03/04/2023
Upungugu wa nguvu za kiume, unaweza kusababishwa na sababu mbalimbali za kimwili na kisaikolojia. Miongoni mwazo ni uvutaji wa sigara. Uvutaji sigara unaweza kuharibu mishipa yako ya damu, na hivyo kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwa sababu ili uume usimike barabara inahitahitajika usambazaji bora wa damu wa ateri kwenye uume. Upungufu wa nguvu za kiume
Uvutaji sigara huharibu mzunguko wa damu kwa njia nyingi, na kusababisha shida nyingi za kiafya k**a vile ugonjwa wa moyo, mshtuko wa moyo na kiharusi. Uvutaji wa sigara unaua kabisa nguvu za kiume.
Kusimama kwa uume kunawezekana tu wakati mishipa ya damu kwenye uume inapoongezeka na kujaa damu. Uvutaji sigara huvuruga mishipa ya damu katika eneo hilo la mwili, kumaanisha kitendo hicho hakiwezi kutokea kila mara.
Hata kwa wanaume wenye umri mdogo k**a miaka 20 sigara inaweza kabisa kuteketeza nguvu za kiume, ikiwa ni pamoja na kupunguza sana hamu ya tendo la ndoa.
Ugumba
Matumizi ya tumbaku yanaweza kuathiri vibaya uzazi kwa wanaume na wanawake. Wavutaji sigara wa kiume na wa k**e wana takriban mara mbili ya kiwango cha ugumba kinachopatikana kwa wasiovuta.
Uvutaji sigara unahusishwa na changamoto za uzazi kwa njia kadhaa. Uvutaji sigara huharibu DNA katika mayai na manii, jambo ambalo linaweza kusababisha matatizo ya uzazi. Aidha, wanawake wanaovuta sigara wanaweza pia kuwa na dirisha fupi la kupata mimba kwa sababu kemikali zinazopatikana katika bidhaa za tumbaku, ikiwa ni pamoja na nikotini, sianidi na monoksidi kaboni, huongeza kasi ya kupoteza mayai na kusababisha wavutaji kupata hedhi mapema kuliko wasiovuta. Upungufu wa nguvu za kiume uliotajwa hapo juu unaweza pia kuchangia kushindwa kushika mimba. KOSA KUBWA WANALOFANYA WANAUME WENGI
Wanaume wengi wanapopungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, na siyo kutibu chanzo cha tatizo. Hili ni KOSA KUBWA sana!
Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu eneo au kitu gani mwilini. Kwa njia hiyo, utamaliza miaka hata zaidi ya 100 na hata miaka elfu moja na hautapona!
Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe kuanzia chanzo cha tatizo; kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung'olewe kwanza!
Mathalani, k**a tatizo ni la homoni ijulikane kwanza; k**a ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kisha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo. Hayo ndiyo matibabu, na si vinginevyo.