07/05/2026
Harufu mbaya ya ukeni (hasa ile ya “shombo” k**a samaki 🐟) mara nyingi inaashiria kuna mabadiliko au maambukizi. Hizi ndizo sababu kuu:
1. Bacterial Vaginosis
Hii ndiyo sababu ya kawaida sana.
Hutokea bakteria wazuri wanapopungua na wabaya kuongezeka
Harufu huwa k**a samaki hasa baada ya tendo la ndoa
Mara nyingine huambatana na uchafu mweupe au wa kijivu
2. Maambukizi ya zinaa (STIs)
Mfano: kisonono au klamidia
Husababisha harufu, maumivu au uchafu usio wa kawaida
Huja hasa kwa kufanya ngono bila kinga
3. Kutumia sabuni kali au kemikali ukeni
Kusafisha uke kwa ndani (douching) huua bakteria wazuri
Husababisha harufu mbaya na muwasho
4. Usafi duni wa sehemu za siri
Kubadilisha chupi mara chache
Kutokausha vizuri uke baada ya kuoga
Kutumia chupi zisizopitisha hewa
5. Kusahau kitu ukeni
K**a tampon au kitambaa
Hutoa harufu kali sana isiyo ya kawaida
6. Fangasi (yeast infection)
Mara nyingi huleta muwasho na uchafu mzito
Harufu si kali sana k**a BV, lakini inaweza k