Gcat hospital

Gcat hospital Tunatoa huduma ya vipimo na matibabu

TATIZO LA KUZIDI KWA KIWAGO CHA ACID TUMBONI (ACID REFLUX-GERD)๐Š๐€๐‘๐ˆ๐๐” Gastroesophageal reflux disease (GERD).-Ni hali in...
17/10/2024

TATIZO LA KUZIDI KWA KIWAGO CHA ACID TUMBONI (ACID REFLUX-GERD)

๐Š๐€๐‘๐ˆ๐๐”

Gastroesophageal reflux disease (GERD).
-Ni hali inayotokana na kuzid kwa kiwango cha Acid tumboni (Hydrochloric Acid) ambapo hupelekea kupanda kwa acid kutoka tumboni kuelekea katika koo la Chakula (Oesophagus) na kupelekea kudhurika kwa mfumo wa chakula upande wa juu ambao unahusisha koo la chakula na mdomo pia.

Watu wengi sana wanasumbuliwa na tatzo hili bila wao kujua wanasumbuliwa na tatzo hili na hufikia hatua wengine kudhani wamerogwa kutokana na dalili ya tatzo hili. Tutaangalia dalili ambazo mtu anaweza kugundua kuwa anasumbuliwa na tatzo hili.

DALILI ZA MTU ANAYESUMBULIWA NA KUZID KWA ACID TUMBONI (GERD-Acid Reflux
-Zipo dalili nyingi ambazo huashiria mtu kusumbuliwa na tatizo la kuzidi kwa Acid tumboni,dalili hizo ni zifuatazo:โคต๏ธโคต๏ธ

1.๐Ÿ–‡๏ธ Kuwaka moto kifuani(Kiungulia) hasa wakati wa usiku au unapolala,hali hii hutokea pia mara baada ya kula.
2.๐Ÿ–‡๏ธ Mapigo ya moyo kwenda mbio/kushtuka kwa moyo baadhi ya nyakati.Hali hii hupelekea baadhi ya watu kuhisi wana matatizo ya moyo.
3.๐Ÿ–‡๏ธ Kuhisi k**a kichwa kimevurugika na kuhusi kuchanganyikiwa.
4.๐Ÿ–‡๏ธ Kusahau mara kwa mara hata vitu vya kawaida kabisa/Kupungua kwa kumbukumbu.
5.๐Ÿ–‡๏ธ Kujisaidia choo kigumu k**a cha mbuzi.
6.๐Ÿ–‡๏ธ Kuwa na wasiwasi na khofu kubwa na hufikia hatua hata ukipigiwa simu hasa nyakati za usiku moyo huanza kwenda mbio na kujawa na wasiwasi mkubwa.
7.๐Ÿ–‡๏ธ Kukosa usingizi ama kushtuka mara kwa mara kutoka usingizini.
8.๐Ÿ–‡๏ธ Kupumua kwa tabu baadhi ya nyakati.
9.๐Ÿ–‡๏ธ Kupata maumivu ya kichwa ya mara kwa mara kwa baadhi ya watu wenye tatizo hili.
10.๐Ÿ–‡๏ธ Kupata kikokozi kisichoisha
11.๐Ÿ–‡๏ธ Kuvimba Tonsillitis/mafidofido mara kwa mara.
12.๐Ÿ–‡๏ธ Mdomo kuwa mchachu na huwez kupelekea kutoa harufu mbaya ya kinywa.
13.๐Ÿ–‡๏ธ Kuhisi k**a kuna kitu kimekwama kooni lakin kila unavyojaribu kukitoa hakitoki
14.๐Ÿ–‡๏ธ Kupata fangasi mdomoni(mdomo huanza kutoa ute mweupe ambao una harufu mbaya).
15.๐Ÿ–‡๏ธ Huweza kupelekea ukaanza kuota ndoto za kutisha pindi ulalapo na kuhisi umerogwa.
16.๐Ÿ–‡๏ธ Kupata maumivu ya mgongo hasa sehemu ya mabega,maumivu makali kana kwamba umenyanyua vitu vizito.
17.๐Ÿ–‡๏ธ Mwili kuwa na uchovu usioisha utadhani unafanyakaz ngumu kila siku.
18.๐Ÿ–‡๏ธ Macho kupunguza uwezo wa kuona vizuri.
19.๐Ÿ–‡๏ธ Kupungua uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
20.๐Ÿ–‡๏ธ Mwili kupata baridi na wakat mwingine kuhisi homa kabisa.
21.๐Ÿ–‡๏ธ Maumivu ya tumbo kati ya kifua na tumbo.
22.๐Ÿ–‡๏ธKichefuchefu na kutapika.

