05/03/2025
Maswali Na Majibu
KWA NINI UJITOLEE KUCHANGIA DAMU?
Hadi sasa hakuna utaalamu wa kuzalisha damu nje ya binadamu. Kwa hiyo, wewe ni miongoni mwa wanaopaswa kujitolea damu. Unapojitolea damu unashiriki kikamilifu kuokoa maisha ya binadamu
NI MARA NGAPI MTU ANATAKIWA KUCHANGIA DAMU KWA MWAKA?
Mwanamke anaweza kuchangia kila baada ya miezi minne.
Mwanamume anaweza kuchangia kila baada ya miezi mitatu
JE NAWEZA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI WAKATI WA KUCHANGIA DAMU?
Hapana.
Kuchangia damu ni kitendo salama kabisa kwani vifaa vyote vinavyotumikwa ni safi na salama hutumika mara moja kwa mtu mmoja.
JE DAMU YANGU ITAFANYIWA VIPIMO GANI?
Damu itapimwa vipimo vifuatavyo:-
Kiwango cha damu
UKIMWI (VVU)
Kaswende
Homa ya Ini (Hepatitis B na C)
Makundi ya damu.
JE NITAPEWA MAJIBU YA VIPIMO VYA DAMU YANGU?
Ndio
Utapewa majibu yako kupitia mshauri nasaha baada ya kupimwa. Vipimo vyote vya maabara hufanywa kwa usiri wa hali ya juu. Hakuna mtu yeyote atakayeambiwa majibu ya vipimo vyako bila ya idhini yako.
changia damu
changia damu
Je, huwezi kushiriki katika michezo au shughuli nyingine zinazohusisha kutumia nguvu baada ya kuchangia damu?
Kuchangia damu hakuathiri uwezo wa kufanya michezo, mazoezi au shughuli nyingine za mwili. Ushauri unaotolewa ni kuepuka kuinua vitu nzito au mazoezi magumu kwa siku nzima baada ya kutoa damu. Unaweza kuendelea na uinuaji wa vitu vizito au mazoezi magumu kwenye siku inayofuata hasa kwenye mkono uliochomwa sindano.
Je Vigezo/Sifa gani za mtu anayeweza kuchangia damu?
Mtu yeyote, mwanamke au mwanaume anaweza kuchangia damu k**a ana vigezo vifuatavyo:
Umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 65
Uzito usiopungua kilo 50
Kwa mwanamke asiwe mjamzito au anaenyonyesha
Asiwe na maradhi ya muda mrefu k**a Shinikizo la damu, Kisukari, Kifafa, Pumu n.k
Awe mzima wa afya njema na asiwe na Homa
Asiwe na mienendo hatarishi ya kupata maambukizi ya magonjwa k**a Homa ya Ini (B&C), UKIMWI (HIV/AIDS)
Mwanamke anaweza kuchangia kila baada ya Miezi