24/05/2026
Watu wengi wakisikia neno “acid” wanafikiri ni ugonjwa mmoja.
Mtu anasema:
“Nina acid.”
Lakini swali ni…
Acid gani?
Kuna watu wanaumwa viungo, miguu kuvimba, mawe ya figo…
Wanaambiwa wana uric acid.
Wengine wanapata moto kifuani, kiungulia, chakula kupanda kooni…
Nao wanasema wana acid.
Tatizo ni kwamba…
Uric acid na acid reflux si kitu kimoja kabisa.
Na ukichanganya…
Unaweza kutibu kitu ambacho hata huna.
Tuyaweke sawa leo.
# 1. URIC ACID NI NINI?
Uric acid ni taka inayotengenezwa mwilini baada ya kuvunjwa kwa vitu vinavyoitwa purines.
Purines huongezeka zaidi unapokula:
* Nyama nyekundu
* Maini na organ meats
* Samaki baadhi
* Vyakula vya processed
* Soda zenye fructose nyingi
* Pombe
Kwa kawaida…
Figo zinatakiwa kuchuja uric acid na kuitoa kupitia mkojo.
Lakini ikizidi…
Au figo zikichoka…
Uric acid inaanza kujikusanya kwenye damu.
Na hapo ndipo shida huanza.
Inaweza kusababisha:
* Gout (maumivu makali ya joint hasa kidole kikubwa cha mguu)
* Kuvimba viungo
* Mawe ya figo
* Uchovu
* Presha Kupanda
Hii si acid ya tumboni.
Ni acid ya kwenye damu na joints.
# 2. ACID REFLUX NI NINI?
Hii ni tofauti kabisa.
Acid reflux ni hali ambapo tindikali ya tumboni inapanda juu kuelekea kwenye koo.
Kawaida…
Kuna geti kati ya tumbo na koo.
ikilegea…
Acid inapanda juu.
Dalili zake:
* Kiungulia
* Moto kifuani
* Chakula kupanda kooni
* Kukohoa usiku
* Ladha chungu mdomoni
* Tumbo kujaa sana
* Gesi
Kwa hiyo acid reflux haihusiani na joints wala uric acid.
Ni tatizo la mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Hapa ndipo mambo yanavutia.
Vyakula vya kisasa vinachangia yote mawili.
Diet yenye:
* Processed foods
* Mafuta mengi
* Sukari nyingi
* Soft drinks
* Nyama nyingi
* Fiber kidogo
Inaweza:
* kuongeza uric acid
* na pia kuongeza acid reflux
Kwa hiyo mtu anaweza kuwa na vyote kwa pamoja…
Lakini bado ni magonjwa mawili tofauti.
Cha Kufanya...
Kwa uric acid:
* Kunywa maji ya kutosha
* Kupunguza nyama na sukari rahisi k**a soda
* Kupunguza uzito
* Kula chakula hai (Vyakula vinavyotokana na mimea katika uasili wake)
* Mazoezi
Kwa acid reflux:
* Kuepuka kula baada ya saa 1 usiku
* Kupunguza kula kuvimbewa
* Kupunguza mafuta kwenye mapishi yako
* Kupunguza uzito
* Kula vyakula rahisi vya asili (chakula hai)
Coach Wako,
Yusufu M Filemon, MD
(Dr Nature Lifestyle Clinic)
0767759137