05/12/2025
PID ni kifupi cha Pelvic Inflammatory Disease, kwa Kiswahili huitwa Ugonjwa wa Maambukizi ya Ukeni na Sehemu za Ndani ya Uzazi. Ni maambukizi yanayoathiri mlango wa uzazi (cervix), mji wa mimba (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes), na wakati mwingine mashikio ya mayai (ovaries).
Ni tatizo linalotokea pale bakteria wanaoingia kupitia uke wanapofika juu kwenye mfumo wa uzazi.
Sababu za PID
PID mara nyingi hutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, hasa:
1. Klamidia (Chlamydia trachomatis)
Hii ndiyo inayoongoza kusababisha PID.
2. Kaswende ya bakteria gonorrhea (Neisseria gonorrhoeae)
Husababisha PID kwa kasi na huweza kuleta uharibu mkubwa ndani ya mirija.
3. Bakteria wengine wa kawaida ukeni
K**a flora wa uke wanapobadilika (bacterial vaginosis), wanaweza kuingia juu na kusababisha PID.
4. Kuingiza kitu kwenye uke bila usafi
Vipandikizi k**a IUD wakati wa kuwekwa
Kufanya uchunguzi wa uzazi bila kuchukua tahadhari
Kutumia vifaa vya kuingiza ukeni visivyo safi
5. Kuwa na wapenzi wengi au kutojikinga
Huongeza uwezekano wa kupata STIs, hivyo kuongeza hatari ya PID.
Madhara ya PID
PID ikiachwa bila kutibiwa inaweza kusababisha matatizo makubwa:
1. Kuziba kwa mirija ya uzazi
Husababisha ugumu wa kupata mimba (infertility).
2. Mimba kutunga nje ya kizazi (Ectopic pregnancy)
Mirija ikiziba, kiinitete hushindwa kupita hadi kwenye mji wa mimba.
3. Maumivu sugu ya tumbo la chini
Yaweza kudumu miezi au miaka kwa sababu ya makovu (scar tissue).
4. Majipu kwenye mirija na ovari (Tubal-ovarian abscess)
Hali hii ni hatari na inaweza kuhitaji upasuaji.
5. Kuenea kwa maambukizi mwilini
Katika hatua mbaya, bakteria wanaweza kuingia kwenye damu (sepsis), hali inayotishia maisha.
Dalili za PID
👉Maumivu ya tumbo la chini
👉Kutokwa na uchafu mwingi au unaonuka
👉Maumivu wakati wa kujamiiana
👉Homa na baridi
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Kutokwa damu bila mpangilio