MAMBO YANAYOWEZA KUCHOCHEA TATIZO LA KUZIDI KWA ACID TUMBONI
1.๐Ÿ–‡๏ธ Uvutaji wa sigara
2.๐Ÿ–‡๏ธ Unywaji wa pombe
3.๐Ÿ–‡๏ธ Utumiaji wa vyakula au vinywaji vywenye Caffeine k**a vile Kahawa,Chocolate, Soda nk
4.๐Ÿ–‡๏ธ Kula vyakula vyenye mafuta mengi/vyakula vilivyokaangwa
5.๐Ÿ–‡๏ธ Kula chakula kingi kupita kiasi ama kula usiku sana.
6.๐Ÿ–‡ Kutumia baadhi ya Madawa k**a vile ASPIRIN
7.๐Ÿ–‡๏ธ Ngiri ya kifua pia husababisha GERD lakin pia GERD huweza kisababisha Ngiri ya Kifua(Huatal hernia)
8.๐Ÿ–‡๏ธ Kuwa Mjamzito
9.๐Ÿ–‡๏ธ Uzito kupita kiasi (Obesity)
10.๐Ÿ–‡๏ธ Matatzo ya mmeng'enyo wa chakula au kuchewa Kujisaidia pindi uhisipo haja kubwa.

MATIBABU YA TATIZO LA KUZIDI KWA ACID TUMBONI-GERD
-Matibabu ya KUZIDI kwa Acid tumbon yamegawanyika katika aina mbili k**a ifuatavyo:โคต๏ธโคต๏ธ

1๏ธโƒฃ MATIBABU YA KISASA
-Matibabu haya yanahusisha utumiaji ya njia za hospital katika matibabu ikiwemo utumiaji wa PPIs(Proton pump inhibitors),Antacids,Histamine, H-2 Blockers k**a vile Cimetidine (tagament HB),famotidine (Pepcid AC),Nizatidine (Axid AR)
-esomeprazole (Nexium), lansoprazole (Prevacid), omeprazole (Prilosec), pantoprazole (Protonix), rabeprazole (Aciphex) and dexlansoprazole (Dexilant) .Magnesium nk.
Dawa hizi zimekuwa zikitumiwa sana na watu wenye changamoto za Acid nying tumboni na miongoni mwa changamoto ni kwamba dawa hizi zimekuwa zikionesha msaada mdogo sana kwa asilimia kubwa ya wagonjwa na hutoa naafuu ya muda tu.

2๏ธโƒฃ MATIBABU KWA TIBA ASILI/TIBA MBADALA.
-Njia hii inahusisha matibabu kwa kutumia mimea tiba na imeonekana kuwa na ufanisi mkubwa kutokana na uwezo mkubwa wa mimea mingi katika kupambana na magonjwa mbalimbali kwasababu mimea kutibu kiini cha tatzo kwa kuzifanya kuwa mpya seli za mwili hivyo kuufanya mwili kuwa na uwezo mpya katika kufanyakazi zake.

Wasiliana nami kwa msaada zaidi wa kitaalamu katika kupambana na tatizo hili

*Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha goiter, ikiwa ni pamoja na*1. Upungufu wa Iodini: Iodini ni madini muhimu amb...
17/10/2024

*Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha goiter, ikiwa ni pamoja na*

1. Upungufu wa Iodini: Iodini ni madini muhimu ambayo tezi ya kongosho hutumia kutengeneza homoni za kongosho. Upungufu wa iodini mwilini unaweza kusababisha tezi ya kongosho kufanya kazi kupita kiasi ili kujaribu kuzalisha homoni za kongosho, na hivyo kusababisha uvimbe wa tezi ya kongosho.

2. Ugonjwa wa Hashimoto: Ugonjwa wa Hashimoto ni hali ya kinga ya mwili inayoshambulia tezi ya kongosho. Mchakato huu husababisha uvimbe wa tezi ya kongosho na kupungua kwa uzalishaji wa homoni za kongosho.

3. Uzalishaji wa Homoni za Kongosho Kupita Kiasi (Hyperthyroidism): Hali ambapo tezi ya kongosho inazalisha homoni za kongosho kupita kiasi inaweza kusababisha goiter. Uzalishaji wa homoni nyingi za kongosho unaweza kuchochea ukuaji wa tezi ya kongosho na hivyo kusababisha uvimbe.

