11/08/2023
FAHAMU KUHUSU U.T.I NA FANGASI SUGU.
U.T.I na fangasi ni tatizo kubwa ambalo huwapata wanawake wengi duniani mara kwa mara. Husababishwa na bakteria anaitwa E. coli ambaye huwa wanaishi kwenye utumbo mnene sehemu za tundu la haja kubwa, mwanamke anaambukizwa kirahisi sababu anapokuwa anachuchumaa kwenye haja kubwa au ndogo.
Madhara yake kwenye kibofu cha mkojo baada ya kuwa wengi wanahamia mwenye figo, ndio maana leo hii wanawake wengi wanaumwa figo. Figo zao zimeharibika sababu ya U.T.I. na kufa kifo cha ghafla.
MIWASHO.
Kawaida mwanamke ana ulinzi ukeni kwake, yaani bakteria wazuri wanaishi kule kwa ajili ya kulinda uke, japo pia bakteria wabaya wanaishi kule lakini kwa uwiano, ya kwamba wale wazuri wanakuwa wengi ,kuliko wabaya . Sasa ikitokea kwamba wale bacteria wabaya wakawa wengi, hapo ndio utaona miwasho kwa mwanawake haishi kujikuna mara kwa mara.
FANGASI.
Inasababishwa na jamii ya fungi anaitwa CANDIDA. Seli za fangasi na bacteria wazuri huishi ukeni bila tatizo lolote.Tatizo linakuja endapo ukuaji wa fangasi hawa ukeni watakuwa wengi kushinda wazuri. Basi hapo ndio inapotokea ugonjwa wa fangas na miwasho mingi.
DALILI ZA U.T.I
1. Kukojoa mara kwa mara.
2. Mkojo kuwa na harufu kali.
3. Kusikia kichefu chefu na kupatika.
4. Maumivu ya misuli na tumbo hasa chini ya kitovu.
5. Kusikia maumivu wakati wa kukojoa.
6. Maumivu ya kiuno.
7. Kuwashwa sehemu za siri.
8. Kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana.
9. Kupata vidonda vya ukeni.
10. Kuvimba na kuwa mwekundu kwa mdomo wa inje wa uke.
11. Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri baada ya tendo la ndoa.
12. Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi au mzito au majimaji.
VISABABISHI VYA FANGASI.
1. Mabadiliko ya homoni katika kipindi cha upevushwaji wa mayai kwa mwanamke kipindi cha ujauzito, utumiwaji wa uzazi, wa mpango na kukoma kwa hedhi.
2. Upungifu wa kinga mwilini: Mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini k**a vile mwenye kuugua kansa, ukimwi, magonjwa mbalimbali yenye kupunguza kinga ya mwili.
3. Kukosa usingizi stress, vidonda sehemu za siri,matumizi ya antibiotics, kuweka marashi sehemu za siri.
4. Watu wanaougua kisukari ambao hawawezi kudhibiti kwa kutumia dawa za kisukari, inakuwa kwenye damu na hicho kisukari ndiyo chakula kikuu cha hao fangasi.
Hata wanawake ambao wanapenda kula vyakula vya sukari nyingi k**a vile chocolates, soda, na vingine vyenye sukari nyingi ambavyo ni chakula cha fangasi.
5. Mazingira ya joto hii inamaanisha nguo ambazo tunatakiwa kuvaa k**a vile chupi za cotton hasa kwa wanawake, hazihitaji joto sababu bacteria wabaya wanakuwa wengi sana na kusababisha miwasho na FANGAS
6. Kondomu na mbegu za kiume huharibu hali ya asidi iliyopo ukeni ambayo ni ya muhimu sana maana inasaidia kukinga uke usiingiliwe na bacteria wabaya.
MADHARA MAKUBWA YA FANGASI NA U.T.I.
Kupatwa kwa ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) maambukizi katika via za uzazi na kupelekea kuwa ngumba, ndio maana wanawake wengi ni wagumba.
➡Kupata maambukizi ya mara kwa mara
➡Kupata uharibifu wa figo wa kudumu na kuhitaji huduma maalumu ya kutibu figo (dialysis).
➡Kutokea uwezekano wa kuzaa watoto wenye uzito mdogo au wanaozaliwa kabla ya wakati.
➡Wanaume wanaougua UTI mara kwa mara wanakuwa kwenye hatari ya kupata madhara kwenye tezi dume (prostatitis).
➡Uvimbe huweza kutokea kwenye tezi dume na kusababisha maumivu wakati wa haja ndogo au kutoa shahawa.
➡Sumu katika damu. Mara chache huweza ikatokea kuwa bakteria wakasambaa kutoka ndani ya figo na kuingia kwenye mfumo wa damu (sepsis) na baadaye kusambaa hadi kwenye viungo vingine muhimu vya mwili. Hali hii ikitokea, itabidi mgonjwa awekwe chini ya uangalizi mkali wakati akipewa tiba ya kuwaua bakteria hao.
➡Kuharibika kwa mimba (Miscarriage)
➡Maumivu ya misuli na tumbo
SULUHISHO LA WENGI.
Watu wengi wanapokuwa na U.T.I huenda kupewa antibiotics ambazo huenda kuua bakteria wazuri na matokeo yake baada ya muda U.T.I inarudi kwa kasi sana.
USISUBILI HADI MADHALA YAWE MAKUBWA FUNGUS NA U.T.I INATIBIKA
Kwa mawasiliano kupata ushauri,maswali na matibabu nitafute kwa +255692 524 186 whatsapp/txt na calls