20/04/2021
Tatizo hili husimama lenyewe k**a ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili k**a mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba.
Kusimama kwake k**a ugonjwa ni pale yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu.
Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.
Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa k**e na wa kiume, watoto wachanga wa k**e na wa kiume.
Chanzo cha tatizo
Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya homoni mwilini.
Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya ‘prolactine’.
Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.
Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni ‘Prolactin’, Estrogen’ na Progesterone.
Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa k**a Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili.
Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu na wasiwasi au shauku f’lani,
mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.