06/05/2026
Siku figo zako zikifeli, Kuna option mbili tu za kunusuru Maisha yako...🩺
DIALYSIS au KUPANDIKIZWA FIGO... Na Hakuna Option ya Tatu..!
Kabla hujafikia hatua ya kuishi kwa kutegema Mashine ya dialysis, Tafakari haya kwa makini...
→ Unapokunywa maji yenye uchafu, unapokula vyakula vilivyojaa chumvi na kemikali, Unatumia dawa hovyo bila vipimo sahihi, Kunywa pombe N.K
Figo zako huumia, Polepole, Kimya kimya, Bila dalili za Mapema.
Mpaka siku moja... zinakataa kazi kabisa (Kidney failure)
Na hapo...
Maisha yako yanagawanyika mara mbili k**a pasazia la ekaluni...👇
OPTION YA KWANZA NI— DIALYSIS...
Figo zako ni mashujaa wa kimya kimya, Kazi yao Ni...
Kusafisha damu yako, Kuondoa sumu, Kuondoa maji ya ziada, Kila sekunde, Kila dakika, Kila saa.
Fikiria figo inavyofanya kazi 24/7, bila kupumzika hata sekunde moja.
Fikiria inavyochuja lita zaidi ya 180 za damu kwa siku, bila jasho, bila malalamiko....
Lakini zikifeli...?
Mashine ya kuchukua nafasi hiyo inaitwa Dialysis...
Na huu ndio ukweli wake mchungu..
Damu yako inatolewa mwilini kupitia bomba jekundu
Inapita kwenye mashine ya dialysis, ambako uchafu, sumu, na maji ya ziada vinaondolewa
Kisha inarudishwa mwilini kupitia bomba la buluu
Kila session ni masaa manne. Ukiwa umelala au umekaa, Ukiwa umeunganishwa kwenye mashine.
Na si mara moja tu...
↳ Ni mara 3 kwa wiki
↳ Ni masaa 12 kwa mwezi
↳ Ni masaa 48 kwa mwezi
↳ Ni sindano, ni uchovu, ni maumivu, ni gharama... Maisha hayawi k**a mwanzo, Mpira shingoni mpka kufaa kwako....
Sasa tafakari tena…
Figo zako zinapokuwa na afya, hufanya kazi hii mara 36 kwa siku – bila mashine, bila sindano, bila maumivu, bila kukuzuia kuishi maisha yako...👇
OPTION YA PILI NI— KUPANDIKIZWA FIGO...
Ndiyo.... Unaweza kuishi tena kwa figo mpya...
Lakini...
↳ Kupata figo inayolingana si kazi rahisi
↳ Gharama ni kubwa mno
↳ Kuna hatari ya mwili kukataa figo mpya
↳ Pamoja na kupandikiza figo, Unakuwa kwenye dawa za kinga ya mwili maisha yako yote...
Na
Si kila mtu hupata nafasi hii, Wengi hupoteza maisha wakisubiri msaada huo.....
Sasa jiulize... Je, unazitunza figo zako kwa kweli..?
↳Unakunywa maji ya kutosha?
↳Unapunguza chumvi na vyakula vya kusindikwa?
↳Unapima presha yako mara kwa mara?
↳Unakagua mkojo wako?
↳Unakimbilia dawa hovyo hovyo bila ushauri wa kitaalamu?
NB: Usisubiri hadi mashine ichukue nafasi ya figo zako....
Usisubiri hadi sindano zigeuke kuwa maisha yako ya kila wiki...
Usisubiri hadi U*i, mwingine uwe wa kuomboleza...
TUNZA FIGO ZAKO. NI UHAI WAKO, POMBE SIO SIFA🫵