
18/05/2024
MAMA MJAMZITO MWENYE BAWASIRI ANA KUTANA NA CHANGAMOTO KADHAA AMBAZO ZINAWEZA KUA NGUMU NA KULETA USUMBUFU KATIKA KIPINDI CHAKE CHA UJAUZITO HIZI NI BAADHI YA CHANGAMTO
1.MAUMIVU NA USUMBUFU
bawasiri inaweza kusababisha maumivu makali haswa wakati wa kujisaidia haja kubwa hii inaweza kuwa tatizo kubwa kwa mama mjamzito kwani inachangiia hali ya kutojisikia vizuri na stress
2.KUTOKWA NA DAMU
bawasiri mara nyingi husababisha kutowa na damu wakati wa kujisaidia hii inaweza kuwa ya kutisha na kusababisha wasi wasi kwa mama mjamzito kuhusu afya yake na ya mtoto
3.KUCHUBUKA NA KUWASHWA
ngozi inayo zunguka bawasiri ina weza kuwashwa na kuchubuka ikisababisha usumbufu zaid na kuwa vigumu kupata usingizi mzuri au kupumzika
4.KUHISI KUUNGUA
wanawake waja wazito wanaweza kuhisi hali ya kuungua sehemu ya mkundu kutokana na bawasiri ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na ongezeko la shinikizo kwenye maeneo ya chini ya mwili wakati wa ujauzito
5.VIZUIZI VYA DAWA
matibabu ya bawasiri yanaweza kua changamoto kwani baadhi ya dawa zinazo tumika kawaida haziwezi kutumiwa wakai wa ujauzito kutokana na hatari kwa mtoto hii inamaanisha kuwa mama mjamzito anaweza kuwa na chaguo chache za matibabu
6.KUJIHISI KUKOSA RAHA
kutokana na maumivu na usumbufu wa bawasri mama mjamzito anaweza kujikuta akikosa raha na kuathiri hali yake ya kisaikolojia ikiwema stressna wasi wasi
7.KUJIKINGA NA KUONGEZEKA KWA TATIZO
wajawazito wana kumbana na changamoto ya kuhakikisha bawasiri haizidi kuwa mbaya kwa mfano kupitia mabadiliko ya lishe kuongeza ulaji wa nyuzi nyuzi na kuhakikisha wanapata maji ya kutosha pia wanapaswa kuepuka kukaa na kusimama kwa muda mrefu na kufanya mazoezi mepesi k**a kutembea
KUPITIA UANGALIZI MZURI NA USHAURI KUTOKA KWA MTAALAMU WA AFYA MAMA MJAMZITO ANAWEZA KUPATA MSAADA WA KUPUNGUZA CHANGAMOTO HIZI NA KUHAKIKISHA ANAPATA UJAUZITO WENYE AFYA SALAMA
KWA MATIBABU ZAIDI WASILIANA NA
DR SIMU NAMBA 0788 742 203
LIFE NATURAL TUPO KWA AJILI YAKO ASANTENI