18/04/2025
MAJI NI UHAI: LAKINI JE UNAYANYWA YA KUTOSHA🤨⁉️
Maji ni sehemu ya kundi la chakula, pia yana umuhimu mkubwa kiafya katika kufanikisha kazi mbalimbali mwilini.
Asilimia 60 ya mwili wa binadamu ni maji, lakini kiasi kikubwa cha maji hupotea mwilini Kila siku kupitia mkojo,kinyesi na jasho.Hivyo basi, ni muhimu kuwa na utaratibu wa kunywa Kiwango cha maji kinachohitajika ili kuuweka mwili katika afya bora.
NI ZIPI FAIDA ZA KUNYWA MAJI YA KUTOSHA❓
🔺Maji husaidia katika uyeyushwaji wa chakula, usafirishaji wa virutubishi na ufyonzaji wa virutubishi mwilini.
🔺Maji husaidia katika kutengeneza maji maji yanayopatikana katika viungo vya mwili k**a vile viwiko na magoti, hivyo husaidia viungo hivyo kufanya kazi.
🔺Maji hurekebisha joto mwilini.
🔺Maji husaidia kuondoa uchafu na mabaki ya uchafu mwilini kwa njia ya jasho na mkojo.
🔺Maji husaidia kupunguza uchovu mwilini.
🔺Maji husaidia kuzuia uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa k**a vile saratani ya tumbo na kibofu cha mkojo, maambukizi ya njia ya mkojo
(UTI) na mawe kwenye figo(renal calculi)
🔺Maji husaidia kuboresha Afya ya ngozi.
NI KIASI KIPI CHA MAJI AMBACHO MTU ANASHAURIWA KUNYWA KWA SIKU ❓
Kiwango cha maji kinachohitajika Kunywewa kwa siku kinatofautiana kutokana na sababu mbalimbali k**a vile umri,jinsia na uzito.
🔺Kwa watu wazima, mwanaume anashauriwa Kunywa maji takriban lita 3.6 kwa siku huku mwanamke akishauriwa Kunywa takriban lita 2.7 kwa siku.
🔺Watoto walioanza kupewa chakula( miezi 6 na kuendelea) wapewe maji kulingana na uhitaji wao.
🔺Watoto Kabla ya miezi sita hairuhusiwi kiafya kupewa chakula na kinywaji chochote zaidi ya maziwa ya mama.
🔺watu wenye uzito mkubwa wanahitaji Kiwango kikubwa zaidi cha maji ukilinganisha na watu wenye uzito mdogo.Ili kupata Kiwango sahihi cha maji (katika lita) kulingana na uzito wako, chukua uzito wako(Kg) gawa kwa 24.
🔺Uhitaji wa maji mwilini pia unaweza kuathiriwa na hali ya afya, hali ya hewa na shughuli za mwili
(Physical activity) k**a vile mazoezi n.k.
ANGALIZO‼️
Usinywe maji mengi kwa wakati mmoja utahatarisha figo zako. Jitahihidi Kunywa maji kidogokidogo.
ZINGATIA
Kunywa maji safi na Salama kulinda Afya yako. Kwani maji yasiyo safi na Salama huweza kusababisha magonjwa k**a typhoid na kipindupindu.
Marejeo:
https://www.medicalnewstoday.com/articles/290814
https://www.tfnc.go.tz/tips/umuhimu-wa-maji-mwilini
https://www.who.int/publications/i/item/9789240045064
https://wa.me/c/255656169598
Usisahau kulike, kuccoment na kushare ili elimu iwafikie watu wengi kwa ujumla.