18/06/2025
Lijue tatizo la presha kuwa juu wakati wa ujauzito.
Shinikizo la damu ni ile nguvu ambayo moyo wako unatumia kusukuma wakati damu inapopita kwenye mishipa ya damu. Wakati mwingine moyo utahitaji nguvu kubwa kusukuma damu katika mishipa ya mwili. Hali hii inapotea unakuwa na shinikizo la damu linakuwa juu. Hapa ndipo utaambiwa una ugonjwa wa shinikizo la juu la damu ambayo kwa kitaalam inaitwa hypertension au kwa lugha yenu huko mtaani inaitwa presha ya kupanda.
Je ni wakati gani presha inakuwa juu
Presha inapopimwa majibu yake huwa katika namba ya juu na ya chini(A/B). Sasa utaambiwa una presha ya kupanda iwapo namba ya juu itakuwa zaidi ya 140 au zaidi na namba ya chini iko zaidi 90 au zaidi.
Shinikizo la damu la kawaida huwa kati ya mmHg 90/60 ( ‘milimita tisini kwa sitini’ za zebaki,) na chini ya mmHg 140/90 (‘milimita mia moja arubanini kwa tisini’ za zebaki). Kawaida presha huwa haiongezeki sana wakati wa ujauzito.
Madhara ya kuwa na presha ya kupanda wakati wa ujauzito
Ukipata tatizo la presha ya kupanda wakati wa ujauzito maana yake ni kwamba moyo unatumia nguvu kubwa kusukuma damu. Hivyo basi unaweza kupata madhara yafuatayo
▪︎Kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo.
▪︎ Kujifungua njiti,
▪︎Mtoto kufia tumboni,
▪︎Mama anaweza kupata matatizo ya figo,
▪︎Kondo la nyuma kuachia kabla ya kujifungua hivyo kuvuja damu nyingi
▪︎ Kupata kiharusi(stroke).
▪︎Kupata magonjwa ya moyo
Ufanye nini?
▪︎Hakikisha unahudhuria clinic
▪︎Iwapo umegundulika kuwa na presha ya kupanda tumia dawa utakazopewa.
▪︎Fanya mazoezi
▪︎Kula mlo kamili
▪︎Punguza matumizi ya pombe na sigara
Wasiliana nami wa.me/255683822021