afya na dr emanuel

afya na dr  emanuel Afya na Dr Emanuel

  👉🏾Sababu kubwa inayofanya chanzo cha magonjwa mengi kuanzia tumboni ni kwa sababu tumbo (mfumo wa mmeng’enyo) ndicho k...
18/09/2025




👉🏾Sababu kubwa inayofanya chanzo cha magonjwa mengi kuanzia tumboni ni kwa sababu tumbo (mfumo wa mmeng’enyo) ndicho kiini cha kupata virutubisho vinavyojenga na kuendesha mwili wote. Nikieleze hatua kwa hatua:

1. Mfumo wa kinga uko tumboni kwa kiasi kikubwa

Takribani 70–80% ya seli za kinga zipo kwenye utumbo.

Hii inamaanisha ukuta wa utumbo na bakteria wazuri waliopo humo (gut microbiota) ndio walinzi wa kwanza wa mwili dhidi ya vijidudu na sumu. Ukivurugika, kinga inashuka → magonjwa mengi yanapata nafasi.

2. Virutubisho hutoka tumboni

Mwili wote hutegemea chakula kinachovunjwa tumboni ili kupata vitamini, madini, protini, mafuta na wanga.

Ikiwa mmeng’enyo ni mbovu au chakula ni duni, mwili unakosa nguvu na kinga → kusababisha maradhi mbalimbali k**a upungufu wa damu, uchovu, kisukari, nk.

3. Bakteria na usawa wa vijidudu

Utumbo una mamilioni ya bakteria wazuri (probiotics).

Wakipungua au kuharibiwa na vyakula vibaya, dawa (mfano antibiotics), au msongo wa mawazo, hutokea hali inayoitwa dysbiosis → matokeo yake ni magonjwa ya ngozi, akili (mfano depression), mzio (allergies), na hata saratani.

4. Sumu na taka

Ukuta wa utumbo ukiharibika (leaky gut), sumu na vipande vya chakula visivyovunjika vizuri huingia kwenye damu. Hii husababisha mwili kujibu kwa magonjwa ya kinga mwilini (autoimmune diseases) k**a arthritis, kisukari cha aina 1, na mengine.

5. Tumbo lina uhusiano na ubongo (gut-brain axis)

Kuna mawasiliano ya moja kwa moja kati ya tumbo na ubongo kupitia mishipa (mfano vagus nerve).

Hali ya tumbo ikiharibika → huathiri hisia, mawazo, usingizi, hata matatizo ya akili k**a wasiwasi na sonona.


👉 Tumboni ndiko hutokea usawa au machafuko ya afya.
Chakula, mazingira, msongo wa mawazo na maisha yetu huathiri tumbo kwanza, ndipo matokeo yake yanaonekana mwilini mzima.

🙏🏽🙏🏽🙏🏽

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU TUWASILIANE 065513738

 !Tunatoa suluhisho la haraka, salama na la uhakika kwa nguvu za kiume.âś… Salama kwa afya yakoâś… Matokeo ya uhakikaâś… Hudum...
15/09/2025

!
Tunatoa suluhisho la haraka, salama na la uhakika kwa nguvu za kiume.

âś… Salama kwa afya yako
âś… Matokeo ya uhakika
âś… Huduma ya siri na ya heshima

📞 Piga simu: 0695 513 738
đź’¬ WhatsApp: 0761 847 263

đź’Ş !

Ujue ugonjwa wa Homa ya Ini Homa ya ini ni ugonjwa ambao hushambulia na kusababisha ini kuvimba.Baada ya ini kuathirika ...
19/08/2025

Ujue ugonjwa wa Homa ya Ini

Homa ya ini ni ugonjwa ambao hushambulia na kusababisha ini kuvimba.Baada ya ini kuathirika ama hupona lenyewe au unaweza kuwa sugu hivyo kusababi ini kupata makovu, kuharibika na kushindwa kufanya kazi au kansa..

Kuna sababu mbalimbali zinazosabisha mtu kupata homa ya Ini. Virusi vya Homa ya Ini ni chanzo kikubwa cha ugonjwa huu. Sababu nyingine ni pamoja na sumu, pombe, maambukizi, madawa na magonjwa mengine mbalimbali.

Katika makala hii tutaangalia ugonjwa wa homa ya ini unaosababishwa na virusi. Kuna aina 5 kuu za virusi ambavyo vinajulikana k**a aina A, B, C, D na E.

