30/11/2025
UKISIKIA HERNIA JUA HAYA, INAKUPASA UOGOPE
Hernia au Ngiri ni hali inayotokea pale ambapo kiungo au nyama ya ndani ya mwili inatokea nje kupitia pengo au udhaifu uliopo kwenye misuli ya tumboni.
Kwa lugha rahisi: ni k**a ukuta wa mfuko kupasuka kidogo, halafu kitu cha ndani kinajitokeza.
DALILI ZA HERNIA (NGIRI)
Mtu mwenye ngiri mara nyingi anaweza kuona au kuhisi:
Uvimbaji kwenye sehemu ya tumbo au kinena (unene wa upande wa chini ya tumbo).
Maumivu yanayoongezeka ukibeba vitu vizito.
Kukaza tumbo au kiuno unapojikaza chooni.
Kuvimbiwa mara kwa mara.
Uvimbaji kutoweka ukiwa umelala na kurudi ukiwa umesimama.
SABABU ZINAZOCHANGIA KUPATA HERNIA
Hernia inaweza kusababishwa na mambo haya:
Kuinua vitu vizito kupita kiasi.
Kujikaza chooni kwa muda mrefu (constipation).
Kukohoa sana kwa muda mrefu.
Uzito mkubwa / kitambi.
Kuwa na misuli dhaifu ya tumbo (kwa mfano kwa wazee).
Kuwa na jeraha au upasuaji wa zamani tumboni.