19/06/2025
VIONGOZI WA CHAMA CHA WAUGUZI MNH- MLOGANZILA WAPONGEZWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA NDANI YA MUDA MFUPI TOKA KUCHAGULIWA MWEZI FEBRUARI, 2025.
Viongozi wa Chama Cha Wauguzi Tanzania tawi la MNH-MLOGANZILA wamepongezwa kwa mafanikio makubwa ambayo Chama kimeyapata ndani ya muda mfupi tokea kuchaguliwa kwao kuwa viongozi Mwezi February 2025. Pongezi hizo zimetolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi msaidizi wa huduma za uuguzi na ukunga MNH-MLOGANZILA Bwn. Lukasi Mwaijage akimwakilisha Dr. Deborah Bukuku na kusema kuwa, ndani ya muda mfupi Wanachama wameongezeka kutoka 72 mwezi machi 2025 na kufikia 135 mwezi Juni 2025. Vile vile wamepongezwa kwa kuongeza mapato ya Chama kwa Kasi kubwa na kuweka mipango na mikakati mizuri ya kuendelea kuongeza mapato kwa kubuni miradi mipya ya Maendeleo, kutangaza uuguzi na Wauguzi wa Mloganzila. Hayo yote yamesemwa Leo Juni 19, 2025 katika kikao Cha wanachama na Wauguzi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano (Auditorium) na kuongozwa na viongozi wa Chama hicho.
Aidha, akitoa hali ya Chama, mwelekeo na malengo kwa miezi mingine mitatu ijayo, M/kiti wa Chama hicho Bwn. Amon Kaponda amesema Chama kimejipanga vyema katika kuhakikisha wanachama wanongezeka, mapato ya Chama yanaongezeka na kubuni miradi mipya ya Maendeleo kwa kutumika Kamati ndogo ndogo za Chama ambazo ziliundwa na kwamba zinakamilisha kukusanya maoni na mapendekezo mwezi Juni 2025 na kutakuwa na kikao Cha pamoja Cha kupitia mapendekezo hayo Juni 26, 2025 ili kuyaweka katika utekelezaji.
Vile vile mwanachama wa Chama hicho Bwn. Daniel akichangia katika kikao hicho alisisitiza Wauguzi kupendana na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia malengo makubwa ya Chama hicho.
Paschalina Axwesso
Katibu Mwenezi TANNA MNH-MLOGANZILA
------------------------------
Juni 19, 2025