Aina hizi 5 zina umuhimu mkubwa kwa sababu zinasababisha idadi kubwa ya wagonjwa na vifo pia vina uwezo mkubwa wa kusababisha mlipuko na ugonjwa kuenea. Hata hivyo, aina B na C zina uwezo mkubwa wa kusababisha ugonjwa sugu wa ini katika mamilioni ya watu na, pia ndio sababu ya kuu ya ini kuharibika na kupata kansa ya ini.

Virusi vya Homa ya Ini aina A na E(Hepatitis viruses type A and E)
Watu wengi hupata virusi hawa baada ya kunywa maji au chakula kilichochanganyika na kinyesi kutoka kwa watu wenye maambukizi haya. Pia kushiriki mapenzi kinyume na maumbile husababisha mtu kupata maambukizi. Mara chache ugonjwa huu husababisha ugonjwa mkali. Wagonjwa wengi hupona bila madhara yoyote.

Virusi vya Homa ya Ini aina ya B,C na D(Hepatitis viruses types B,C, D)
Mtu anaweza kupata maambukizi ya virusi hivi kwa kugusana na damu, manii au majimaji kutoka kwa mgonjwa. Mtoto anaweza kupata maambukizi kutoka kwa mama yake wakati wa kuzaliwa au kwa wanafamilia. Pia mtu anaweza kupata maambukizi kutokana na kuongezewa damu yenye maambukizi, vyombo vyenye ncha kali na kwa njia ya ngono.

Aina B ya virusi ina chanjo. Chanjo hiyo humkinga mtu pia asipate maambukizi kutoka virus aina D. Lakini Virusi Aina C havina chanjo.

Dalili za ugonjwa
Licha ya kwamba ugonjwa huu unasababishwa na aina tofauti za virusi, dalili zake hufanana. Hata dalili zinaweza kutofautiana kati ya mgonjwa mmoja na mwingine. Baadhi ya dalili hizo za awali ni pamoja na uchovu, homa, kuharisha, maumivu ya tumbo na mwili kuwa na manjano.

Uchunguzi na matibabu
Mgonjwa atafanyiwa vipimo na kuanzishiwa matibabu kulingana na aina na hatua ya ugonjwa wake.
Kwa tiba na ushauri piga simu 0695513738

âš« DALILI ZA PID  (Maambukizi kwenye via vya uzazi)đź§·Uchafu mzito ukeni wa rangi nyeupe au njanođź§·Uke kutoa harufu mbayađź§·Ku...
19/08/2025

âš« DALILI ZA PID
(Maambukizi kwenye via vya uzazi)
đź§·Uchafu mzito ukeni wa rangi nyeupe au njano
đź§·Uke kutoa harufu mbaya
đź§·Kuwashwa sehemu za siri
đź§·maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu
đź§·Uke kuwa mlaini sana
đź§·Maumivu wakati wa tendo la ndoa
đź§·Kuvurugikwa kwa hedhi
đź§·Kutokwa na majimaji ukeni kupita kiasi
đź§·Maumivu wakati wa kukojoa
đź§·Homa/uchovu na kuchoka
đź§·kizungu zungu na n.k

âš« Kwa tiba na ushauri piga
0695513738

SABABU ZA MAUMIVU YA KIUNO NA MGONGO KWA WANAWAKEKUNA sababu nyingi zinazofanya wanawake wengi wasumbuliwe na maumivu ya...
19/08/2025

SABABU ZA MAUMIVU YA KIUNO NA MGONGO KWA WANAWAKE

KUNA sababu nyingi zinazofanya wanawake wengi wasumbuliwe na maumivu ya kiuno mara kwa mara hasa wakati wa hedhi na kuna wengine huugua kwa muda mrefu zaidi ya miezi mitano. Zipo sababu nyingi za kuzuka kwa maumivu haya k**a vile kuwa na matatizo kwenye via vya uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo mkubwa au misuli ya nyonga kuwa na tatizo. Maumivu yanaweza kuwa yanaendana na mzunguko wa hedhi au la, mara nyingi hujitokeza chini ya kitovu na kiunoni.

Sababu ni nyingi ambazo zinaweza kusababisha mwanamke kupata maumivu haya ya kiuno kwa muda mrefu, k**a vile kuwa na maumbukizi ya ndani ya kiuno ya muda mrefu kitaalamu huitwa Chronic Pelvic Infection. Maambukizi haya hutokana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) na huweza kusababisha maumivu ya kiuno.

