25/07/2025
Hongera kwa kufika hatua hii muhimu ya kuwa mama!
Hapa kuna KUCHEKA, KULIA, KUKESHA, MAUMIVU... n.k
Baada ya kujifungua, majukumu yako yanabadilika sana—kulea mtoto mchanga,
..kujitunza kimwili na kiakili, na kuzoea hali mpya ya maisha.
Kuzungumza kuhusu ugumu wa safari ya uzazi hakukufanyi kuwa mama dhaifu, wala hakumaanishi kuwa hutambui uzuri wa safari hii.
Kushiriki changamoto zako ni muhimu kwa afya bora ya akili na kupunguza msongo wa mawazo.
Je, umepitia changamoto yoyote katika safari yako ya uzazi?
Tufahamishe kwenye maoni au tag mama mwingine mzuri anayestahili kusikia haya.
Pamoja tunaweza kujenga jamii inayoungana na kupeana nguvu! 🌸❤️