
09/09/2024
Mzunguko wa hedhi kawaida huchukua kati ya siku 21 hadi 35, ingawa wastani kwa wanawake wengi ni siku 28.
Zijue awamu za Mzunguko wa hedhi👇🏼
1️⃣ Awamu ya Hedhi: Hizi ndiyo siku ambazo mwanamke hutokwa na damu. Huchukua kati ya siku 3 hadi 7.
2️⃣ Awamu ya Follicular: Huanza siku ya kwanza ya hedhi na kuendelea hadi ovulation. Hii ni kati ya siku 1 hadi 14 kwa wastani.
3️⃣ Ovulation: Huu ni mchakato wa yai kutoka kwenye ovari, hufanyika katikati ya mzunguko, karibu siku ya 14 kwa mzunguko wa siku 28.
4️⃣ Awamu ya Luteal: Huanza baada ya ovulation na kuendelea hadi mwanzo wa hedhi ijayo. Hii ni kati ya siku 15 hadi 28.