Sababu nyingine ni kuwa na Endometriosis, hii ni hali ambayo seli za ukuta wa uzazi huota sehemu nyingine za uzazi na itokeapo hivyo basi mwanamke hujikuta akipata maumivu makali wakati wa hedhi au tendo la ndoa. Wengine hupata maambukizi ya muda mrefu ya shingo ya uzazi au mji wa uzazi nayo husababisha maumivu ya kiuno wakati wowote na hasa wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

Wanawake wengine hupata maumivu hayo kutokana na mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi kitaalamu huitwa Ectopic Pregnancy. Baadhi ya wanawake hutokwa na uvimbe mdogomdogo wa kizazi ambao husababisha maumivu pale unapokua kwa haraka na kukandamiza viungo vingine. Maumivu yake huwa ya wakati, huja na kuacha.

Wengine hupata maumivu wakati wa kukojoa kutokana na kuwa na maambukizi kwenye njia ya mkojo ya muda mrefu huku baadhi yao wakipata maumivu baada ya kupata maambukizi ya via vya uzazi kitaalamu huitwa Pelvic Inflammatory Disease – PID au wale wenye maambukizi ya Kibofu cha Mkojo yaani Interstitial Cystitis.

Wale wenye hali hii hupata maumivu hasa chini ya kibofu cha mkojo ambayo hupungua pale anapokojoa na hujikuta akikojoa mara kwa mara na kushindwa kubana mkojo. Lakini pia ugonjwa wa Kidole Tumbo yaani Chronic Appendicitis huleta maumivu upande wa kulia chini ya kitovu ambayo huwa hayatulii na dawa za kutuliza maumivu na wapo wanaougua kiunoni chini ya kitovu kutokana na kuwa na Saratani ya Utumbo Mpana.

Wapo wanaougua kiuno kutokana na kusagika kwa mifupa kwenye maungio yaani Degenerative Joint Disease na hali hiyo inapotokea husababisha maumivu makali maeneo ya kiunoni hasa wakati wa kutembea.

TIBA

Tuwasiliane kupitia simu namba 0695513738

Madhara Makali ya BawasiriBawasiri (au hemorrhoids) ni hali inayoweza kusababisha usumbufu mkubwa, na katika baadhi ya m...
19/08/2025

Madhara Makali ya Bawasiri

Bawasiri (au hemorrhoids) ni hali inayoweza kusababisha usumbufu mkubwa, na katika baadhi ya matukio, madhara makali yanaweza kutokea. Ni muhimu kuelewa madhara haya ili kutafuta matibabu sahihi kwa wakati. Haya ni baadhi ya madhara makali ya bawasiri:

* Kutokwa na Damu Nyingi:
Ingawa kutokwa na damu kidogo ni kawaida kwa bawasiri, baadhi ya watu wanaweza kupata kutokwa na damu nyingi kiasi cha kusababisha upungufu wa damu mwilini (anemia). Hii inaweza kujionyesha k**a uchovu, udhaifu, na rangi nyeupe ya ngozi.

* Maumivu Makali na Uvimbe:
Bawasiri, hasa zile zilizojitokeza nje (external hemorrhoids), zinaweza kuwa chungu sana, hasa wakati wa kukaa au baada ya kujisaidia. Iwapo damu itaganda ndani ya bawasiri (thrombosed hemorrhoid), maumivu huwa makali ajabu na uvimbe mkubwa huonekana. Hali hii inahitaji matibabu ya haraka.

* Kukwama (Prolapse) na Kutokwa Nje Kabisa: Bawasiri za ndani zinaweza kuanza kujitokeza nje ya njia ya haja kubwa wakati wa kujisaidia, na hatimaye kukwama nje kabisa (pr*****ed hemorrhoids). Zinaweza kuendelea kukwama nje hata baada ya kujisaidia, na hii inaweza kusababisha maumivu, usumbufu, na ugumu wa kudhibiti harakati za matumbo.

* Kushindwa Kudhibiti Kinyesi (F***l Incontinence): Katika hali nadra na mbaya, bawasiri kubwa au zilizodumu kwa muda mrefu zinaweza kudhoofisha misuli inayodhibiti njia ya haja kubwa, na kusababisha kushindwa kudhibiti kinyesi au gesi.

