21/11/2025
Kurasa 2:🧠🧠🧠SONONA🧠🧠🧠🧠🧠🧠
SWALI LA KUJIULIZA JE WEWE NA MIMI TUPO SALAMA ?
Twende pamoja
Kurasa ya pili
Ni nini Haswa chanzo cha sonona ?
Kitaalamu kabisa ugonjwa huu unasababu mbalimbali kuu yani za kibiologia , kisaikologia lakini pia za kijamii
KIBIOLOGIA:
🦠🦠🦠Sababu za kurithi yaani genetic factors kulingana na tafiti za kisayansi zenye ushahidi wa kisayansi kuna uhusiano mkubwa wa ugonjwa wa sonona na vinasaba ni hivi kuna nafasi kubwa k**a wazazi wako walishawai kupitia ama kuugua maradhi haya basi na wewe upo kwenye nafasi kubwa ya kuweza kuumwa ama kuonesha dalili hizo
🫄🏿🫄🏿🫄🏿Kipindi cha ujauzito wako kuna ushaidi pia wa kisayansi ambao unaonesha kipindi cha ujauzito mama anayepitia hali ya sonona ana nafasi kubwa kuzaa mtoto ambaye baadaye anaweza kupata shida hii ili nitalieleza private kwa anayetaka kufahamu zaidi
🥃🥃🥃🍻🍺🍺Matumizi ya vileo k**a vile pombe kupitiliza ,sigara ,bangi, mirungi , ugoro na matumizi ya vileo vingine ambazo upelekea magonjwa katika mifumo yetu ya ubongo katika kutafsiri, kuamua na kutenda
😱Magonjwa ya muda mrefu k**a vile kisukari , hypertension, magonjwa ya tezi hyperthryodism ,hypothyroidism, cancer , HIV na magonjwa yanayoweza kuathiri mifumo ya fahamu na ubongo
🎃🎃UMRI japenye umri hakuna specific age unayoweza kusema hii ndio sababu ya magonjwa ya sonona japo kwa tafiti za hivi karibuni inaonesha kundi la vijana linaathirika zaidi kuliko kundi lolote na tafiti zaidi zinendelea kuthibitisha jambo ili
KISAIKOLOGIA:
Kupitia kipindi kigumu kwenye maisha k**a vile msiba, kukosa kazi , ajali mbaya ya kukatisha uhai , kupitia manyanyaso ya kimwili ama kihisia k**a vile kubakwa kupigwa , vita
Kufeli kimaisha ,kibiashara, kielimu ,yatima ,kutengwa na familia, ukimbizi ,
KIJAMII:
Changamoto za mahusiano uchumba na ndoa hapo ndio changamoto nyingi utokea
Maisha magumu kukosa maitaji ya msingi k**a vile chakula,maladhi na mavazi
Mimba za utotoni ama mimba zisizotarajiwa haswa kwa vijana wetu
Tuendelee