJUA: UFAHAMU UGONJWA WA CANDIDIASIS

Kuna aina nyingi sana za fungus wanaoishi ndani ya mwili wa binadamu. Moja ya aina hizo ni fungus aitwaye candida. Huyu ni aina ya yeast apatikanaye kwa kiwango kidogo na ambaye kwa kawaida anaishi kwenye midomo, tumboni au juu ya ngozi bila kuleta madhara. Lakini mazingira yanaweza yakabadilika na kusababisha akaongezeka idadi na kuanza kuleta madhara. Maambukizi haya huitwa candidiasis.
Candida yeast huyu akisambaa kwenye mdomo na koo, anaweza kusababisha maambukizi yanayoitwa thrush (oropharyngeal candidiasis). Hali ni inaonekana sana kwa watoto wachanga na watu wa umri mkubwa ambao wana upungufu wa kinga za mwili. Watu walio kwenye hatari ya kumpata yeast huyu ni: Watu walio kwenye tiba ya kansa Watu wanaotumia antibiotics Watu wenye meno bandia Watu wenye kisukari

Dalili Za Thrush
Vijidoa vyeupe au vya njano juu ya ulimi, lips, fizi, kuta za ndani za mdomo, kuta za ndani za ya mashavu Wekundu kwenye midomo na kooni Kuchanika kwenye kingo za mdomo Maumivu wakati wa kumeza, k**a imesambaa kooni

Vaginal Candidiasis au Vulvovaginal Candidiasis (VVC)


Maambukizi ya yeast ukeni huitwa vaginal candidiasis. Wanawake 3 katika 4 hupata maambukizi haya katika maisha yao. Wanawake wengi hupata maambukizi haya angalau mara mbili. Maambukizi haya hutokea wakati aina hii ya fungus wanapoongezeka na kuzidi idadi. Kuongezeka huku kunatokana na mabadiliko katika uwiano wa uke yanayoweza kusababishwa na ujauzito, kisukari, matumizi ya dawa, vilainishi au kushuka kwa kinga za mwili. Mara chache maambukizi haya hutokana na kujamiiana.
Chanzo Cha Vaginal Candidiasis
Maambikizi ya ugonjwa huu yanasababishwa na yeast wa jamii ya Candida albicans, ingawa jamii nyingine za candida pia zinaweza kuleta maambukizi.
Bakteria na fungus aina ya yeast huishi kwa uwiano fulani katika uke, lakini mvurugiko wa uwiano huu dhalili unaweza kuleta mambukizi.
Kwa kawaida bakteria aitwaye Lactobacillus huweka mazingira ambayo huzuia mwongezeko wa yeast, lakini yeast akiweza kuyavuruga, anaweza kuongezeka na kuleta maambukizi. Maambukizi haya huonekana zaidi kwa wanawake wanaoshiriki sana ngono.

Mazingira yanayosababisha kuongezeka kwa yeast ni: Matumizi ya antibiotics Ujauzito Kisukari kisichodhibitiwa Upugufu wa kinga za mwili
Shughuli yo yote inayoleta mabadiliko kwenye mazingira ya uke, pamoja na kujiosha (douching), yanaweza kuchangia maambukizi ya yeast. Lishe duni na kukosa usingizi wa kutosha pia vinaweza kuwa na mchango.

Dalili Za Candidiasis Kuwashwa ukeni Wekundu au kuvimba ukeni na nje ya uke (v***a) Maumivu wakati wa haja ndogo Maumivu wakati wa tendo la ndoa Uchafu mweupe, mzito k**a jibini


Tiba Ya Candidiasis


Maambukizi ya yeast yanaweza kutibiwa kwa kutumia antifungal creams au vidonge.

Mimi naitwa Dr. elly karibu katika kujifunza na kujua habari zote zinazohusu afya

K**a una swali au unahitaji ushauri na matibabu
namba yangu whatsapp 👉👉+255687347027
eHealthtz "Linda afya Yako"

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when eHealthtz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram