16/07/2025
Huyu ndie Jeffery Epstein- Baba wa Makuwadi Duniani...!
"Nimemjua Jeff kwa miaka 15. Anapenda wanawake wazuri wazuri, k**a mimi, lakini yeye nasikia anapenda wasichana wadogo wadogo", hayo yalikuwa maneno ya Donald Trump, Rais wa sasa wa Marekani akizungumza na mwandishi wa Gazeti la New York Times mwaka 2002.
Kuna tofauti kati ya binti mdogo na mwanamke kijana. Jeffery yeye alikuwa wazi kabisa. Alikuwa anapenda vibinti vidogo vidogo. Jeffery alikula mpaka kuku wa dawa. Hiki ndicho kilichomwingiza matatizoni.
Ukiacha yeye mwenye kupenda vibinti vidogo pia alikuwa kuwadi pengine ndie baba wa makuwadi wa dunia hii. Aliwakuwadia wanaume matajiri. Aliwakusanya mabinti wadogo ambao wengi walikuwa hawajatimiza miaka 18 na kuwapa matajiri kula nao raha kwenye jumba lake la kifahari..
Jeffery Epstein ni nani sasa. Jeffery Epstein alizaliwa huko New York, Marekani. Wazazi wake walikuwa Mayahudi. Jeffery alikuwa na kusoma k**a watoto wengine tu. Akaenda chuo Kikuu huko akasoma Fizikia na Hisabati. Jeffery hakumaliza chuo. Akarudi mtaani. Akawa mwalimu wa Hisabati. Baadae mzazi mmoja akavutiwa sana na Jeffery. Akamtafutia kazi kwenye benki ya uwekezaji.
Baada ya miaka kadhaa Jeffery akaanzisha kampuni yake mwenyewe ya usimamizi wa fedha. Hapo ndipo Jeffery akawa tajiri wa kutupwa. Akawa na mihela. Akaanza kutapanya na kujichanganya na matajiri na masupastaa wa Marekani na nje ya Marekani. Mojawapo ya Marafiki zake walikuwa ni Rais Donald Trump, Bill Clinton na Mwana Mfalme wa Uingereza, Prince Andrew. Trump yeye anasema hakuwahi kushiriki kwenye ujinga wa Jeffery Epstein.
Baada ya miaka kwenda mzazi wa binti mmoja wa miaka 14 akalalamika polisi kwamba Jeffery alikuwa amelala na mtoto wake. Polisi walipofanya msako nyumbani kwa Jeffery walikuta picha za mabinti kila mahali.Hapo ndipo matatizo yakaanza. Mashtaka juu ya Mashtaka.
Mwaka 2019 Jeffery alijinyonga akiwa gerezani. Alikuwa akishatakiwa kwa makosa ya kuwafanyisha watoto biashara ya ngono. Jeffery mpaka anafariki hakuwahi kuoa. Aliwahi kuwa katika mahusiano na Miss Sweden pamoja na Ghislaine Maxwell. FBI wamekanusha kwamba Jeffery hakuacha list yoyote yenye majina ya watu aliokua anashirikiana nao..!