Kliniki Ya Baba, Mama Na Mtoto: Rch kiganjani

Kliniki  Ya Baba, Mama Na Mtoto: Rch kiganjani Huu ni ukurasa kuhusu afya .Tutatoa mafunzo huu ya afya ya uzazi na mada nyingine za afya. Lengo le

Kwa kuku safi wa nyama (stopper) wanapatikana Kila wiki ya tatu ya mwezi kuanzia tarehe 20.0652700929
10/05/2026

Kwa kuku safi wa nyama (stopper) wanapatikana Kila wiki ya tatu ya mwezi kuanzia tarehe 20.
0652700929

25/04/2026

Je! Kila mwanamke mjamzito lazima awe na cravings (hamu kubwa ya kula au kufanya kitu kimoja kwa kujirudiarudia) mfano kula udongo

Dalili za mwanzo za kujifungua;2. Kushuka kwa mtoto: Utaona mgandamizo kwenye kinena ni mkubwa ila unapumua kwa urahisi.
01/04/2026

Dalili za mwanzo za kujifungua;
2. Kushuka kwa mtoto:
Utaona mgandamizo kwenye kinena ni mkubwa ila unapumua kwa urahisi.

Energy burst:Mama mjamzito anapokaribia kujifungua utaona anakuww na Ari na nguvu ya kufanya kazi nyingi sana.Hata k**a ...
21/03/2026

Energy burst:

Mama mjamzito anapokaribia kujifungua utaona anakuww na Ari na nguvu ya kufanya kazi nyingi sana.Hata k**a kipindi Cha ujauzito alikuwa mtu wa kulala tu, utaona anaamka mapema na kujishughulisha.
Hii hutokea kwa Amina mama wengi na miongoni mwa dalili za kujifungua.

K**a unajua dalili nyingine ya kukaribia kujifungua, andika kwenye comment section.

Sio Kila uvimbe kwenye via vya uzazi unatibiwa kwa upasuaji.
15/10/2025

Sio Kila uvimbe kwenye via vya uzazi unatibiwa kwa upasuaji.

08/05/2025

Baada ya kujifungua kwa upasuaji, miezi mitatu baadae akajikuta ni mjamzito tena. Ungelikuwa ni wewe ungefanyaje?

28/03/2025

Tafadhali,pendekeza mada yoyote ya kiafya, tutaizungumzia kwa kina.
(Saa 24)

28/03/2025

Ni muda Sasa wa kuanzia tena kufahamishana habari za afya.

Sauti ya mtoto aliye tumboni: Mama kunywa maji ya kutosha, naona kiu
27/01/2025

Sauti ya mtoto aliye tumboni: Mama kunywa maji ya kutosha, naona kiu

25/01/2025

UMUHIMU wa MAJI KIPINDI Cha UJAUZITO.

Maji ni kimiminika muhimu sana kwenye mwili wa binadamu. Kazi nyingi zinazofanyika mwilini huhitaji maji ili zikamilike Mfano; Mmeng'enyo wa chakula, usafirishaji wa chakula kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, na kazi nyingine nyingi.
Kwa kifupi tunaweza kusema bila maji, mwanadamu hana kitu (amekufa).

Ikiwa maji yana kazi nyingi hivyo kwenye mwili wa mtu asiye na UJAUZITO, vipi kwa mama mjamzito? Na kwa Nini mahitaji ya maji kwa mama mjamzito yanaongezeka?

Baki nami tulidadavue hilo swala mtambuka.

Awali ya yote tunapaswa kujua kuwa tunapata maji(maji yanaingia mwilini mwetu) kwa njia mbalimbali, k**a;
1. Vyakula Mfano, Tikiti maji, Madafu,
2. Kunywa maji
3. Vinywaji Mfano,soda, juisi, n.k
4. Kuongezewa maji ukiwa mgonjwa n.k
5. Maji ya ndani ya miili yetu

Pia maji hayo yanatoka mwilini mwetu kwa njia tofauti tofauti ikiwemo kwa njia ya mkojo, jasho, kupumua (mdomoni au puani) na njia ya haha kubwa.
Kwa kawaidi miili yetu inaweza kubalansi kiwango Cha maji kinachoingia na kinachotoka.

Kipindi cha UJAUZITO Huwa Kuna mabadiliki mengi ya kimwili. Mfano wa mabiliko hayo ni uwepo wa kondo la nyuma, kuongezewa kwa ukubwa wa mfuko wa mimba, mabadiliki ya kwenye Figo na mengine mengi.

Kiwango Cha damu (blood plasma) huongezeka taratibu kuanzia wiki ya sita Hadi ya nane na kufikia kiwango chake Cha juu kwenye wiki ya 34. Ikiwa sehemu kubwa ya damu ni maji (83%), hivyo mama mjamzito ni vyema akaongeza unywaji wa maji ili kufidia ongezeko hilo.

Vilevile kiwango Cha upumuaji huongezeka kwa 40%, kasi ya kutokwa na jasho huongezeka, urination rate pia huongezeka ; hayo oyte hupoeteza maji kwa haraka sana,basi mama mjamzito anapaswa kunywa maji ya kutosha angalau glass 6 Hadi 8 kwa siku Moja ili kufidia upotevu huu wa maji.

Pia mahitaji ya virutubisho huongezeka kipindi cha UJAUZITO. Ili kusafirisha virutubisho hivyo,maji yanahitajika.

Mabadiliko hayo yote husababisha ongezeko la mahitaji ya maji mwilini.

K**a hutopata maji ya kutosha kipindi cha UJAUZITO unaweza kusababisha mtoto kuzaliww akiwa na uzito mdogo (chini ya 2•5Kg). Pia Kuna tafiti huko California ilionesha kuwa ukinywa maji mengi unasaidia kuongeza kiwango Cha maji ya uzazi(Amniotic fluid).

American institute of medicine wanapendekeza mama mjamzito anywe angalau 2.7L kwa siku huku shirika la afya duniani linapendekeza 4.8L kwa siku.

Tuhitimishe kwa kusema, maji ni muhimu sana kwenye kipindi cha UJAUZITO . Akina mama wasizembee kunywa maji au kula vyakula vyenye maji mengi.

Sauti ya mtoto aliye tumboni: "Mama kunywa maji ya kutosha, naona kiu."

Imeandaliwa na;
Godlove Ituga
0652700929

15/12/2024

Address

Virtual
Dar Es Salaam
255

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kliniki Ya Baba, Mama Na Mtoto: Rch kiganjani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Kliniki Ya Baba, Mama Na Mtoto: Rch kiganjani:

Share