4. Matumizi ya Dawa: Baadhi ya dawa, k**a vile dawa za kukandamiza uzalishaji wa homoni za kongosho au dawa zinazotumika kutibu magonjwa mengine, zinaweza kusababisha uvimbe wa tezi ya kongosho.

5. Magonjwa Mengine: Magonjwa mengine k**a vile tumors, maambukizi au magonjwa ya autoimmune yanaweza pia kusababisha goiter.
K**a una tatizo hili Usisite kuwasiliana nami moja kwa Moja Kupata tiba sahihi ya kumaliza kabisa tatizo lako

๐——๐—”๐—Ÿ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐—ฉ๐—œ๐——๐—ข๐—ก๐——๐—” ๐—ฉ๐—ฌ๐—” ๐—ง๐—จ๐— ๐—•๐—ข (๐—จ๐—Ÿ๐—–๐—˜๐—ฅ๐—ฆ)๐Ÿ‘‡ โœ๏ธKuchoka sana bila sababu maalum.โœ๏ธKuumwa mgongo/Kiuno.โœ๏ธKupungukiwa au kupoteza ...
16/10/2024

๐——๐—”๐—Ÿ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐—ฉ๐—œ๐——๐—ข๐—ก๐——๐—” ๐—ฉ๐—ฌ๐—” ๐—ง๐—จ๐— ๐—•๐—ข (๐—จ๐—Ÿ๐—–๐—˜๐—ฅ๐—ฆ)๐Ÿ‘‡
โœ๏ธKuchoka sana bila sababu maalum.
โœ๏ธKuumwa mgongo/Kiuno.
โœ๏ธKupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kiume (Wanaume)
โœ๏ธKizunguzungu
โœ๏ธKukosa usingizi
โœ๏ธMaumivu makali sehemu ya mwili
โœ๏ธMaumivu ya Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali.
โœ๏ธKichefuchefu/Kiungulia
โœ๏ธTumbo kujaa gesi
โœ๏ธTumbo kuwaka moto
โœ๏ธMaumivu makali sehemu kilipo kidonda
โœ๏ธKukosa choo au kupata choo kwa shida (Constipation)
โœ๏ธKutapika nyongo
โœ๏ธKutapika damu au kuharisha
โœ๏ธSehemu za mwili kupata ganzi
โœ๏ธKukosa hamu ya kula
โœ๏ธKula kupita kiasi
โœ๏ธKusahahu sahau Mara kwa Mara
โœ๏ธHasira bila sababu.
โœ๏ธKuwa na Tatizo la Bawasiri

MAUMIVU YA HEDHI MAKALI SANA๐Ÿ‘‰Dysmenorrhea Ni Kitu Gani?Dysmenorrhea ni jina la kitabibu kwa maumivu kipindi cha hedhi. M...
16/10/2024

MAUMIVU YA HEDHI MAKALI SANA

๐Ÿ‘‰Dysmenorrhea Ni Kitu Gani?

Dysmenorrhea ni jina la kitabibu kwa maumivu kipindi cha hedhi. Maumivu ambayo hutokana na kusinyaa kwa misuli ya mji wa mimba. Wakati wa hedhi misuli husinyaa, ili kuruhusu kumeguka kwa ukuta na kutoa damu iliyochanganyika na yai ambalo halikurutubishwa nje. Maumivu haya yamegawanyika katika aina mbili

Aina Ya Kwanza Ya maumivu ya Kawaida (Primary Dysmenorrhea)

Maumivu haya ni ya kawaida kabisa kwa wanawake wanapopitia kipindi hikia ambacho hujirudia kila mwezi. Maumivu kikawaida huanza kati ya siku moja ama mbili kabla ya hedhi kuanza kutoka. Mwanamke hujiskia mamumivu haya kwenye tumbo la chini, kwenye nyonga na kiuno kwa ujumla.

Maumivu haya yanaweza kuwa madogo au yakawa makali sana na huisha ndani ya masaa 12 mpaka 72. Yanaweza kuambatana na kutapika na kupata kizunguzungu. Kwa wanawake wengi maumivu haya ambayo ni ya kawaida kabisa hupungua kadiri umri unavoenda na pia pale mwanamke akijifungua.

Maumivu Aina Ya Pili Yasiyo Ya Kawaida (Secondary Dysmenorrhea)

Maumivu haya ni kutokana na tatizo fulani la kiafya kweye via vya uzazi vya mwanamke. Changamoto k**a vile uvimbe ambayo siyo wa saratani ndani ya mfuko wa mimba (uterine fibroids), kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba kuelekea kwenye viungo vingine k**a uke na mifuko ya mayai (endometriosis).

Na pia kupanuka kwa ukuta wa uterus kutokana na kukua kwa tishu za ndani za uterus kuelekea ukuta wa nje (adenomyosis). Maumivu haya pia yasiyo ya kawaida yanaweza kuwa yamesababishwa kwa athari za bacteria ama virusi katika via vya uzazi.

Kikawaida maumivu haya huanza mapema zaidi wakati wa hedhi ya huchukua muda mrefu zaidi kuisha ukilinganisha na maumivu yake ya kawaida (primary dysmenorrhea). Na pia maumivu haya yanakuwa hayaambatani na kutapika, kuharisha, kizunguzungu wala kukosa nguvu na ganzi.

Maumivu ya tumbo la hedhi kikawaida yanatambulika k**a tumbo la chango kwa wakinamama. Katika hali ya kawaida maumivu haya sio makali kiasi cha kuharibu ratiba za mwanamke. Lakini hutokea wakati mwingine yakawa makali sana kiasi cha kupelekwa hospitali, ama mwanamke kushindwa kufanya shughuli zake. Sasa nini sababu ya maumivu haya kupitiliza? Makala hii itakwenda kuangalia sababu za maumivu makali ya tumbo la chango au maumivu makali ya tumbo la hedhi.

Sababu za maumivu makali ya tumbo la hedhi
K**a mwanamke anaingia hedhi kwa na maumivu makali anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu k**a ibuprofen. Lakini k**a kuna sababu nyingine zinazopelekea maumivu kuwa makali hata akimeza dawa hii maumivu yatakuwa ni yenye kuendelea.

Dalili za maumivu makali ya hedhi ni
1.maumivu yasiyokata hata baada ya kumeza dawa za kupunguza maumivu
2.K**a maumivu makali kiasi cha kuharibu ratiba za shunguli za kawaida
3.K**a maumivu yanafuatana na damu nyingi ama kuganda kwa damu

Nini sababu ya maumivu makali ya hedhi?
1.kuota kwa tishu (nyamnyama) maeneo mengine tofauti na tumbo la mimba. Kitaalam hali hii inatambulika k**a endometriosis. Hali pia inaweza kuwa na dalili zifuatazo:-
A.Kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi
B.Hedhi kuchukuwa siku zaidi ya 7
C.Kutokwa na damu kabla ya siku za hedhi kufika
D.Maumivu ya tumbo
E.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
F.Kupata maumivu wakati wa haja kubwa.
G.Kuchelewa kupata ujauzito

2.Shida kwenye mfumo wa homoni, hali hii kitaalamu inatambulika k**a Polycystic O***y Syndrome (PCOS). hali hii ni ya kawaida sana takribani kwa kila wanawake 10 mmoja wao huwa na hali hii. Miongoni mwa sababu kuu ni kuwa na homoni za kiume nyingi (androgens) na kutokuwa na siku maalumu za kupata hedhi. Hali hii inaweza kuwa na dalili k**a:
A.Kutokwa na damu nyingi sana
B.Kupata hedhi kwa muda mrefu
C.Kuota ndevu ama mwele kuwa nyingi maeneo mbali mbali ya mwili k**a ilivyo kwa wanaume
D.Kuwa na uzito mwingi na usio rahisi kuupunguza
E.Kuota chunusi
F.Kunyonyoka kwa nywele na kukosa afya
G.Kuwa na madoa madoa meusi kwenye ngozi

3.kuwa na uvimbe kwenye kizazi kitaalamu hali hii hutambulika k**a fibroids. Huu I uvimbe usio wa saratani unaoota kwenye tumb la mimba. Unaweza kuwa uvimbe mmoja ama zaidi. Unaweza pia kuwa na uvimbe bila ya kuonyesha dalili zozote hali hii ikichanganyika na maumivu ya chango inaweza kuonyesha dalili kaka:
A.Maumivu ya mgongo kwa chini
B.Maumivu ya miguu
C.Kupata damu nyingi ya hedhi
D.Kupata hedhi zaidi ya wiki
E.Kukosa choo kikubwa
F.Kukojoakojoa mara kwa mara
G.Kushindwa kumaliza mkojo wote.

4.kuwa na maambukizi ama mashambulizi ya bakteria, fangasi ama virusi kwenye kizazi. Kitaalamu hii huitwa Pelvic Inflammatory disease au maarufu k**a PID. Miongoni mwa dalili zake ni:-
A.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
B.Kutokwa na damu kabla ya hedhi na baada ya hedhi
C.Kutokwa na majimaji yanayotoa harufu kwenye uke
D.Maumivu wakati wa kukojoa
E.Homa
F.Kutokwa na damu kidogo kabla ya kuingia hedhi na baada ya kuingia hedhi

5. Maumbile ya kwenye shingo ya uzazi kitaalamu huitwa cervical stenosis, hii ji hali ambayo mlango wa shingo ya kizazi unakuwa ni mdogo sana. Huenda mwanamke amezaliwa ivyo ama mlango umeziba baadaye.

6.kukaza kwa tishu (nyamnyama) za kwenye tumbo la mimba kitaalamu hai hii inatambulika k**a (andenomyosis). hali hii hutokea pale nyamnayma laiki za kwenye tumbo la mimba zinapokuwa ngumu na kubadilika kuwa misuli.

7.matumizi ya baadhi ya njia za kuthibiti uzazi k**a Intrauterine Device (IUD). hiki ni kifaa kidogo kinachowekwa kwenye tumbo la mimba. Kijikifaa hiki mwa wanawake wengine kinaweza kuwaletea shida za kiafya k**a:
A. Maumivu makali wakati wa hedhi
B. Kutokuwa na siku maalumu za hedhi yaani hedhi inaruka ruka
C. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi

NINI NIFANYE KUKABILIANA NA MAUMIVU HAYA
1.fanya mazoezi mara kwa mara
2.Tumia pad zilizo kavu
3.Hakikisha huna stress yaani misongo ya mawazo kupitiliza
4.Oga maji ya moto
5.Tumia dawa za kupunguza maumivu ya chango k**a ibuprofen na acetaminophen
6.Tumia vitamini k**a vitamini B1, na B6, madini ya magnesium na omega-3 fatty acid.

Kadri umri wa mwanamke unavyosogea , Mayai huwa yanapungua kwa Kasi zaidi๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ  Hii inatokea kwa sababu ya utaratibu ulio...
16/10/2024

Kadri umri wa mwanamke unavyosogea , Mayai huwa yanapungua kwa Kasi zaidi๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ Hii inatokea kwa sababu ya utaratibu uliopo wa mayai kupungua na kuzeeka (Oocyte aging) ambao hupelekea kupungua kwa ubora na wingi wa mayai.

Mwanamke mwenye umri mkubwa anaweza akaendelea kupevusha mayai ila akashindwa kupata mimba kutokana na uchovu wa mayai na mayai kukosa ubora๐Ÿค”,

Pia upungufu wa baadhi ya homoni muhimu zinazochochea upatikanaji wa Ujauzito

Hivyo Nafasi ya kubeba ujauzito inapunguaa.

๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ Mwanamke huchukua muda mrefu kushika ujauzito!

๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ Pia uwezekano mkubwa wa Mimba kuharibika ni Mkubwa!

๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ Unaweza kupata zaidi changamoto za wakati wa ujauzito, sukari wakati wa ujauzito, shinikizo la damu la juu, na mimba kuharibika
:

NB : Hayo yote pia yatachangiwa na hali binafsi ya kiafya . Sio wote wanaopitia hizo changamoto ila risk ni kubwa zaidi kwa wale ambao wapo over 35.

USHAURI WANGU๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
K**a huna matatizo ya uzazi ni vyema ukaanza kuzaa mapema!! Walau ukifika miaka 35 uwe umeshazaa hata mara moja!!

Kwako ambaye Bado hujazaa na unamatatizo ya uzazi, basi usikate tamaa endelea kupambana!

Una swali lolote, unahitaji kuwasiliana na Mimi basi nitumie Ujumbe

๐——๐—”๐—Ÿ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐— ๐—œ๐—™๐—จ๐—ฃ๐—” ๐—ก๐—” ๐— ๐—”๐—จ๐—ก๐—š๐—œ๐—ข ๐Ÿ‘‡๐ŸŒฟ Kusagika kwa Pingili za Mgongo๐ŸŒฟ Maumivu Makali ya Kiuno na Mgongo๐ŸŒฟ Mifupa Kusagana๐ŸŒฟ Miguu...
16/10/2024

๐——๐—”๐—Ÿ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐— ๐—œ๐—™๐—จ๐—ฃ๐—” ๐—ก๐—” ๐— ๐—”๐—จ๐—ก๐—š๐—œ๐—ข ๐Ÿ‘‡
๐ŸŒฟ Kusagika kwa Pingili za Mgongo
๐ŸŒฟ Maumivu Makali ya Kiuno na Mgongo
๐ŸŒฟ Mifupa Kusagana
๐ŸŒฟ Miguu Kuwaka Moto
๐ŸŒฟ Kuhisi Ganzi
๐ŸŒฟ Maumivu ya Shingo, Kiuno
๐ŸŒฟ Kukosa Uteute kwenye Magoti
๐ŸŒฟ Kushindwa Kutembea n.k

๐—ฆ๐—”๐—•๐—”๐—•๐—จ ๐—ญ๐—œ๐—ก๐—”๐—ญ๐—ข๐—ฆ๐—”๐—•๐—”๐—•๐—œ๐—ฆ๐—›๐—” ๐— ๐—”๐—ง๐—”๐—ง๐—œ๐—ญ๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—œ๐—™๐—จ๐—ฃ๐—” (๐—ข๐—˜๐—ง๐—˜๐—ข๐—ฃ๐—ข๐—ฅ๐—ข๐—ฆ๐—œ๐—ฆ) ๐Ÿ‘‡
โœ๏ธ Magonjwa ya figo.
โœ๏ธ Upungufu wa hormone za estrogen hii ni kwa wanawake hasa wale wenye (Menopause) kikomo cha hedhi
โœ๏ธ Upasuaji na kuondolewa (ovaries) mayai ya uzazi kwa wanawake
โœ๏ธ Anorexia uzito mdogo kupita kias APA ni kwa wale wanaopenda sana kujinyima kula kupita kiasi wakikwepa kunenepa sana na kufanya mazoezi kupita kiasi.

๐—”๐—ง๐—›๐—”๐—ฅ๐—œ ๐—ญ๐—œ๐—ก๐—”๐—ญ๐—ข๐—ฆ๐—”๐—•๐—”๐—•๐—œ๐—ฆ๐—›๐—ช๐—” ๐—ก๐—” ๐—–๐—›๐—”๐—ก๐—š๐—”๐— ๐—ข๐—ง๐—ข ๐—ญ๐—” ๐— ๐—œ๐—™๐—จ๐—ฃ๐—” ๐—ก๐—” ๐— ๐—”๐—จ๐—ก๐—š๐—œ๐—ข ๐Ÿ‘‡
๐Ÿ€ Mifupa kuvunjika kwa urahisi.
๐Ÿ€ Kupinda Mgongo wakati wa Uzeeni
๐Ÿ€ Maumivu makali ya Mifupa hasa Katika uti wa mgongo, Mabegani, Kifuani na hi

โ˜Ž๏ธ0764933072

๐— ๐—”๐——๐—›๐—”๐—ฅ๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—ง๐—”๐—ง๐—œ๐—ญ๐—ข ๐—Ÿ๐—” ๐— ๐—”๐—ช๐—˜ ๐—ž๐—ช๐—˜๐—ก๐—ฌ๐—˜ ๐—™๐—œ๐—š๐—ข ๐Ÿ‘‡Mawe kwenye figo, yanayojulikana pia k**a mawe ya figo au calculi za figo, ni vij...
16/10/2024

๐— ๐—”๐——๐—›๐—”๐—ฅ๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—ง๐—”๐—ง๐—œ๐—ญ๐—ข ๐—Ÿ๐—” ๐— ๐—”๐—ช๐—˜ ๐—ž๐—ช๐—˜๐—ก๐—ฌ๐—˜ ๐—™๐—œ๐—š๐—ข ๐Ÿ‘‡
Mawe kwenye figo, yanayojulikana pia k**a mawe ya figo au calculi za figo, ni vijiwe vidogo vinavyotengenezwa na madini na chumvi. Madhara ya mawe kwenye figo yanaweza kuwa makubwa na ni pamoja na:

๐Ÿญ. ๐— ๐—”๐—จ๐— ๐—œ๐—ฉ๐—จ ๐— ๐—”๐—ž๐—”๐—Ÿ๐—œ๐Ÿ‘‡
Mawe ya figo yanaweza kusababisha maumivu makali yanayojulikana k**a renal colic. Maumivu haya yanaweza kuwa kwenye mgongo, upande wa tumbo, au kwenye sehemu za chini za tumbo.

๐Ÿฎ. ๐— ๐—”๐—”๐— ๐—•๐—จ๐—ž๐—œ๐—ญ๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—™๐—œ๐—š๐—ข๐Ÿ‘‡
Mawe ya figo yanaweza kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo (UTI), ambayo yanaweza kuenea kwenye figo (pyelonephritis) na kusababisha dalili k**a homa, baridi, na maumivu.

๐Ÿฏ. ๐—ž๐—จ๐—›๐—œ๐—ฆ๐—œ ๐—ž๐—œ๐—–๐—›๐—˜๐—™๐—จ๐—–๐—›๐—˜๐—™๐—จ ๐—ก๐—” ๐—ž๐—จ๐—ง๐—”๐—ฃ๐—œ๐—ž๐—”๐Ÿ‘‡Watu wenye mawe kwenye figo mara nyingi huhisi kichefuchefu na kutapika, hasa wakati mawe yanaposababisha kuziba au maumivu makali.

๐Ÿฐ. ๐— ๐—ž๐—ข๐—๐—ข ๐—ช๐—˜๐—ก๐—ฌ๐—˜ ๐——๐—”๐— ๐—จ๐Ÿ‘‡
Mawe ya figo yanaweza kusababisha mkojo kuwa na damu (hematuria) kutokana na kukwaruza au kujeruhi njia za mkojo

๐——๐—”๐—Ÿ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฉ๐—œ๐— ๐—•๐—” ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ง๐—˜๐—ญ๐—œ ๐——๐—จ๐— ๐—˜ ๐Ÿ‘‡๐Ÿ€ Kukojoa Mara kwa mara.๐Ÿ€ Kubakiza mkojo kwenye kibofu.๐Ÿ€ Kukojoa sana hasa Nyakati za u...
16/10/2024

๐——๐—”๐—Ÿ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฉ๐—œ๐— ๐—•๐—” ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ง๐—˜๐—ญ๐—œ ๐——๐—จ๐— ๐—˜ ๐Ÿ‘‡
๐Ÿ€ Kukojoa Mara kwa mara.
๐Ÿ€ Kubakiza mkojo kwenye kibofu.
๐Ÿ€ Kukojoa sana hasa Nyakati za usiku.
๐Ÿ€ Maumivu wakati wa kukojoa na mkojo usioenda mbali.
๐Ÿ€ Kupungukiwa nguvu za kiume.
๐Ÿ€ UTI ya Mara kwa mara.
๐Ÿ€ Mawe kwenye kibofu kutokana na Mrundikaniko wa Mkojo.
๐Ÿ€ Figo kujaa maji.
๐Ÿ€ Kupoteza fahamu.
๐Ÿ€ Maumivu ya Mara kwa mara ya kiuno kwa nyuma ya mgongo na mapaja.
๐Ÿ€ Uume kushindwa kusimama vizuri.
๐Ÿ€ Kuwa na wakati mgumu wakati wa kukojoa na kuzuia mkojo.

๐—”๐—ง๐—›๐—”๐—ฅ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐—ง๐—˜๐—ญ๐—œ ๐——๐—จ๐— ๐—˜ ๐—ž๐—”๐— ๐—” ๐—›๐—”๐—œ๐—ง๐—”๐—ช๐—”๐—›๐—œ ๐—ž๐—จ๐—ง๐—œ๐—•๐—œ๐—ช๐—” ๐Ÿ‘‡
โœ๏ธ Kushindwa kabisa kukojoa.
โœ๏ธ Kupatwa na maambukizi ya UTI.
โœ๏ธ Kupatwa na vijiwe kwenye kibofu.
โœ๏ธ Uharibifu wa kibofu unaweza kutokea.
โœ๏ธ Figo inaweza kuharibika.
โœ๏ธ Saratani ya Tezi Dume (Prostate Cancer)
โœ๏ธ Kifo ๐Ÿ˜ฅ

๐—ž๐—ช๐—” ๐—ง๐—œ๐—•๐—” ๐—ก๐—” ๐—จ๐—ฆ๐—›๐—”๐—จ๐—ฅ๐—œ ๐—ญ๐—”๐—œ๐——๐—œ
Tembelea Ofisi Zetu Zilizopo Nchi Nzima au Tupigie Sasa Kupitia

โ˜Ž๏ธ0783933072

*"SARATANI YA TEZI DUME(PROSTATE CANCER) & BUSHA"๐Ÿ‘‰ MAANA, VYANZO, DALILI, MADHARA na TIBA.**Tezi dume ni nini?*     Tezi...
16/10/2024

*"SARATANI YA TEZI DUME(PROSTATE CANCER) & BUSHA"๐Ÿ‘‰ MAANA, VYANZO, DALILI, MADHARA na TIBA.*

*Tezi dume ni nini?*

Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa kwa kila mwanaume. Tezi hii ina *kazi ya kutengeneza majimaji meupe mepesi yenye unato kidogo(shahawa)*. Majimaji haya husaidia mbegu za kiume kutembea kwa urahisi.

