Chakula & afya na lishe

  • Home
  • Chakula & afya na lishe

Chakula & afya na lishe Sayansi ya vyakula 🔬
Ulaji Bora Kwa afya njema🥗
"Simplified food science for a healthier you." Follow us for updates
📞 0693405161

Usidanganywe na Rangi: Ukweli Kuhusu matikiti yaliyotiwa Rangi BandiaJe, umewahi kujiuliza k**a tikitimaji unalonunua so...
17/05/2025

Usidanganywe na Rangi: Ukweli Kuhusu matikiti yaliyotiwa Rangi Bandia
Je, umewahi kujiuliza k**a tikitimaji unalonunua sokoni ni salama kweli kuliwa? Linaonekana tamu na nyekundu, lakini je, hiyo rangi ni ya asili au imeongezwa kwa kemikali.

Uchakachuaji wa tikitimaji uhusisha vitendo vya kuongeza au kubadilisha sifa za tikitimaji ili lionekane bora zaidi sokoni. Baadhi ya wauzaji huongeza rangi, maji au kemikali za kuharakisha uivaji kwa lengo la kuvutia wanunuzi au kuongeza faida.

Erythrose (E127)
Ni rangi ya bandia ambayo huwekwa kwenye matikiti ili yaonekane na rangi nyekundu zaidi, hata k**a halijaiva vizuri. Rangi hii ni aina ya kemikali ambayo hapo kabla ilitumika kwenye baadhi ya vipodozi ,vyakula na dawa, lakini si salama kwa matumizi kwenye vyakula na matunda yakiwemo matikiti kwani ilipigwa marufiku na mamlaka ya chakula na dawa marekani ( FDA ) January 2025 . Hii ni kwasababu ilionekana kusababisha madhara k**a matatizo ya homoni ,msisimko na hata kansa iwapo itatumika kwa kiwango kikubwa.

SULUHISHO
Tumia njia hizi Mbili kujua
I)Tumia pamba au kitambaa cheupe . Kata tikitimaji na upake sehemu nyekundu kwa kutumia pamba nyeupe au kitambaa . Ikiwa pamba itapata rangi, linaweza kuwa limeongezwa kemikali.k**a rangi itaacha doa, hilo tikitimaji si salama.
II) Angalia rangi ya juisi ya tikitimaji: ikiwa ni nyekundu sana au inaacha mabaki mekundu, kuna uwezekano mkubwa wa kuwa limechakachuliwa.

# Afya yako ni muhimu usidanganywe na rangi ya tikitimaji , Chagua tikitimaji la asili #

➡️ TIPS 5 ZA SIKU YA UNENE DUNIANI -  WORLD's OBESITY DAY TIPS .Kila mwaka, tarehe 4 Machi ni Siku ya Watu Wenye Uzito M...
04/03/2025

➡️ TIPS 5 ZA SIKU YA UNENE DUNIANI - WORLD's OBESITY DAY TIPS .
Kila mwaka, tarehe 4 Machi ni Siku ya Watu Wenye Uzito Mkubwa Duniani (overweight and obese). Hivyo fahamu vidokezo 5 virahisi ( tips) vya kudhibiti kiasi Cha chakula tunachokula ( portion Sizes) ili kuwa na uzito sahihi na kuepukana na unene

Ili kuweza kupunguza uzito na kuwa na uzito sahihi ( weight loss and weight maintance), kiasi Cha chakula ni Moja kati ya mambo yanayo chukua nafasi kubwa zaidi. Hii ni Kwa sababu,safari ya kupunguza uzito huwa ngumu sana endapo mtu hufanya mazoezi pekee bila kuzingatia aina ya vyakula anachokula ,kiasi Cha chakula na wakati anapokula.

✔️Vifuatavyo ni vidokezo 5 vya kudhibiti kiasi cha chakula ( portion size ) ili kupunguza uzito/ unene:

1. Sikiliza mwili wako. Jifunze kutofautisha kati ya njaa na hamu ya kula. Kumbuka kuacha kula unaposhiba na Kuwa na ratiba maalumu ya muda wa kula pamoja na orodha ya manunuzi ya vyakula husaidia kuzuia kula ovyo na kupita kiasi.

