05/12/2024
Mvurugiko wa hedhi ni tatizo ambalo huanza ghafla au polepole ambalo mwanzo mwanamke alikuwa atapata siku zake katika utaratibu aliouzoea, mara haelewi mzunguko wake unavyoenda
🧵 Mvurugiko wa hedhi ni pale mwanamke anaanza kuona siku zake bila mpangilio maalimu na matokeo yake ni kuwa atashindwa kutimiza malengo yake ya uzazi.
🧵Mvurugiko wa hedhi unaweza kupelekea tu ukapata hedhi wakati ambao hukutarajia, jambo ambalo linakufanya ubaki na uwoga na huelewi nini cha kufanya kwani ulikuwa hujajiandaa kwa tukio hilo
🧵 Wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi au miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakuwa huna ujauzito wala dalili za ujauzito huna
MADHARA YA KUVURUGIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI
🫒 Madhara ya kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi kwa mwanamke ni k**a yafuatayo
👉 Kushindwa kupata ujauzito
👉 Inachochea maambukizi kwenye kizazi k**a P.I.D na UTI
👉 Kuziba kwa mirija ya uzazi
👉 Inapelekea saratani kwenye kizazi
FAIDA ZA KUWA NA MZUNGUKO WA HEDHI ULIO SAWA
Mzunguko wa hedhi ulio sawa utamsaidia mwanamke kufanya yafuatayo
👉 Kupata ujauzito alioupangilia
👉 Kuepuka ujauzito ambao hukupangilia
👉 Kuepeka changamoto za mfumo wa uzazi k**a mirija kuziba na uvimbe kwenye kizazi
👉 Kuepuka maumivu ya kiuno na chini ya kitovu wakati wa hedhi.
👉 Kumfanya mwanamke kujiamini hata pindi anapoingia hedhi
SABABU ZINAZOPELEKEA MVURUGIKO WA MZUNGUKO WA HEDHI
Ni rahisi kugundua k**a mzunguko wako wa hedhi umevurugika ikiwa tu unafahamu vizuri mzunguko wako wa hedhi ulio sahihi
Kufahamu mzunguko wako kufahamu siku ambayo ulianza kuona damu hadi pale utakapoona tena mzunguko unaofata.
Tatizo linaweza kuanza kwa kuruka kwa hedhi, kukosa hedhi kwa baadhi ya miezi, mwingine anaweza kuingia hedhi mara mbili kwa mwezi mmoja, mwingine damu yake inaweza kutoka kidogo kidogo kila siku, mwingine anaweza kuwa na hedhi ya mabonge mabonge na maumivu pia
Maumivu haya chini ya kitovu huanza chini ya tumbo mpaka miguuni na kiunoni ambayo kitaalamu hujulikana k**a "dymenorrhea "
Zifuatazo ni sababu zinazopelekea kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi
👉 Mabadiliko ya mazingira
Mabadiliko ya mazingirs yanaweza kupelekea baadhi ya mifumo ya mwili kubadilika hali ambayo kitaalamu kitaalamu hujulikana k**a " Adaptive mechanism " hasa mwanamke akitokea sehemu za joto kwenda sehemu za baridi au sehemunza baridi kwenda sehemu za joto
👉 Msongo wa mawazo
👉 Hofu
👉 Mabadiliko ya Kisaikolojia
👉 Uvimbe kwenye kizazi
👉 Matatizo kwenye mfumo wa homoni
👉 Matatizo kwenye vifuko vya mayai
👉 Mimba kuharibika
👉 Maambukizi sugu kwenye kizazi mfano P.I.D
JINSI YA KUREKEBISHA MVURUKIKO WA HEDHI
Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri kuonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndo sababu ya tatizo kwa upande wako kati ya zile nimekuainishia pale juu 👆👆👆
Vyakula/ matunda yafuatayo hurekebisha Mvurugiko wa hedhi ukitumia uwapo katika mazingira ya nyumbani
👉 PAPAI🍐
Papai lina virutubisho muhimu k**a carotene, chuma ( iron ), kalsiumu ( calcium ), vitamin A na C ambavyo kwa pamoja husaidia kurekebisha mvurugiko wa hedhi
Unashauriwa kula papai kila siku, nusu papai au papai zima kutegemea na uwezo wake au uwezo wako wa kula
Pia unashauriwa kutumia papai katika mlo wako wa kila siku siyo mpaka muugue
👉 MDALASINI ☕️
Ina sifa ya kusaidia kuondoa tatizo la damu kuganda, sifa inayoweza kusaidia kuondoa maumivu wakati wa hedhi
Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi ( fibers ), kalsiumu ( calclium ), Chuma ( iron ), manganizi ( manganese )
🍸Jinsi ya kutumia mdalasini
Changanya kijiko kidogo cha mdalasini wa unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako
👉TANGAWIZI 🫚
Tangawizi ni dawa yenye maajabu katika kutibu changamoto za mfumo wa hedhi.
Tangawizi hufanya kazi muhimu katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu wakati wa hedhi iitwayo " prostaglandin "
Tangawizi pia husaidia kuondoa uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku za mwanzo wa hedhi au siku mbili hivi kabla hujaingia hedhi.
Kubwa zaidi hufanya mzunguko wa hedhi usio sawa kuwa sawa
🍸Jinsi ya kutumia Tangawizi kutibia Mvurugiko wa hedhi
Tengeneza chai ya Tangawizi, ukitumia tangawizi mbichi, hakikisha chai yako inakuwa kali kwa kuweka tangawizi nyingi, kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata ladha badala ya sukari.
Kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 fanya hivo siku yeyote tu k**a kinga kwenye mwili wako.
Pia unaweza kuongeza Tangawizi kwenye chakula na mboga nyingi unazopika kila siku
👉 MREHANI ( BASIL )
Mrehani ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla
Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahoteli ya kitalii Dar es salaam na Zanzibar kwani unao sifa kuu ya kuzuia na kuondoa maumivu mwilini
🍸 Jinsi ya kutumia mrehani katika mvurugiko wa hedhi
Chukua kijiko kimoja cha majani ya mrehani yaliyokatwa katwa na kisu ( chop ) na weka kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipoe, ikishapoa kunywa yote na ufanye zoezi hili kutwa mara 3
Pia unaweza kutengeneza juisi ya majani haya kwa kuyabona kwenye kinu au kusaga kwenye blenda ya umeme kisha chota vijiko 2 vya chai na uweke kwenye kikombe cha maji ya moto na unywe yote, fanya zoezi hiki kutwa mara 3
Unaweza pia kuongeza majani ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku k**a wafanyavyo kwenye mahoteli makubwa.
👉 MAJI YA KUNYWA🥛
Matatizo ya kiafya karibu yote mwilini chanzo chake kikubwa ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha, jitahidi ujijengee desturi ya kunywa maji mengi, walau lita 2-3 kila siku
✍️HITIMISHO
Mvurugiko wa mzunguko wa hedhi mara nyingine husababishwa na mvurugiko wa homoni
Mvurugiko wa homoni kwa mwanamke ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa homoni katika mwili wa mwanamke.
Hivyo ikiwa changamoto yako ya mvurugiko wa hedhi imetokana na mvurugiko wa homoni, Nashauri utumie virutubisho vilivyotokana na matunda na mimea, Virutubisho hivi vitamaliza kabisa changamoto yako na kukufanya uwe katika hali yako ya wali ya kupata hedhi katika mpangilo mzuri
Kupata Virutubisho hivyo wasiliana kwa kupiga/WhatsApp kupitia namba 0776250309