* Maambukizi:
Iwapo bawasiri zitapasuka au kuwa na vidonda, zinaweza kuwa lango la bakteria kuingia na kusababisha maambukizi. Dalili za maambukizi ni pamoja na homa, maumivu kuongezeka, na usaha.

* Kufa kwa Tishu (Necrosis) au Gangrene:
Katika matukio machache sana, hasa ikiwa bawasiri iliyokwama nje imekauka damu na kupoteza mzunguko wa damu, tishu zinaweza kufa (necrosis), na kusababisha hali mbaya inayoitwa gangrene. Hii ni dharura ya kimatibabu.

Ni muhimu kuchukua bawasiri kwa uzito na kutafuta ushauri wa daktari mara tu unapohisi dalili, hasa ikiwa unapata maumivu makali, kutokwa na damu nyingi, au dalili zingine za kutisha. Matibabu ya mapema yanaweza kuzuia madhara makali na kuboresha ubora wa maisha yako.

Kwa mawasiliano zaidi tupigie:

0695513738
(WhatsApp//normal call)

15/08/2025
UGONJWA WA P.I.D.PELVIC INFLAMMATIRY  DISEASE  PID.Ugonjwa huu unafahamika k**a  PID, ni maambukizi kwenye via vya uzazi...
05/08/2025

UGONJWA WA P.I.D.

PELVIC INFLAMMATIRY DISEASE PID.
Ugonjwa huu unafahamika k**a PID, ni maambukizi kwenye via vya uzazi wa mwanamke .

• PID ni miongoni kwa magonjwa hatari sana kwa mwanamke una madhara makubwa na unaambukizwa kwa njia ya kujamiiana.
Ugonjwa huu unaweza ukapelekea uharibifu mkubwa kwenye mfuko wa uzazi,mayai ,mirija ya uzazi au sehemu nyingine za uzazi wa mwanamke
Na pia Pid ni moja ya chanzo cha ugumba kwa mwanamke ambacho kinaweza kuzuilika.

•TAKWIMU ZINAONESHA
Kila mwaka,zaidi ya wanawake milioni moja nchini marekani wanapatwa na ugonjwa huu wa PID,
Matokeo yake zaidi ya wanawake 100000 wanakuwa wagumba kila mwaka.
Zaidi ya hayo idadi kubwa ya mimba zaidi ya 100000 inatungiwa kwenye mirija ya uzazi(ectopic pregnancy) inahusishwa na tatizo hilo la PID.
Kiwango kikubwa cha maambukizi ni kwa wasichana wadogo

•VISABABISHI VYA PID
Kwa kawaida mlango wa uzazi (cervix) inazuia bakteria ambao wameingia ukeni wasisambae sehemu zingine za ndani za uzazi
K**a mlango wa uzazi cervix umepatwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana k**a kisonono na/au clamydia
Mlango huo wa uzazi cervix unaathirika na unakuwa na uwezo mdogo
wa kuzuia kusambaa kwa bakteria sehemu za ndani za uzazi.
PID inatokea pale vimelea vya magonjwa vinaposafiri kutoka kwenye mlango wa uzazi cervix kwenda sehemu za juu za uzazi.
Aslimia 90 ya PID husababishwa na kutotibiwa ugonjwa wa kisonono na klamidia
Visababibishi vingine vya pid
👉Kutoa mimba
👉Kujifungua
👉Vipimo kwenye mlango wa uzazi

DALILI ZA PID
zinatofautiana,zinaweza kuwa zifuatazo
👉Maumivu ya tumbo sehemu ya chini au upande wa kulia
👉Kutokwa kwa uchafu ukeni usio wa kawaida wenye rangi ya kijani au ya njano na wakati mwingine una harufu isiyo ya kawaida
👉Kichefuchefu na kutapika
👉Maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Maumivu sehemu ya kulia upande wa juu wa tumbo.

MAMBO YANAYOWEZA KUMUWEKA HATARINI MWANAMKE KUPATA PID

Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinamuweka mwanamke katika hatari ya
kupata PID ni k**a vifuatavyo

1.Wanawake wenye magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana k**a kisonono na klaimidia wako hatarini sana kupata PID
2.Wanawake ambao waliwahi kupata PID wako hatarini kupata tena.

3. Wasichana wadogo wapo hatarini kupata PID kuliko wazee.

4.Wanawake wenye wapenzi wengi wako katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na PID.