2. Tumia sahani ndogo.Hii hudanganya akili yako kufikiri una kiasi kikubwa, hivyo husaidia kula kidogo.Tukiacha sababu za vinasaba, sababu za kimetaboliki, matatizo wakati wa ujauzito (fetal programming ), chanzo kikubwa cha uzito mkubwa kinachopelekea unene ni ulaji mkubwa wa vyakula vinavyoupa mwili nguvu nyingi kuliko matumizi ya nguvu zinazohitajika mwilini

3. Punguza ulaji wa wa vyakula vyenye mafuta mengi au sukari pia epuka unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi na vyakula visivyo na lishe( junk foods ) kwani huupa mwili nguvu kubwa zaidi kuliko mahitaji . Pendelea kiasi kikubwa cha mboga, matunda na nafaka zisizokobolewa.

4. Kunywa maji kabla ya kula. Hii hutoa hisia ya kushiba, hivyo kupunguza ulaji wa chakula kwa ujumla. Kwa sababu wakati mwingine miili yetu huchanganya kiu na njaa. Kuwaa na maji ya kutosha mwilini kunaweza kuzuia kula kupita kiasi kwani utambuzi wa ishara za njaa hupungua.

5. Epuka vikengeusha ( distarbunces and destructions ) wakati wa kula.Kula mbele ya TV, kompyuta, kula ukiwa umesimama au huku ukitumia simu kunaweza kukufanya ule kupita kiasi bila kujua na kupelekea kuongezeka uzito .

✔️Kutokana na athari nyingi zinazotokana na unene k**a vile utasa, muda mfupi wa kuishi, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ,magonjwa ya kisukari pamoja na mengine mengi, ni muhimu kubadili mfumo wa ulaji kwa kuepuka / Kupunguza mambo yote yanayosababisha unene.

# changing system for healthier lives #

➡️ KWANINI NI MUHIMU KULA CHIPS PAMOJA NA  KABICHI ?Je, umewahi kujiuliza kwa nini kwenye migahawa ya chakula maranyingi...
01/03/2025

➡️ KWANINI NI MUHIMU KULA CHIPS PAMOJA NA KABICHI ?
Je, umewahi kujiuliza kwa nini kwenye migahawa ya chakula maranyingi chipsi huandaliwa pamoja na kabichi 🤔 ? Zijue sababa kuu 3 zinazopelekea madai hayo

Kabichi ni mboga yenye kalori chache na virutubisho vingi muhimu k**a vitamini C, K, antioxidants( glucosinolates), madini (k**a potasiamu, manganisi), na nyuzinyuzi. Hii huifanya kuwa na faida nyingi kiafya k**a vile kutoa kinga dhidi ya kansa, kuiimarisha kinga ya mwili, kusaidia kupunguza uzito, na kudhibiti shinikizo la damu.

✔️ Zifuatazo ni sababu kuu 3 zinazopelekea kabichi kushauriwa kuliwa na vyakula vya kukaanga k**a vile chips .
-(I) Kabichi za kijani Zina nyuzinyuzi nyingi wastani wa 3 g/100g, juu ya wastani wa mboga nyingine za majani ambazo huwa na wastani wa 2.43g/100g za nyuzinyuzi. Nyuzinyuzi hizi husaidia usagaji mzuri wa chakula, hasa baada ya kula vyakula vyenye mafuta mengi k**a chips ambazo huwa na mmeng'enyo mgumu.

- (II) kabichi ina phytosterols ambazo huzuia ufyonzwaji wa cholesterol kwenye utumbo mdogo. Chipsi zina mafuta mengi ambayo hupelekea , kiwango cha cholesterol mbaya kwenye damu kupanda. Uwepo wa phytosterols hupunguza kiwango cha cholesterol mbaya kwenye damu Kwa kuzuia ufyonzwaji wake. Hii husaidia kupunguza madhara ya mafuta mengi kutoka kwenye chipsi.

- (III) Kabichi zina kalori chache sana (25-31cal/100g), hivyo zinapoliwa na chipsi ambazo huwa na kalori nyingi (536cal/100g) husaidia kupunguza jumla ya kalori unazotumia, hivyo kupunguza hatari ya kupata uzito mkubwa.

✔️ Ni muhimu kuzingatia uandaaji sahihi wa kabichi kwa kuzingatia usafi . kuongeza viungo na mboga nyingine k**a vile karoti na nyanya huongeza ladha na virutubisho zaidi. Vilevile kuepuka kuongeza mafuta ya kupikia ni Bora Kwa afya njema zaidi .

By Thomass Arnold

➡️FAHAMU USIYOJUA KUHUSU MAJI YA KWENYE CHUPA ZA PLASTICS .°Tarehe ya mwisho ya matumizi kwenye chupa ya maji ( expire d...
08/12/2024

➡️FAHAMU USIYOJUA KUHUSU MAJI YA KWENYE CHUPA ZA PLASTICS .
°Tarehe ya mwisho ya matumizi kwenye chupa ya maji ( expire date ) ni kwa chupa, sio maji. kwa kawaida Maji yenyewe hua hayaharibiki, lakini chupa ya plastiki iliyobeba maji ndani yake uharibika baada ya muda kutokana na kuvuja Kwa kemikali za chupa ndani ya maji yaliyondani.

°Shirika la Chakula na Dawa duniani (FDA) halilazimishi wazalishaji wa maji ya chupa kuweka tarehe ya kumalizika matumizi kwake kwani, ikiwa yamehifadhiwa vizuri na hayajafunguliwa, yanaweza kudumu kwa muda mrefu. Hata hivyo, baadhi ya kampuni huweka tarehe ya matumizi bora kati ya mwaka 1 - 2.

°Chupa za maji za plastiki za kawaida hutengenezwa kwa polyethylene terephthalate (PET), ambayo Katika joto au mwanga wa jua inaweza kutoka na kuingia ndani ya maji .

° uhifadhi wa Maji ya chupa za plastiki Katika Joto Kali huweza kupelekea Maji kubadilika rangi na kuwa ya kijani kutokana na kuota Kwa algae ( mwani) au baadhi ya bacteria ambao hubaki Kwa kiasi kidogo Baada ya Maji kutibiwa .

°Uhifadhi mbaya wa Maji ya chupa za plastiki hupelekea kemikali ,metals k**a antimony na vipande vidogo vya plastiki ( microplasticts ) ambavyo havionekan Kwa macho kuingia kwenye maji Ambavyo hupelekea athari Kwa afya ya mtumiaji k**a vile matatizo ya ini na utumbo, matatizo ya upumuaji ,homoni n.k

°Uhifadhi wa maji karibu na kemikali (volatile solvents ) K**a vile petroli, thinners za rangi, na bidhaa za kusafisha zinaweza kuingia kwenye maji yaliyo kwenye chupa za plastiki na kuchafua maji.

✔️ SULUHISHO
Epuka kuweka chupa za plastiki kwenye sehemu zenye Joto Kali au mwanga wa jua pia epuka kuweka chupa zenye Maji karibu na kemikali k**a vile petroli ,mafuta na bidhaa mbalimbali za usafi .

Kupunguza matumizi ya chupa za plastiki na kutumia chupa za maji zinazoweza kutumika tena zilizotengenezwa kwa kioo au chuma ni Bora zaidi Kwa Afya. Pia kutotumia chupa za plastiki zilizoharibika kwa namna yoyote ile husaidia Kupunguza athari zaidi.

By Thomass Arnold

➡️ FAHAMU ZAIDI KUHUSU MBOGA ZA CHAINIZI & SPINACH Kumekuwa na mitazamo tofauti Katika jamii  kuhusu mboga za spinach & ...
03/11/2024

➡️ FAHAMU ZAIDI KUHUSU MBOGA ZA CHAINIZI & SPINACH
Kumekuwa na mitazamo tofauti Katika jamii kuhusu mboga za spinach & chainizi, ambapo baadhi wanaziona k**a mboga zenye faida nyingi kiafya, huku baadhi kuziona kuwa na madhara kiafya hasa Katika katika suala la ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume.

