18/12/2025
MAJANI YA MPERA NA MAAJABU YAKE
Majani ya mpera ni miongoni mwa tiba asilia zilizotumika kwa muda mrefu katika jamii zetu kutokana na virutubisho na kemikali asilia zinazopatikana ndani yake. Yafuatayo ni baadhi ya matumizi na faida zake:
1. Chai inayotengenezwa kwa majani ya mpera husaidia kupunguza matatizo ya kifua pamoja na kikohozi cha mara kwa mara.
2. Majani ya mpera yakioshwa na kusagwa vizuri hutumika kupaka kwenye ngozi yenye muwasho unaosababishwa na mzio (allergy).
3. Unywaji wa chai ya majani ya mpera husaidia kudhibiti kiwango cha mafuta (cholesterol) kilichozidi mwilini.
4. Kwa watu wenye changamoto ya sukari, chai ya majani ya mpera imekuwa ikitumika kusaidia kusawazisha kiwango cha sukari kwenye damu.
5. Majani ya mpera pia yanatajwa kusaidia wanaume wanaokumbana na changamoto za nguvu za kiume.
6. Yakisagwa na kuchanganywa na maji kidogo, majani haya hutumika k**a scrub ya asili ya kusafisha uso na kuondoa uchafu uliojificha kwenye ngozi.
7. Chai ya majani ya mpera ni msaada mzuri kwa watu wanaosumbuliwa na kuhara au tumbo kujaa gesi.
8. Kwa majeraha madogo, majani ya mpera yaliyosagwa yanaweza kupakwa ili kupunguza maumivu na kusaidia kuzuia maambukizi ya bakteria.
9. Majani haya yakisagwa na kupakwa kwenye sehemu iliyoumwa na mdudu husaidia kupunguza maumivu na muwasho.
10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kusaidia katika matatizo yanayohusiana na tezi dume.
11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi, majani ya mpera husaidia kupunguza chunusi na kuboresha afya ya ngozi.
12. Chai ya mpera husaidia kupunguza uzito wa mwili na kuboresha matumizi ya sukari ndani ya mwili.
13. Kwa watu wenye tatizo la nywele kukatika au kupungua, majani ya mpera yakichemshwa na maji yake kupakwa kichwani husaidia kuimarisha na kurefusha nywele.
14. Tafuna majani mabichi ya mpera ikiwa unasumbuliwa na maumivu ya jino, vidonda vya ufizi au harufu mbaya mdomoni.
15. Majani ya mpera yakisagwa laini na kutumika k**a scrub husaidia kupunguza dalili za ngozi kuzeeka mapema.
16. Chai ya mpera husaidia kutuliza mvurugiko wa tumbo na maumivu ya ndani ya tumbo.
Mbali na majani, juisi ya tunda la pera imekuwa ikitumika kusaidia matatizo k**a bawasiri, afya ya figo na kupunguza mafuta kwenye moyo. Kwa ujumla, karibu kila sehemu ya mti wa mpera ina matumizi ya kitabibu, ikiwemo mizizi yake ambayo ikichemshwa husaidia wanawake wenye changamoto za hedhi au kutokwa na majimaji yenye harufu sehemu za siri.
17. Majani ya mpera husaidia kuzuia kukatika kwa nywele. Chemsha majani, acha yapoe, kisha yapake kichwani na kuyasugua taratibu kwa dakika 15. Acha kwa dakika 30 kisha osha kwa maji safi bila sabuni. Fanya mara tatu kwa wiki.
18. Kwa lengo la kupunguza uzito, kunywa chai ya majani ya mpera mara kwa mara k**a sehemu ya mtindo bora wa maisha.
NAMNA YA KUTUMIA MAJANI YA MPERA
Njia ya Kwanza
Chemsha maji glasi nne kwa dakika 15–20 mpaka yatokote. Chukua majani ya mpera 10–15, yaweke kwenye maji ya moto, funika na uache kwa dakika 10–15. Koroga, chuja, chai iko tayari.
Njia ya Pili
Weka majani ya mpera moja kwa moja kwenye maji na yachemshe kwa dakika 15–20. Yakishatokota, ondoa kwenye moto, acha kwa dakika 10–15 kisha chuja.
Unaweza pia kutumia majani yaliyokauka na kusagwa; tumia kijiko kimoja cha chakula kwenye maji ya moto.
👉 Ushauri: Changanya chai ya majani ya mpera na asali mbichi badala ya sukari ili kuongeza ufanisi wake.