13/06/2022
*Lesson 3; Banda bora la kuku*
Banda bora ni banda ambalo linakidhi mahitaji ya kuku wako na liendane na idadi ya kuku unaofuga.
Umuhimu wa banda bora;
Banda bora linasaidia kupunguza changamoto za magonjwa
Sifa za banda bora.
I. Lijengwe sehemu isoyotuama maji
II. Likinzane na uelekeo wa upepo na mvua
III. Liruhusu mzunguko wa hewa
IV. Liwakinge kuku wako dhidi ya baridi
V. Liwe na vichja kwaajili ya kupumzika, kufanya mazoezi na kulala, pia Liwe na viota vya kutagia ambavyo huwekwa kuku wakifikisha miezi 3
VI. Liwe rahisi kusafishika
VII. Liendane na idadi ya kuku bandani
Hapa sasa watu wengi hua wanafeli na kujisababishia changamoto za magonjwa, kudonoana na kula mayai.
Kuku anahitaji sehemu ya kutosha ili aweze kuwa huru na kufanya mazoezi ndio maana wanaofuga huria au nusu ndani nusu nje wanapata matokeo mazuri.
Kila aina ya kuku anahitaji nafasi yake.
1m square inahitaji kuku chotara 4/5
1m square inahitaji kuku wa mayai 6/8
1m square inahitaji kuku wa kienyeji/nyama 8.
Mfano unataka kujenga banda la kuku chotara 100, unachukua 100÷4=25m square au 100÷5=20m square, sasa hii 25/20m square ndio ukubwa wa banda. 25=6.25x4 na 20=5x4.
Ukizingatia vipimo utapunguza changamoto.
*UMUHIMU WA VIOTA*
Viota ni mahali ambapo kuku hutaga mayai, kuatamia na kuangua vifaranga. Hii inamaanisha kuwa viota ni sehemu muhimu sana ya kuzingatia ili kuweza kupata mayai mengi yaliyo salama pamoja na vifaranga.
_Aina za viota_
Kuna makundi mawili ya viota vinavyotumiwa na kuku pamoja na ndege wengine wafugwao.
1. Kiota kilicho tengenezwa na kuku mwenyewe
Hii ni aina ya viota ambavyo kuku huchagua mahali pa kutaga na kuhifadhi mayai. Inaweza kuwa mahali popote ambapo kuku ataona mayai hayataweza kudhurika au kuonekana. Kwa mfano, vichakani, stoo au kona yenye giza.
Njia hii si nzuri kwani husababisha upotevu wa kuku na uharibifu wa mayai.
Kwa kutagia stoo au sehemu iliyojificha ya ndani, japokua ni sehemu salama ambayo haiwezi kufikiwa kirahisi na wezi au wanyama, maya