✔️Spinach na chainizi ni mboga za majani zinazopatikana Katika kundi Moja la mboga linaloitwa Brassica ambalo linahusisha pia mboga nyingine k**a kabichi na broccoli.Chainizi na spinach Zina virutubisho muhimu k**a vitamini A, C, E, K, na B, antioxidants pamoja na madini k**a chuma, kalsiamu, magnesiamu, na potasiamu ambayo husaidia kuboresha afya ya macho , ngozi na kuzuia uharibifu wa seli mwilini pia vinaimarisha mifupa na kupunguza hatari ya kuvunjika.
Kiwango Cha spinach kinachoshauriwa Kwa siku ni takriban nusu kikombe ikiwa imepikwa

❌ MADHARA YA ULAJI WAKE KUPITA KIASI
•Spinachi ina phytoestrogens kwa kiwango kidogo, inayofanana na homoni ya estrogen inayodhibiti mfumo wa uzazi wa k**e. Tafiti zinaonyesha kuwa kiwango hiki kidogo hakina athari kwenye utasa kwa wanaume, ingawa dozi kubwa za phytoestrogens zimeonekana kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume kwa panya dume wazima.
•Asidi ya oxaliki kwenye spinachi inaweza kuungana na kalsiamu, magnesiamu, na zinki, na kufanya mwili kushindwa kufyonza madini haya kwa urahisi.
•Spinachi ina nyuzi nyingi ambazo zinaweza kusababisha gesi, kuvimbiwa, maumivu ya tumbo, kuharisha, na wakati mwingine homa.
•Spinachi ina vitamini K Kwa wingi , ambayo inaweza kuingiliana na baadhi ya dawa za kupunguza kuganda kwa damu na kusababisha kuganda kwa damu.
•Spinachi ina purini, ambazo,huweza kupelekea matatizo ya Figo na maumi ya viungo Vya mwili.

✔️ SULUHISHO
•Unaweza kupunguza kiwango cha asidi ya oxaliki kwenye spinachi kwa kupika au kuiloweka. Kuchemsha spinachi kwa dakika 12–15 kunaweza kupunguza asidi ya oxaliki kwa 30–87%. Epuka kutumia maji yaliyopikia , kwani asidi ya oxalic hubaki zaidi kwenye maji.

•Kula spinachi pamoja na vyakula vyenye kalsiamu (k**a maziwa) kunaweza kusaidia kubadilisha asidi ya oxalic, kwani kalsiamu inashikilia oxalate .

# Tafiti zinaonyesh Chainizi haina kemikali sumu zinazoathiri ufanisi wa wanaume. ingawa tatizo hilo Iinawezekana kutokana na mabaki ya aina ya dawa zinazotumika katika kuzikuza na kuzilinda dhidi ya wadudu . #

Tujifunze pamoja kupitia maswali na maoni Yako .

By Thomass Arnold

➡️ FAHAMU KUHUSU SOLANINE ,SUMU INAYOPATIKANA KWENYE  VIAZI  VYA KIJANI.Solanine ni kemikali yenye sumu inayopatikana kw...
26/10/2024

➡️ FAHAMU KUHUSU SOLANINE ,SUMU INAYOPATIKANA KWENYE VIAZI VYA KIJANI.
Solanine ni kemikali yenye sumu inayopatikana kwa asili katika baadhi ya mimea, k**a viazi, nyanya, na biringanya. Kwa kawaida solanine husaidia mimea kujikinga na wadudu na magonjwa

RANGI YA KIJANI ,MACHIPUKIZI NA LADHA CHUNGU ni viashiria Vya uwepo wa kiwango kikubwaa Cha solanine kweny viazi. Sehemu za viazi zenye mashimo huwa na kiwango kikubwa cha solanine.

Viazi vinavyoanza kuchipua au kuwa na rangi ya kijani huzalisha kemikali ya solanine.kwa Kawaida, viazi ambavyo havijachipua huwa na kiwango kidogo cha solanine kwenye maganda tu, lakini baada ya muda kemikali hii husambaa hadi ndani. Mwanga huwezesha viazi kuwa na rangi ya kijani na kuongeza kiwango cha solanine. Uharibifu k**a kupasuka kwa viazi huchangia kuongezeka kwa kemikali hii.

❌ Madhara
Kula kiasi kikubwa cha solanine kunaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika, maumivu ya tumbo, na kuhara, pamoja na changamoto katik mfumo wa fahamu k**a maumivu ya kichwa na kizunguzungu.
Kulingana na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA),Kiwango cha solanine hakitakiwi kuzidi 20 mg kwa kila gramu 100 za viazi ( 0.2 mg/g ), kwani dalili za sumu ya solanine huanza kuonekana Baada ya kiwango hichoo kuzidi .

✔️ SULUHISHO
Kuhifadhi viazi kwenye sehemu yenye giza na isiyo na joto kali husaidia kupunguza uzalishaji wa solanine. Kemikali hii ya sumu haiwezi kuondolewa kwa njia ya kupika, na hata kumenya viazi vilivyoota au kuwa na rangi ya kijani hakuhakikishi kuondoa solanine yote, kwa kuwa inaweza kuwa tayari imepenya ndani ya viazi. Kwa hiyo, ni vyema kutupa viazi vilivyo na dalili hizi ili kuepuka madhara. Pia, si salama kuwalisha wanyama maganda ya viazi vya aina hii, kwani inaweza kuwadhuru .

By Thomass Arnold

➡️ FAHAMU KUHUSU LECTIN ,SUMU ILIYOPO KWENYE MAHARAGE .Hemagglutinins (Lectin) ni protini za asili zinazopatikana kwenye...
19/10/2024

➡️ FAHAMU KUHUSU LECTIN ,SUMU ILIYOPO KWENYE MAHARAGE .
Hemagglutinins (Lectin) ni protini za asili zinazopatikana kwenye mimea, na zinapatikana katika vyakula vingi kwa viwango vidogo, lakini kwa viwango vya juu katika mbegu, nafaka, na jamii ya kunde k**a maharagwe na mbaazi. Viwango Vya juu zaidi Vya lectin hupatikana kweny maharage mekundu ya Figo . Piaa Maharagwe mabichi yana kiwango cha juu cha lectin.

❌ Lectin zikiliwa bila kupikwa vizuri, zinaweza kuleta madhara k**a kuharibu usagaji chakula , Maumivu ya tumbo,Kuharibu utando wa tumbo na kupelekea vidonda Vya tumbo vile vile uhaaribu mfumo wa mgawanyiko wa seli nyekundu na seli nyeupe Za damu

✔️ SULUHISHO
Ili kupunguza au kuondoa sumu hizi, ni muhimu kuzingatia uandaaji sahihi wa maharage. Kuosha vizuri na kuloweka maharage kwenye maji kwa masaa 8 hadi 12 kabla ya kupik husaidia kupunguza kiwango cha lectin. Kumwaga maji yaliyoloweka na kuchemsh Kwa muda mrefu Katika Joto la kutosha na kwenye maji safi huondoa lectin Kwa kiwango kikubwaa .

Pia Kuloweka maharage ,kubadilisha maji na Kupika maharage kwa muda mrefu hadi yawe laini husaidia kuondoa oligosaccharides, aina ya wanga ambaz mwili unashindwa kuvunja kwa urahisi, na hivyo hupunguza gesi tumboni hivyo hupunguza matatizo ya gesi na kupumua kwa harufu mbaya.

By Thomass Arnold

➡️ JE KUNA  MADHARA GANI UKINYWA MAJI MENGI KUPITA KIASI ?Maji  yanachukua takriban 50% hadi 70% ya uzito wa mwili wa bi...
14/10/2024

➡️ JE KUNA MADHARA GANI UKINYWA MAJI MENGI KUPITA KIASI ?

Maji yanachukua takriban 50% hadi 70% ya uzito wa mwili wa binadamu. Kila seli, tishu na kiungo mwilini huhitaji maji ili kufanya kazi vizuri. Ingawa maji Yana faida nyingi k**a vile kusaidia kutoa takamwili kupitia mkojo na jasho, kuweka joto la mwili sawa,kulainisha viungo na kulinda tishu,matumizi yake kupita kiasi yanaweza kuwa na madhara.

Maji, k**a vitu vingine vyovyote, yanaweza kuwa sumu yakinywewa kwa wingi ndani ya muda mfupi. Sumu ya maji ( water intoxication/ water poisoning) ni hali inayotokea baada ya kunywa maji mengi kupita kiasi. Mara nyingi hali hii hutokea baada ya kunywa lita 3 hadi 4 za maji ndani ya saa moja au mbili. Matokeo ya sumu ya maji ni:

(I) Hyponatremia
Ni hali ambayo kiwango cha sodiamu katika damu inakuwa chini sana, na hivyo kuvuruga uwiano wa maji ndani na nje ya seli. Katika hali hii, mwili hushikilia maji mengi sana ambayo hufanya sodiamu kupungua kwenye damu. Hii inaweza kusababisha seli, hasa seli za ubongo, kuvimba na kusababisha dalili k**a vile kichefuchefu, maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, kifafa, na katika hali mbaya, koma au kifo.