Baadhi ya tafiti zinaeleza uoshaji wa uke unachangia kupata PID.Kuosha uke( Douching) kunaweza pelekea kusukuma bakteria sehemu za juu za via vya uzazi na kuzuia kutoka kwa uchafu ambao mwanamke angeweza kutumia k**a ishara ya kwenda kuonana na wataalamu wa Afya mapema.

MADHARA YA PID

Kutokea /kujirudia kwa PID kunaweza kusababisha
kutokea kuharibika mirija ya uzazi ambayo inaweza kupelekea
•Ugumba
•Mimba kutunga kwenye mirija ya uzazi(ectopic pregnancy)
•Maumivu makali kwenye shingo ya kizazi
Kati ya wanawake nane (8) wanaougua PID mmoja(1) unakuwa mgumba

JINSI YA KUJIKINGA NA PID

PID inaweza kuzuilika kabisa ,kisababishi kikubwa cha pid ni magonjwa ya zinaa Mambo ya kuzingatia ili uweze kujikinga na PID
•Epuka kufanya mapenzi na watu wengi
•Tumia njia za uzazi wa mpango(barrier) k**a kondomu
•Tumia spermicides kwa kila tendo la ndoa hata k**a unameza vidonge vya uzazi
•Usitumie IUDs k**a unawapenzi wengi.
Note
IUDs ni vitu vinavyowekwa ndani ya uke kuzuia mimba
•Wahi matibabu ukiona dalili zozote za PID au za magonjwa ya zinaa k**a kuto=
kwa na uchafu usio wa kawaida ukeni,maumivu kiunoni nk
•Pia fanya uchunguzi wa afya ya uzazi mara kwa mara ili k**a kuna tatizo ligundulike na litibiwe kabla halijasambaa kwenda kwenye viungo vya ndani vya uzazi

Kwa kupata tibalishe itakayokuponya moja kwa moja .

PIGA /whatsApp
0695513738
0761847263

DALILI ZA U.T.I, FANGASI SUGU (ILIO SHINDIKANA KUPONA) NA DAWA YAKE MADHUBUTI 1. Kukojoa mara kwa mara.2. Mkojo kuwa na ...
05/08/2025

DALILI ZA U.T.I, FANGASI SUGU (ILIO SHINDIKANA KUPONA) NA DAWA YAKE MADHUBUTI

1. Kukojoa mara kwa mara.
2. Mkojo kuwa na harufu kali.
3. Kusikia kichefu chefu na kupatika.
4. Maumivu ya misuli na tumbo hasa chini ya kitovu.
5. Kusikia maumivu wakati wa kukojoa.
6. Maumivu ya kiuno.
7. Kuwashwa sehemu za siri.
8. Kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana.
9. Kupata vidonda vya ukeni.
10. Kuvimba na kuwa mwekundu kwa mdomo wa inje wa uke.
11. Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri baada ya tendo la ndoa.
12. Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi au mzito au majimaji.

K**a tatizo hili limekua sugu unatumia dawa na haliponi naomba piga simu namba 0695513738 au bip

20/07/2025

HABARI KARIBU

Tunatibu changamoto yoyote iliyoko kwenye mfumo wa uzaz wa mwanamke
* Magonjwa ya zinaa sugu yaani PID
* Hormone imbalance /hupati ute wa uzazi
* fungus za ndani ya kizaz zinazosababisha harufu ukeni
* ukavu ukeni
* Maumivu wakati wa tendo

K**a utapenda upo na changamoto hizo njoo Whatsapp au piga kawaida 0695513738

Magonjwa ya zinaa ndo sababu kubwa Kwa magonjwa sugu k**a PID, UTI sugu , miwasho na Fangasi, uvimbe kwenye kizaziMwanau...
20/07/2025

Magonjwa ya zinaa ndo sababu kubwa Kwa magonjwa sugu k**a PID, UTI sugu , miwasho na Fangasi, uvimbe kwenye kizazi

Mwanaume na mwanamke mnatakiwa kupima mara Kwa mara afya zenu hasa ( Afya ya uzazi ) ili kujiepusha na magonjwa hayo ambyo yamekuwa tishio ulimwenguni

Na k**a ndo mnakutana mara ya kwanza tumie tu kondomu...
Kumpima mwanamke au mwanaume Kwa macho ni kuumizana baadae

Kwa msaada zaidi tupigie simu 0695513738

Address

Kilungule
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when afya na dr emanuel posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram