19/04/2021
TATIZO LA NGUVU ZA KIUME :
Leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote. Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake.
Kuna sababu zaidi ya 200 zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume. Mtu aweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo?
Nguvu za kiume ni nini?
Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo la lenyewe.
Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume?
Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.
Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.
Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayopubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k.
Nini maana ya kupungua nguvu za kiume?
Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri jinsi ipasavyo na inavyotakiwa. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una