(II) Uharibifu wa figo
Figo zina uwezo wa kuchuja kiasi kidogo tu cha maji ( lita 0.8 - 1) kwa saa. Kunywa maji mengi kupita kiasi huleta mzigo kwa figo, jambo ambalo linaweza kusababisha uharibifu wa figo kwa muda mrefu na kulazimisha mwili kutoa maji hayo Kwa kukojoa mara kwa mara.

✔️ SULUHISHO
• Kuelewa mahitaji ya mwili wako , hali ya mazingira uliyopo na shughuli unazofanya, kutakusaidia kukadiria kiasi cha maji unachohitaji kunywa kila siku. Kwa wastani Mtu mzima anahitaji karibu lita 0.035 za maji kwa kila kilo ya uzito wa mwili. Kwa mfano, mtu mwenye uzito wa kilo 50 anahitaji takriban lita 1.7 za maji Kwa siku .

• Ikiwa unafanya mazoezi au shughuli nzito, ongeza kiasi cha maji unachokunywa ili kufidia maji yanayopotea kupitia jasho. Pia unawezaa kuongeza electrolytes k**a glucose unapo kunywa maji wakati wa mashindano .

• Epuka kunywa maji mengi kwa wakati mfupi, kunywa hatua kwa hatua. Pia Rangi ya njano iliyokolea ya mkojo inaonyesha unahitaji kunywa maji zaidi.

By Thomass Arnold

➡️ FAHAMU ZAIDI KUHUSU NGOZI YA KUKU ? Baadhi ya watu wanaamini kuwa kula ngozi ya kuku inaweza kuwa na madhara kwa afya...
04/10/2024

➡️ FAHAMU ZAIDI KUHUSU NGOZI YA KUKU ?
Baadhi ya watu wanaamini kuwa kula ngozi ya kuku inaweza kuwa na madhara kwa afya na Wanapokula vyakula vya kuku, mara nyingi huondoa ngozi . Sasa tuangalie mtazamo huu kwa kuzingatia faida na hatari za kiafya za ngozi ya kuku.

Kwanza, kulingana na maudhui ya lishe, kipimo cha gramu 100 Cha ngozi ya kuku kina takriban kalori 450, gramu 36 za mafuta (ikiwa ni pamoja na gramu 11 za saturated fats na gramu 25 za unsaturated fats ), gramu 13 za protini, miligramu 70-100 za kolesteroli, na hakuna wanga.

✔️ Faida za kiafya za ngozi ya kuku
• Uwepo wa unsaturated fats ambazo Huwa Katika hali ya kimiminikaa kwa asili Kwa wingi kuliko saturated fats ambazo hua Katika hali ya mgando husaidia kupunguza shinikizo la damu na kolesteroli mbaya.Kwa kuwa mwili hauzalishi mafuta haya, lazima uyapate kupitia chakula unachokula.
• Pia ngozi ya kuku ina asidi ya oleic (aina ya mafuta) ambayo huboresha hali ya moyo kwa kupunguza kolesteroli na kuzuia uvimbe.
• Ngozi ya kuku ina takriban 35% ya tishu unganishi, nyingi zikiwa ni collagen. Collagen ni sehemu muhimu ya mifupa, ngozi, misuli, na sehemu nyingine za mwili.
• Kutokuwepo kwa wanga na uwepo wa protini ya ziada kunafanya ngozi ya kuku kuwa chanzo kizuri cha protini. Licha ya kuwa na mafuta , haina wanga, ambayo ni nzuri kwa wale wanaofuata lishe yenye wanga kidogo.

❌ Hatari za kiafya za ngozi ya kuku
Hatari za kiafya za kula ngozi ya kuku zipo katika uwepo wake wa Mafuta na uwezo wake wa kuongeza kalori kwenye mlo.Ngozi ya kuku ina saturated fats ambazo zina kalori nyingi kuliko protini au wanga. Kula Kwa kiwango kikubwaa vyakula vyenye kalori nyingi mara kwa mara kunaweza kusababisha kuongeza uzito na unene kupita kiasi, na kuongeza hatari ya magonjwa k**a vile kisukari na magonjwa ya moyo.

✔️ SULUHISHO
kulingana na tafiti nyingi za sasa, imethibitishwa kuwa ngozi ya kuku sio mbaya kabisa. Kula ngozi ya kuku inaweza kuwa na faida ikiwa unakula kwa njia sahihi, au kuwa mbaya ikiwa inaliwa vibaya. Kukaaanga kuku kwa mafuta huongeza mafuta kutoka kwenye mafuta yaliyotumika na kuongeza kalori zaidi.Inashauriwa Kula kwa kiasi na kuchanganya kuku na vyakula vyenye virutubisho vingi na mafuta kidogo . Machaguzi ya njia bora za kupika k**a kuoka badala ya kukaanga inasaidia Kupunguza athari hizo.

By Thomas Arnold

➡️JE, KULA  MAYAI  MAWILI AU MATATU KWA SIKU NI HATARI GANI KWA AFYA YAKO ? Mayai ni chanzo bora cha virutubisho muhimu ...
15/09/2024

➡️JE, KULA MAYAI MAWILI AU MATATU KWA SIKU NI HATARI GANI KWA AFYA YAKO ?

Mayai ni chanzo bora cha virutubisho muhimu k**a vile protini ambayo husaidia kwenye misuli, vitamini A, D, E, na B12 ambazo ni muhimu kwa afya ya macho, mifupa na kinga ya mwili.Aidha, yai lina madini k**a vile seleniamu, chuma, na fosforasi yanayosaidia katika kuimarisha mifupa. Pia Yana cholesterol na mafuta.

Uwepo wa takriban miligramu 186 za cholesterol kwenye yai , unapelekea ulaji wa zaidi ya yai moja usipendekezwe kwani unazidisha kiwango kinachohitajika mwilini. Kwa mujibu wa Food and Drug Association (2024), mtu anashauriwa kula si zaidi ya miligramu 300 za cholesterol kwa siku, kwani kuzidisha kiwango hiki kunaongeza hatari ya magonjwa ya moyo.

Pia kuwepo Kwa protini nyingi (5.2g - 7.1g) kwenye yai unapelekea ulaji wake kupita kiasi kuathiri figo kwa kuongeza kazi ya kuchuja taka k**a urea. Hii inaweza kusababisha uharibifu wa figo na kuongeza hatari ya kupata mawe kwenye figo, hasa kwa watu wenye figo dhaifu.

Vile vile ,Kula mayai kupita kiasi kunaweza kuathiri mmeng'enyo kutokana na kiwango kikubwa cha protini na mafuta hivyo kusababisha gesi na maumivu ya tumbo. Uwepo wa Sulfur kwenye amino acids za protein za mayai unapelekea piaa kuvimbiwa

✔️ SULUHISHO
Shirika la Moyo la marekani linapendekeza kuwa watu wengi wanaweza kula yai moja kwa siku, wakati watu wenye kisukari na magonjwa ya moyo wanapaswa kula hadi nusu yai, huku wachezaji na watu wanaofanya mazoezi wanaweza kula hadi mayai mawili kwa siku.

Pia, ni muhimu kuzingatia uwiano wa Ulaji wa mayai na vyakula vingine k**a vile ujii, mboga, na nafaka ili kupata lishe bora na kuzuia matatizo ya mmeng'enyo wa chakula.

Vile vile ,Kupunguza ulaji wa viini vya mayai, ambavyo vina cholesterol nyingi, kunaweza kusaidia kudhibiti viwango vya cholesterol mwilini na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kwa sababu sehemu nyeupe ya yai ni chanzo kizuri cha protini bila mafuta au cholesterol. Njia hii inasaidia katika kujenga misuli na kudhibiti uzito bila hatari zinazohusiana na cholesterol.

By Thomas Arnold

➡️ JE ,WAJUA MBEGU ZA APPLE   🍎 NI SUMU ?Kawaida kuna wastani wa  mbegu tano hadi kumi  ndani ya  tufaha au apple Kwa ji...
07/09/2024

➡️ JE ,WAJUA MBEGU ZA APPLE 🍎 NI SUMU ?

Kawaida kuna wastani wa mbegu tano hadi kumi ndani ya tufaha au apple Kwa jina lingine. . Mbegu za tufaha ( apple) zina amygdalin, ambayo hutoa cyanide kwenye damu unapoziweka mdomoni na kuzitafuna.