*Ipo wapi?*

Tezi dume iko *mwishoni mwa kibofu cha mkojo.* Pia inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na na mrija wa mkojo wa uume (urethra) na *iko mbele kidogo ya utumbo mpana ndani ya fupa la nyonga.*

*Ugonjwa wa tezi dume hutokeaje?*

Ugonjwa wa tezi dume maana yake ni tezi dume imepata hitirafu na *hii hutokea pale ambapo chembechembe hai za tezi huasi na kuanza kujigawanya bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili, chembechembe asi hizi mwishowe hutengeneza vivimbe hatari ndani ya tezi dume na hatimaye husambaa mwilini.*

*Somo linaendelea ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡;*

*SABABU 10 ZA MAUMIVU YA KIUNO, NYONGA,CHINI YA KITOVU KWA MWANAMKE.*Haya maumivu yanampata mtu sehemu ya chini ya tumbo...
16/10/2024

*SABABU 10 ZA MAUMIVU YA KIUNO, NYONGA,CHINI YA KITOVU KWA MWANAMKE.*

Haya maumivu yanampata mtu sehemu ya chini ya tumbo na nyonga,. Kwa wanawake maumivu haya yanaweza kua dalili ya matatizo kwenye....

๐Ÿ‘‰Mfumo wa kizazi
๐Ÿ‘‰Mfumo wa haja ndogo
๐Ÿ‘‰Mfumo wa chakula au
๐Ÿ‘‰Mifupa ya nyonga

Maumivu yanaweza kua ya kawaida au makali, ya kudumu ama ya wakati, yaani yanakuja na kupotea kulingana na chanzo cha maumivu hayo.

Wakati mwingine maumivu yanaweza kusambaa kwenye mgongo wa chini kwenye miguu na mapaja. Lakini wakati mwingine yanaweza kuja tu pale unakua unakojoa au kushiriki tendo la ndoa.

*SABABU ZAKE/ CHANZO YA MAUMIVU HAYO*

Maumivu haya yanweza kusababishwa na tatizo moja au zazidi hasa kwa yale humsumbua mtu kwa muda mrefu. Matatizo haya haya huwa k**a ifuatavyo....

๐ŸŠMatatizo kwenye mfumo wa kizazi.

๐ŸŠVivimbe kwenye kuta za tumbo la uzazi.

๐ŸŠHali ya tishu zinazoota ndani ya ukuta wa uzazi(endometriosis) au kuota nje ya ukuta wa mji wa uzazi.

๐ŸŠMaumivu wakati wa hedhi ambayo hutokana na vivimbe katika kuta za tumbo la uzazi.

๐ŸŠMimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy)

๐ŸŠMaumivu yanayotokea upande mmoja chini ya kitovu katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya 14.

๐ŸŠSaratani kwenye mfuko wa mayai.

๐ŸŠMaambukizi kwenye mfumo wa uzazi ambayo hutokana na bakteria wanaosababisha kisonono, na klamidia.
Watu wengi wamekua wakipatwa na magonjwa haya pale wanapojaribu kupata ujauzito bila mafanikio(ugumba) au wanaposumbiliwa kwa mda mrefu na maumivu ya kiuno.

๐ŸŠVivimbe kwenye kuta za kizazi(uterine fibroids) ambavyo hutokana na mvurugiko wa homoni ama kurithi kwa vinasaba.

๐ŸŠMaumivu kwenye via vya uzazi ambayo husababishwa kushindwa kishiriki tendo la ndoa mda mrefu ama kishidwa kukaa kwa muda mrefu.


*SABABU YA MAUMIVU YA MGONGO*
๐ŸMaambukizi katika pingili za uti wa mgongo.mfano saratani ya mifupa

๐ŸKuvunjika kwa pingili za uti wa mgongo. Hii hitokana pale mtu anapo pata ajali.

๐ŸUmri mkubwa.

๐ŸUzito kupita kiasi, hii husababisha mgandamizo na kuelemewa kwa uti wa mgongo.

๐ŸKukaa kwa mda mrefu.mfano madereva,wafanya kazi maofisini.

๐ŸMtindo wa maisha(lifestyle). Mfano kupuuza utumiaji wa mbogamboga na vyakula vya asili hupelekea kuwa na mifupa hafifu na hivyo ni rahisi kuathirika hata kwa msuguano mdogo tu.

โš ๏ธMatibabi ya matatizo haya yanapatikana kutokana na chanzo. Kila tatizo tajwa linatibika kabisa. Ushauri wa haraka ni kutibu tatizo.

16/10/2024

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Gcat hospital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram