21/01/2026
PID ni maambukizi kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke, hasa kwenye mfuko wa uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari.
Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa k**a kisonono (gonorrhea) na klamidia (chlamydia) yasipotibiwa mapema.
🔴 Dalili za PID
Mwanamke anaweza kuwa na:
Maumivu ya tumbo la chini au kiuno
Kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu mbaya
Maumivu wakati wa kujamiiana
Homa
Kutokwa damu isiyo ya kawaida
Maumivu wakati wa kukojoa
Hedhi zisizo za kawaida
⚠️ Wengine hawana dalili kabisa, lakini maambukizi yanaendelea kuharibu mfumo wa uzazi.
🔥 Madhara ya PID
K**a PID haitatibiwa mapema, inaweza kusababisha madhara makubwa k**a:
1️⃣ Ugumba (kutopata mimba)
Maambukizi huharibu mirija ya uzazi na kuzuia yai kufika kwenye mfuko wa uzazi.
2️⃣ Mimba nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy)
Mirija ikiharibika, yai linaweza kushindwa kufika tumboni. Hii ni hatari sana kwa maisha.
3️⃣ Maumivu ya tumbo ya muda mrefu
Makovu ndani ya mfuko wa uzazi husababisha maumivu yasiyoisha.
4️⃣ Majipu (abscess)
PID inaweza kusababisha uvimbe wenye usaha kwenye ovari au mirija ya uzazi.
5️⃣ Kuongezeka kwa hatari ya PID kurudia tena
Ukishawahi kupata PID, uwezekano wa kuipata tena unaongezeka.
🛡️ Jinsi ya Kujikinga
Tumia kondomu kila mara
Pima magonjwa ya zinaa mara kwa mara
Tibu maambukizi ya ukeni mapema
Epuka kuwa na wapenzi wengi
Mpenzi wako pia apimwe na kutibiwa
📌 Ushauri Muhimu
PID inatibika ikiwa itagunduliwa mapema.
Ukiona dalili zozote nilizotaja, ni muhimu kumwona daktari haraka kwa vipimo na matibabu zaidi wasiliana nami 0796104434