
06/09/2024
ILI UWE NA AFYA BORA, MSINGI WAKE NI HUU: KILA SIKU FANYA HAYA
1. Kuna umuhimu mkubwa saaana, kufanya mazoezi mepesi ya mwili kwa dakika 15 hadi nusu saa ili kutengeneza mzunguko mzuri wa damu na uimara wa mwili wako kwa ujumla. Mazoezi haya siyo yale ya kukimbia hapana, ukiweza simama au ukiweza kaa kwenye kiti, cha msingi unaweza kunyanyua mikono na kushusha mara kadha, ikiwa nipamoja na miguu, chuchumaa simama mara kadha , inama na kuinuka mara kadha.
Ni mazoezi yale ya kufanya hapo hapo ulipo na iwe tabia yako endelevu, isiache kufanya hata siku moja, siyo leo umfanya kesho umeacha, haitaleta matokeo mazuri au afya Bora, naomba jenga tabia hii ya kutoa dakika 15 hadi nusu saa ufanye mazoezi ya mwili kwa afya Bora kuupa mwili wepesi.
Masomo haya yatakuwa endlevu yatatoka kwa wiki mara tatu, naomba usikose somo letu la 2 umuhimu wa kutumia maji k**a tiba. mwendelezo ,ni kila j3, j5, na ijumaa. Asanteni kwa kunifuatilia.