05/07/2024
_*POMBE HUUWA MTU MMOJA NDANI YA KILA SEKUNDE KUMI...
+255626027279
_*Ripoti hiyo ya WHO iliyopewa jina la โKupunguza madhara yatokanayo na pombe inaonyesha vifo milioni 3 kwa mwaka*_
โข Sawa na watu milioni 3 hufa kila mwaka kutokana na matumizi mabaya ya pombe, hii ni sawa na mtu mmoja kila baada ya sekunde 10 akiwakilisha karibu asilimia 5 ya vifo vyote.
โข Idadi isiyo na uwiano ya vifo hivi vinavyohusiana na pombe hutokea miongoni mwa vijana, huku asilimia 13.5 ya vifo vyote ikiwa ni kati ya wale walio na umri wa miaka 20-39 wakihusishwa na pombe.
โข Matumizi ya pombe kupita kiasi ni moja ya vichocheo vya magonjwa yasiyoambukiza, ,
โข โMwanamke asizidishe bia moja kwa siku na mwanaume asizidishe bia mbili kwa siku. Wanawake wengi wanapenda mvinyo au wine, anatakiwa anywe mililita 125 za wine sawa na glass kwa siku usizidishe na wanaume 250,โ .
โข Ili viungo vya mwili viweze kuchakata sukari vizuri na taka zote zitokanazo na pombe katika viwango, kwa wiki mwanaume asizidishe uniti 14 na mwanamke uniti saba. Uniti moja ni sawa na asilimia 4 ya kilevi.
1. _*Vidonda vya tumbo na Udhaifu wa mwili*_
โข Pombe inaathiri mfumo wote wa mwili kuanzia utumbo ambapo husababisha vidonda vya tumbo hasa inapoingia katika mfumo wa usafishaji mwili au kuchangia kwa kiwango kikubwa utumbo kushindwa kuchakata chakula na kuchukuwa virutubisho , Pia kuondoa kiwango kikubwa Cha virutubisho kupitia mkojo na upelekea miili ya walevi kupita kiasi kuwa dhaifu Sana na kukosa nywele na ngozi zenye muonekano halisi.
2. _*Saratani ya Koo*_
โข Pombe ni kichocheo cha Saratani ya koo inayotokana na kutapika ukali wa pombe unaochoma Koo , Pia inaathiri tezi ya kongosho ambayo inatoa insulin inayosaidia kusaga sukari na usagaji wa sukari ukiathirika kinachotokea mtu anapata ugonjwa wa kisukari,โ .
3. Huathiri fahamu na kumbukumbu*_
โข Unywaji Pombe kupita kiasi huathiri mfumo wa fahamu na kumbukumbu Kutokana na ongezeko za sumu mwilini kusababisha damu kusindwa kupenya kwenye Mishipa midogo imidogo yw fahamu na kupelekea baadhi ya maeneo muhimu kukosa hisia ikiwemo uume na hivyo kusababisha tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume.
โข Pombe inaathiri ubongo na mara nyingi watu hupoteza kumbukumbu wanapozitumia kupita kiasi โKwenye ubongo pombe huondoa baadhi ya madini,hasa folic acid ambayo ni msaada mkubwa wa utendaji kazi wa shughuli za ubongo..
4. _*Magonjwa ya Moyo*_.
โข Unywaji mkubwa wa pombe husababisha matatizo mbalimbali ya moyo ambapo mishipa ya moyo hudhoofika na kushindwa kusukuma damu. Jambo hili huweza kusababisha damu kuganda na kusababisha kiharusi (_*Stroke*_). Pombe huchangia sana katika kudhoofisha mishipa ya moyo hivyo kupelekea ugonjwa huu wa _*Cardiomyopathy*_ , _*Heart attack*_ , __*Cardiac system failure*_ na mengine hatari.
5.. _*Magonjwa ya ini*_
โข Unywaji wa pombe unaweza kusababisha maradhi ya ini yajulikanayo k**a Cirrhosis; ambayo ni maradhi ya ini kushindwa kufanya kazi yake kutokana na uharibifu wa muda mrefu. Uharibifu huu husababisha seli za ini kuwa makovu na kushindwa kufaya kazi vyema. Utafiti umebaini kuwa pombe huchangia sana katika kuharibu seli hizi za ini.