Cyanide ni sumu hatari ikiliwa kwa kiasi kikubwa. Wastani wa milligramu (mg) 50-300 inaweza kusababisha kifo kwa binadamu . Tafiti zinaonyesha kuwa mtu atalazimika kula karibu mbegu 83 hadi 500 ili kupata kiwango Cha cyanide kinachoweza kupelekea kifo. Hata hivyo, kiwango halisi cha cyanide kinachoweza kumfanya mtu awe mgonjwa kinategemea uzito wa mwili na Kinga yake.

Cyanide inazuia seli kutumia oksijeni kuzalisha nishati, hali inayopelekea ukosefu wa oksijeni kwenye viungo muhimu k**a moyo na ubongo. Hii inasababisha dalili k**a kuchanganyikiwa, kushindwa kupumua, na inaweza kusababisha kifo ikiwa haitatibiwa.

✔️ SULUHISHO
Epuka kula mbegu za matunda k**a vile apple, apricot, peas, prunes, cherries na peaches kwani Mbegu hizi zina cyanide . Pia ondoa mbegu unapoandaa apple kwa watoto au kwenye mapishi. Ikiwa utameza mbegu kimakosa, angalia dalili k**a kichefuchefu au kizunguzungu, na utafute msaada wa matibabu .

# ByThomas Arnold

➡️FAHAMU SABABU 4 ZINAZOFANYA ULAJI WA CHIPS WA MARA KWA MARA NA KWA WINGI USIPENDEKEZWE .Madhara ya ulaji wa chips kwa ...
23/07/2024

➡️FAHAMU SABABU 4 ZINAZOFANYA ULAJI WA CHIPS WA MARA KWA MARA NA KWA WINGI USIPENDEKEZWE .

Madhara ya ulaji wa chips kwa afya ya binadamu hutegemea mambo mbalimbali k**a vile kiasi cha ulaji, viwango vya mafuta , sodiamu, na additives , mtindo wa maisha kwa ujumla na hali ya afya iliyopo. Ulaji wa mara kwa mara na kupindukia unaweza kusababisha madhara ya kiafya k**a vile kuongezeka uzito na shinikizo la damu kutokana na sababu zifuatazo:

1. Chips zina virutubisho vichache muhimu. Chips mara nyingi huonekana k**a junk food. Kwa ujumla, zina mafuta yasiyo ya afya, chumvi, na kalori nyingi, huku zikikosa virutubisho muhimu.

2. Chips zina kiasi kikubwa cha mafuta. Viazi vina takriban asilimia 70 -80 ya maji. Wakati wa kupika, joto kubwa husababisha maji katika vipande vya viazi kupotea. Kadri maji yanavyopotea, mafuta humezwa ndani ya viazi, kuongeza kiasi chake cha mafuta. Hali hii hupelekea mvuke kutoka juu ya Mafuta wakati wa kukaanga.

3. Uwepo wa trans fats kwenye chips . Mara nyingi kutokana na aina ya mafuta yanayotumika ,trans fats zinaweza kuongeza viwango vya cholesterol mbaya (LDL) na kupunguza viwango vya cholesterol nzuri (HDL) mwilini na kupelekea madhara mbalimbali.

4. Chips zina viambata sumu k**a acrylamide, ambavyo hutengenezwa wakati viazi vinapopikwa kwa joto la juu . Acrylamide ni kemikali inayoweza kusababisha kansa. Acylamide hutengenezwa Kwa kiwango kikubw pale chips zinapopikwa Katika moto mkal kuliko upikaji Katika Joto la kawaida .

➡️ SULUHISHO

kupunguza ulaji wake mara kwa mara na kwa wingi,kuhakikisha chips zinaliwa k**a sehemu ya mlo wenye virutubisho kamili,kutumia mafuta yenye ubora na kubadilisha Mafuta mara Kwa mara wakat wa uandaaji wa chips ,Kupunguza matumizi makubwa ya chumvi ,Kutumia njia mbadala k**a vile kuoka wakati wa kuandaa chips utasaidia kupunguza madhara ya chips mwilini.

By Thomas Arnold

Address


Telephone

+255693405161

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chakula & afya na lishe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share