6. _*Shinikizo la damu*_ ( _*Pressure*_).
โข Unywaji wa pombe hasa kupitiliza umedhibitishwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maradhi ya shinikizo la damu. Imebainikia kuwa pombe huathiri mfumo wa usukumaji wa damu mwilini jambo ambalo hupelekea shinikizo la damu na baadae matatizo mengine k**a kushindwa kwa figo, ini ,Kiharusi n.k.
7. _*Magonjwa ambukizi*_
โข Mara nyingi mtu anapokunywa pombe hupoteza uwezo wa kutawala mwili na maamuzi yake. Hivyo ni rahisi baada ya mtu kunywa pombe akafanya au akajiingiza kwenye matendo hatarishi yanayoweza kumfanya kuambukizwa magonjwa k**a vile UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.
8.. _*Ugonjwa wa ANAEMIA*_
โข Anemia ni ugonjwa unaotokana na kushindwa kwa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni ya kutosha kwenda kwenye mwili. Hivyo unywaji wa pombe hupunguza uwezo wa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni ya kutosha hivyo kupelekea ugonjwa wa anemia.
9. _*Madhara ya hapo kwa hapo*_
โข Unywaji wa pombe wa kupita kiasi una madhara ya moja kwa moja kwa afya ya binadamu anayetumia. Baadhi ya madhara hayo ni k**a ifuatavyo:
>Kuharisha
>Kutapika
>Maumivu ya kichwa
>Kuumia kutokana na ajali za magari au pikipiki,kuanguka na kuungua
>Ukatili,kujinyonga,ubakaji na ugomvi
>Kuathirika na sumu katika pombe kutokana na kilevi kilichopitiliza
>Tabia hatarishi kiafya k**a kufanya mapenzi bila kinga au kuwa na wapenzi wengi wa nje.
>kutoka kwa mimba kwa wanawake au kuza watoto kabla ya wakati
>Hupunguza hamu na uwezo kujammiana
10. _*Madhara ya muda mrefu*_
Matumizi ya muda mrefu ya pombe yanapelekea kupata magonjwa sugu na madhara mengine kiafya yakiwemo:-
>Msongo mkubwa wa damu-Presha na magonjwa ya moyo.
>Magonjwa ya ini na magonjwa ya mfumo wa chakula
>Kansa ya matiti,mdomo,koo,ini na kansa ya utumbo
>Kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kujifunza (Sababu ya ukosefu wa Vitamini B1)
>Matatizo ya kiakili -Kukosa dira katika maisha ya mbele (Depression)
>Kujenga kasumba ya kutumia pombe (Utumwa wa matumizi ya pombe)
>Vidonda vya tumbo
>Kuongezeka kwa uzito -Kutokana na kiwango cha wanga katika pombe
>Ugonjwa wa mifupa(Osteoporosis)-Pombe inapunguza uwezo wa kalsium kutumika kujenga mifupa
>Matatizo ya Uzazi-Wanaume wanapungukiwa nguvu za kiume na wanawake kushindwa kushika mimba kirahisi.
>Kunywa pombe kidogo kunaweza kupunguza kwa mkiasi kikubwa madhara haya
๐ณ Kwa msaada zaidi :- Tafadhali Usisite Kuwasiliana Nasi Kuhusu Tiba Kwa Njia za Kisasa Kabisa na Ushauri wa Masuala Mbali Mbali Ya Afya.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐A๐๐๐ ๐๐๐๐ & ๐๐๐๐๐๐๐๐
Callโtext&smsโwhatsapp๐
โ Ili Kupata Ushauri Bure na Msaada Zaidi Kuhusu Matatizo Mbali Mbali Kiafya - Mawasiliano - +255655562181 au +255769600821
โ Jiunge na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa ๐๐๐.....
โ SHARE kwenye MA GROUP NA WATU MBALI MBALI UWASAIDIE WENGI WANAO TESEKA ๐๐๐ kisha tuandikie maoni yako au ushauri hapo chini
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐.
TAFADHALI : USISAHAU KU SHARE.